Ni mnyama au mdudu gani akiingia chumba huwa unakosa amani?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,691
7,499
Kila mtu hata kama ni jasiri kiasi gani lazima kuna kitu atakuwa anakiogopa tu. Hitler mwenyewe aliogopa mtihani. Katika mazingira yalituzunguka tunaishi na viumbe hai wengi yaani mimea na wanyama wa aina mbalimbali.

Haijalishi ni nyumba ya aina gani unaweza kushangaa mdudu au mnyama usiyempenda amezama chumbani. Mfano Nyoka kwangu mimi ni kiume hatari kutokana na wale wenye sumu kuua watu.

Nyoka wenye sumu unaweza kuwatambua kwa umbo la kichwa yaani kilicho pembetatu (venomous). Huwa wana sumu mbalimbali mf. Inaoingia kwenye moyo ambapo kwa kitaalam huitwa cardiotoxic snake.

Kimsingi kama siwezi kumua huwa naishiwa hamu hadi nitafute diesel au mafuta ya taa (kerosine/ paraffin) ni mwage humo ndani kwa sababu hawa viumbe wanachukia sana harufu ya mafuta ya taa na diesel.

Wapo viumbe wengi wakiingia ndani huwataki na sijajua unatumia njia gani kuwaondoa, karibu utujuze tupeane mbinu za kupambana na hawa viumbe. Asante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom