Ni mwaka wa sita sasa sijala vitumbua nilijiapiza sitokula vitumbua tena kwa kile nilichokiona

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
439
1,000
Ni miaka 6 sasa imepita sijala vitumbua hivyo ladha ya vitumbua nimeshaisahau.
nilijiapiza sitokula tena vitumbua kwa kile nilichoki shuhudia.

mwaka 2010 nilikuwa naishi na mjomba wangu katika moja ya maeneo.
na huyo mjomba wangu alikuwa mpenzi sana wa vitumbua na uzuri ni
kwamba pale mtaani tunapoishi jirani yetu alikuwa anapika vitumbua hivyo watu asubuhi hukusanyika kwake kibarazani na kununua vitafunwa hivyo.

Mjomba wangu huwa ni mtu anayeswali hivyo saa kumi na moja alfajiri huamka na mara nyingi anapoelekea msikitini hupitia kwa yule mama muuza vitumbua na humpa maelekezo namna vitumbua vyake vipikwe ''huyu mjomba wangu huwa anapenda vitumbua vyake viwekwe hiriki na abdalasini'' kwahiyo yule mama huwa anatenga vitumbua kadhaa labda vitano ambayo huweka viungo hivyo kwaajili ya mjomba wangu,mara nyingi humpitia yule mama ili kumkumbusha tu asije kusahau na ukizingatia yule mama nyumba anapoishi ni jirani na kwetu.

Nakumbuka ilikuwa kipindi ambacho usiku ni mfupi hivyo jua huwahi kuchomoza,kama kawaida mjomba wangu huyo kaamka alfajiri aelekee kuswali msikitini na aliniamsha sababu ilitakiwa niwahi chuoni sababu ya Cat 2 kwahiyo nilimhimiza aniamshe mapema saa kumi na moja ili niweze kupata muda wa kuperuzi na kujiandaa,sasa mjomba wangu huyo akaniomba niende kwenye ile nyumba nimpe maelekezo yule mama ''siyo kila siku anapewa maelekezo sababu kuna baadhi ya siku huwa hanunui vitumbua sasa siku hiyo alikuwa ana uhitaji wa vitumbua''.

maelekezo huwa anampa mapema sababu mjomba huyu huwa anaenda kazini mapema hivyo huwa anapikiwa vitumbua mwanzo kabisa na mida kama ya saa kumi na mbili na nusu au saa moja kasoro huwa anavipata na kuchangamsha tumbo lake kabla ya kuelekea kazini

sasa nimeenda kwenye ile nyumba kuna mlango huwa upo wazi,ni kawaida kwa mida hiyo mlango huo kuwa wazi nikausukumiza nilicho shuhudia sikukiamini kabisa.Yule mama muuza vitumbua yupo uchi kanga ipo pembeni ananyunyuzia maji kwenye uchi wake kisha yale maji yanaingia kwenye beseni la vitumbua,ni kama mithili ya mtu anayetawadha...nilipigwa na butwaa na mshangao sasa wakati nageuza yule mama akastuka akaniona.Kufika nyumbani nikamsimulia mjomba nilichokiona .

Aliniuliza mara mbili mbili akidhani namtania ,kama ni kweli nikamuambia uhakika kwa macho yangu mawili nimemuona akifanya hivyo,kwa hasira mjomba alitaka kwenda kumvamia yule mama nikamtuliza lakini alienda kumchana laivu yule mama asubuhi yake.


Tokea hiyo siku huyo mjomba wangu yeye na vitumbua ni kama panya na paka wakati alikuwa mpenzi sana wa vitumbua,na mimi hapa tokea 2010 mpaka leo hii sijatia kitumbua mdomoni kwangu kila nikitaka kula navuta picha tukio la yule mama akinyunyuzia maji kwenye uchi wake kisha yale maji yanaingia kwenye beseni ya unga wa vitumbua.


yule mama kwa aibu aliondoka pale mtaani alihama kabisa.

kkitu.jpg
vitumbua.jpg
kkitu.jpg
 

Attachments

Nussayr

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
242
250
Pole sana na Hongera kwa Kutimiza miaka sita bila kula Vitumbua. Daah miaka sita yote umechelewa kutuambia.
Kuna vitu ukijivua nikujitia Stress tu
Hasa hii migahawa tunayokula siku za kazi.
 

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
439
1,000
Wenzako wamesomeshwa na vitumbua.
Acha dharau.
Maisha bado safari ndefu.

sijawadharau wauza vitumbua.
na wala sijamkejeli yeyote.
nimeeleza tu experience niliyokutana nayo.
na wala sijasema wauza vitumbua ni miyeyusho
nimejiapiza tu mwenyewe hamu tu imeniondokea,kuna vitu mtu akiviona kumbukumbu humjia na sijasema pahala popote kuwa vitumbua ni vibaya la hasha,usinielewe vibaya
 

mamseri

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
685
250
Sio vitumbua tu vinafanyiwa hivo ni vyakula vingi unavyokula migahawani pamoja na maandazi, halfcake, donati nk. Hivyo usichunguze sana we kula tu
 

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
5,815
2,000
unashangaza,biashara zote ndo hivo,kama unakula mandazi nako ndo hivyohivyo kwj ufupi tunakula sana uchafu
 

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
439
1,000
Pole sana na Hongera kwa Kutimiza miaka sita bila kula Vitumbua. Daah miaka sita yote umechelewa kutuambia.
Kuna vitu ukijivua nikujitia Stress tu
Hasa hii migahawa tunayokula siku za kazi.
wewe acha tu,Mungu tu anatulinda
lakini yule mama miyeyusho sana.
kanifanya mpaka leo nisile vitumbua
bora hata nisingemuona ase
leo nimekutana na picha ya vitumbua mtandaoni ndio nikaamua nishare hili tukio humu.

haha
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,812
2,000
Duh

Basi haya ufanywa na wanaotenda hayo kwenye kila chakula kuvutia wateja haswa au mengine pia kama ya masharti anayopewa ya kitu alivhoomba kiwe kishetani.....ndio maisha yao wengi.

Na pia wale wapenda kufanya sherehe ya lazima vinywaji na vyakula kama nyama choma ya ng'ombe mzima au mbuzi

ila mara bila sababu, hao nao wengi wana masharti.

Ameenda kuendeleza kwingine...

Duniani bora ule unachopika kwako, la sivyo tembea na Mola na imani ya kuwa na nguvu juu ya haya mambo.
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
48,731
2,000
Vitumbua tu ndo huli unajuaje vitu vingine kuwa hawaweki?
Wanawake wa uswazi wana mambo sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom