zema21
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 619
- 257
Imepita miaka miwili tangu nilipoachana na mpenzi wangu, kiukweli huyu mdada nilimpenda kwa moyo wangu wa dhati, sikuwahi kumsaliti nilimwona kila kitu kwangu, kulingana na hali niliyokuwa nayo sikuweza kutangaza ndoa ila nilimwahidi maisha yakikaa sawa ndio jambo litakalofuata, nyumbani nilimtambulisha, na yeye alinitambulisha. Tuliwekeana maagano kwa njia ya maombi, tuliwashirikisha hata baadhi ya watumishi wa Mungu wakatuombea.Hakuwa mpenzi wangu wa kwanza lakn moyo wangu ulimpenda kwa dhati.
Sikuamini siku aliponitamkia kuwa mm na yeye basi akakimbilia kuolewa, niliumia sana mtoto wa kiume. Nilifunga na kuomba sana juu ya hilo lakn haikubadili chochote. ilichukua muda takribani mwaka mzima ndipo nikakubali hali...
Kilichotokea ni kuwa moyo wangu ulikufa ganzi hata kiwango changu cha imani kilirudi nyuma, nikawa nashindwa hata kufanya maombi yale ya kawaida. kwa upande wa mapenzi sikuweza kuwa na hamu ya kupenda tena. Nilipata ushauri nasaha kutoka marafiki na ndugu.
shuda yangu kubwa kwa sasa ni kuwa siwaamini wanawake hata kidogo, yaani nashindwa kabisa kuwa na mahusiano strong tena moyo wangu unashindwa kupenda sijui nifanyeje, natamani sana kuwa na familia lakn shida nashindwa kuwaamini wanawake, yaani nimejikuta niko mbali na wanawake, sina hatta marafiki, nimekuwa na tabia ya ukali na pia nimejikuta ninakuwa mtu wa kupata hasira ghafla vitu ambavyo sikuwa navyo. naomba kwa yeyote anayeweza kunishauri namna bora ya kurejea katika hali yangu ya kawaida plz.
n.b Matusi na kejeli sihitaji hapa plz tuheshimiane. nitashukuru kama psychologist utanishauri