Ni muhimu Rais mstaafu Kikwete aongezewe Ulinzi

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,607
1,596
Tukiangalia hali ya siasa ilivyo sasa baada ya kufariki Mh Rais Magufuli, kuna mambo mengi sana ili yawe sawa katika nchi yanahitajika uwepo wa Mh Kikwete.

Moja Kikwete ndie alietuletea Magufuli baada ya Magufuli kuandaliwa na Hayati Mkapa, hivyo Magufuli kuingia madarakani Kikwete anahusika sana pia inawezekana Mh Kikwete alikua na malengo binafsi hadi kuruhusu Magufuli awe Raisi.
Hivyo Mh Kikwete anajua nini cha kufanya kuweka sawa mambo yote.

Pili Mh Kikwete ndie aliemtengenezea njia Mh Samia kuwa kiongozi mkubwa Tanzania nzima baada ya Mh Samia kufanya vizuri katika ngazi mbalimbali kule Zanzibar kabla ajawa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba hadi umakamu wa Raisi.

Hivyo inawezekana Mh Kikwete akawa anawafahamu vizuri wote wawili, yani Hayati Mh Magufuli na mama Samia na anajua ubora na madhaifu yao sababu kwa njia moja au nyingine aliwaandaa yeye.

Tunajua Mh Kikwete ana mapungufu yake, ila likija jambo lenye maslahi mapana ya Taifa ni mtu mmoja makini sana.

Tatu Mh Kikwete hayupo katika makundi yanayotafuta uongozi kwa sasa sababu ya umri pia inawezekana busara zimeongezeka baada ya kuona vifo vya Mh Mkapa na Mh Magufuli, hivyo psychological hana cha kupoteza ila ataangalia maslahi mapana kwa nchi sasa na hata badae

Hivyo ni muhimu sana vyombo vya ulinzi na usalama vikamuongezea ulinzi Mh Kikwete sababu ndie mtu anaefahamu jambo sahihi la kufanya kwa sasa inawezekana kuliko mtu mwingine yeyote kwa sasa.

Sisemi kwamba mama Samia hana uwezo, ila Mama Samia yupo katikati baada ya uwepo wa makundi yanayoitwa CCM asilia na CCM mamluki kitu ambacho sio sahihi na sio kweli sababu, Katiba ya CCM iko wazi na inatoa fursa kwa wanachama wote.
View attachment 1730511
 
Kwamba asipolindwa atauawa?? toka umezaliwa ushawahi sikia hizo makitu tz, kwa uoga hata wa kuiogopa maiti tulionao, thuubutu
 
Wamuue kwa lipi sasa....walikuwa na hasira na yule chuma mwamba aliewachomesha mafuta ya gulfstream toka marekani mpaka chato na bado mwamba hakuwa na habari nao.

Yule bwanyenye haji kusahau maishani mwake atasimulia na wajukuu naamini.
 
Tukiangalia hali ya siasa ilivyo sasa baada ya kufariki Mh Rais Magufuli, kuna mambo mengi sana ili yawe sawa katika nchi yanahitajika uwepo wa Mh Kikwete.

Moja Kikwete ndie alietuletea Magufuli baada ya Magufuli kuandaliwa na Hayati Mkapa, hivyo Magufuli kuingia madarakani Kikwete anahusika sana pia inawezekana Mh Kikwete alikua na malengo binafsi hadi kuruhusu Magufuli awe Raisi.
Hivyo Mh Kikwete anajua nini cha kufanya kuweka sawa mambo yote.

Pili Mh Kikwete ndie aliemtengenezea njia Mh Samia kuwa kiongozi mkubwa Tanzania nzima baada ya Mh Samia kufanya vizuri katika ngazi mbalimbali kule Zanzibar kabla ajawa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba hadi umakamu wa Raisi.

Hivyo inawezekana Mh Kikwete akawa anawafahamu vizuri wote wawili, yani Hayati Mh Magufuli na mama Samia na anajua ubora na madhaifu yao sababu kwa njia moja au nyingine aliwaandaa yeye.

Tunajua Mh Kikwete ana mapungufu yake, ila likija jambo lenye maslahi mapana ya Taifa ni mtu mmoja makini sana.

Tatu Mh Kikwete hayupo katika makundi yanayotafuta uongozi kwa sasa sababu ya umri pia inawezekana busara zimeongezeka baada ya kuona vifo vya Mh Mkapa na Mh Magufuli, hivyo psychological hana cha kupoteza ila ataangalia maslahi mapana kwa nchi sasa na hata badae

Hivyo ni muhimu sana vyombo vya ulinzi na usalama vikamuongezea ulinzi Mh Kikwete sababu ndie mtu anaefahamu jambo sahihi la kufanya kwa sasa inawezekana kuliko mtu mwingine yeyote kwa sasa.

Sisemi kwamba mama Samia hana uwezo, ila Mama Samia yupo katikati baada ya uwepo wa makundi yanayoitwa CCM asilia na CCM mamluki kitu ambacho sio sahihi na sio kweli sababu, Katiba ya CCM iko wazi na inatoa fursa kwa wanachama wote.
Ni muhimu kulinda na kuwaenzi mentors.
 
JPM alikua analindwa kwa ulinzi wa hali ya juu na smetangulia mbele ya haki. Unafikiri kuna ulinzi unaoweza kuzuia kifo?
Bwana asipoulinda mji, walindao wakesha bure.
Duniani kuna mda tunahitaji ulinzi wa Mungu, pia kuna mda inabidi tujilinde wenyewe kibinadamu
 
Back
Top Bottom