Ni mwaka wa sita sasa sijala vitumbua nilijiapiza sitokula vitumbua tena kwa kile nilichokiona

yule mama akikubadilishia menu akakuwekea maandazi utakula?au vitumbua vikipikwa hapo home kwako hutakula?manake naona specifically una hasira na vitumbua.
 
Kama Unaishi Tanzania, mambo kama Hayo ni vigumu kuguarantee kuwa hutakutana nayo maana hata mkeo huwezi kujua huwa anafanya nini na chakula anachokutengea, mama yako wa kambo, housegirl wako anaewaandalia chakula watoto wako na familia yako yote nae hujui anafanya nini na hicho chakula kabla hamjakila.
 
sijawadharau wauza vitumbua.
na wala sijamkejeli yeyote.
nimeeleza tu experience niliyokutana nayo.
na wala sijasema wauza vitumbua ni miyeyusho
nimejiapiza tu mwenyewe hamu tu imeniondokea,kuna vitu mtu akiviona kumbukumbu humjia na sijasema pahala popote kuwa vitumbua ni vibaya la hasha,usinielewe vibaya
Tatizo liko wapi wewe,wakati kuna watu wanazama humo bila ya kinyaa?
 
Mkuu sio huyo mama tu,mama ntilie wengi,wapika vitafunwa na migahawa mingi ina vituko sana.Mimi sili kabisa magengeni na migahawani mkuu.Nilishashuhudia mama ntilie akikojolea chai,sina hamu mkuu.
Ni miaka 6 sasa imepita sijala vitumbua hivyo ladha ya vitumbua nimeshaisahau.
nilijiapiza sitokula tena vitumbua kwa kile nilichoki shuhudia.

mwaka 2010 nilikuwa naishi na mjomba wangu katika moja ya maeneo.
na huyo mjomba wangu alikuwa mpenzi sana wa vitumbua na uzuri ni
kwamba pale mtaani tunapoishi jirani yetu alikuwa anapika vitumbua hivyo watu asubuhi hukusanyika kwake kibarazani na kununua vitafunwa hivyo.

Mjomba wangu huwa ni mtu anayeswali hivyo saa kumi na moja alfajiri huamka na mara nyingi anapoelekea msikitini hupitia kwa yule mama muuza vitumbua na humpa maelekezo namna vitumbua vyake vipikwe ''huyu mjomba wangu huwa anapenda vitumbua vyake viwekwe hiriki na abdalasini'' kwahiyo yule mama huwa anatenga vitumbua kadhaa labda vitano ambayo huweka viungo hivyo kwaajili ya mjomba wangu,mara nyingi humpitia yule mama ili kumkumbusha tu asije kusahau na ukizingatia yule mama nyumba anapoishi ni jirani na kwetu.

Nakumbuka ilikuwa kipindi ambacho usiku ni mfupi hivyo jua huwahi kuchomoza,kama kawaida mjomba wangu huyo kaamka alfajiri aelekee kuswali msikitini na aliniamsha sababu ilitakiwa niwahi chuoni sababu ya Cat 2 kwahiyo nilimhimiza aniamshe mapema saa kumi na moja ili niweze kupata muda wa kuperuzi na kujiandaa,sasa mjomba wangu huyo akaniomba niende kwenye ile nyumba nimpe maelekezo yule mama ''siyo kila siku anapewa maelekezo sababu kuna baadhi ya siku huwa hanunui vitumbua sasa siku hiyo alikuwa ana uhitaji wa vitumbua''.

maelekezo huwa anampa mapema sababu mjomba huyu huwa anaenda kazini mapema hivyo huwa anapikiwa vitumbua mwanzo kabisa na mida kama ya saa kumi na mbili na nusu au saa moja kasoro huwa anavipata na kuchangamsha tumbo lake kabla ya kuelekea kazini

sasa nimeenda kwenye ile nyumba kuna mlango huwa upo wazi,ni kawaida kwa mida hiyo mlango huo kuwa wazi nikausukumiza nilicho shuhudia sikukiamini kabisa.Yule mama muuza vitumbua yupo uchi kanga ipo pembeni ananyunyuzia maji kwenye uchi wake kisha yale maji yanaingia kwenye beseni la vitumbua,ni kama mithili ya mtu anayetawadha...nilipigwa na butwaa na mshangao sasa wakati nageuza yule mama akastuka akaniona.Kufika nyumbani nikamsimulia mjomba nilichokiona .

Aliniuliza mara mbili mbili akidhani namtania ,kama ni kweli nikamuambia uhakika kwa macho yangu mawili nimemuona akifanya hivyo,kwa hasira mjomba alitaka kwenda kumvamia yule mama nikamtuliza lakini alienda kumchana laivu yule mama asubuhi yake.


Tokea hiyo siku huyo mjomba wangu yeye na vitumbua ni kama panya na paka wakati alikuwa mpenzi sana wa vitumbua,na mimi hapa tokea 2010 mpaka leo hii sijatia kitumbua mdomoni kwangu kila nikitaka kula navuta picha tukio la yule mama akinyunyuzia maji kwenye uchi wake kisha yale maji yanaingia kwenye beseni ya unga wa vitumbua.


yule mama kwa aibu aliondoka pale mtaani alihama kabisa.





View attachment 449927 View attachment 449929 View attachment 449927
 
unachokiongea wapo watakaobeza lakin mimi nimeshuudia kwa kusikia mtaan kwetu marafiki wawili watu wazima waligombana wakaanza kutoleana siri zao mmoja alisema maandaz yako si unaoshea maji ya uchi ndio maana yanapendwa nae alimjibu kwa kashfa kua mbona we ni mwanga

maandazvya huyo mama yalikua yanapendwa sana
 
ahaaaaaaa.....kweli mkuu ndo mana mim mwenyewe nilikuwa nikila vitumbua vya yule mama nakuwa na hamu ya ''kubaka''..........nshajua sirudiii tena............
 
Mbona hata gongo huchujwa kwa kutumia chupi ya mwanamke, ila wenzetu wanaisifia balaa.
 
Niliwahi kusikia kama unga wa vu.tu unafanya chakula kiwe kitamu
Mna-hide sana maelezo yenu saazingine! Sasa "unga wa vu.tu ndiyo nini? Waweza kuwa na sentensi bora ya kuelimisha na kuburudisha, ila kwa uandishi wa kufichaficha huu, unapoteza maana.
 
Mimi napiga tuu ninavyovipenda kwanza huyo anaepika tunamuona
 
Uko SWA mkuu kwa kile ulichokiona lazima utujuze na sisi tujue hayo mambo yanafanyika kabisa wala si masihara.
 
Ukifikiria sana jinsi vyakula vinavyotengenezwa mahotelini,migawahani na mtaani utokula kabisa na wakati mwengine hutashindwa kula kwa jirani au nduguyo
 
Back
Top Bottom