Ni muhimu kuridhika na kile unachojaliwa na Mungu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Kuna bwana mmoja alikuwa na utajiri mkubwa sana. Alianza taratibu mpaka kufikia kutengeneza faida ya milioni 300 -400 kwa mwaka. Kitu kilichomsumbua bwana huyu ni kukosa mtoto wa kiume. Mtoto wa kwanza na wa pili wote walikuwa mabinti waliozaliwa na afya njema.

Bwana huyu alikosa usingizi akiwaza akifa yeye hakuna wa kubeba jina la familia. Hili likumfanya anywe sana pombe. Mke alipobeba mimba ya tatu mipango mikubwa ilifanywa. Mke alishangaa kuwa anapelekwa kujifungua kwenye hospitali ya serikali.

Mke alipojifungua aliletewa watoti wawili, wa kike na wakiume. Manesi walimpa hongera nyingi. Mama kwa mshangao alizipokea habari zile kwa furaha kubwa. Lakini wakati wa mimba hakuna aliyemwambia kuwa anategemea mapacha. Mume alifurahi mno, watoto walikaribishwa nyumbani kwa karamu ya ng’ombe.

Kadiri watoto wale walivyokua ndivyo tabia ya ufujaji wa pesa kwa yule mtoto wa kiume ilivyoongezeka. Alijiunga na magenge mabaya, kule wote walimfahamu ni mtoto wa tajiri vijana wa mjini waliendesha maisha yao kupitia ufala wake. Alitaka ajulikane, wakikaa kijiweni wanaongelea dili za pesa lakini hawana mtaji yeye anawaambia mnahitaji shilingi ngapi kesho nitaleta.

Baba yake alimuonya sana kuhusu tabia hii ya kupenda pesa. Moyoni alijipa moyo kuwa zile dili anazotengeneza na washikaji one day yes zitakubali na ataacha kumtegemea msure. Mzee alishaamua kumtoa kijana yule kwenye mirathi. Alijua wazi kuwa mali aliyoitafuta kwa miaka chini ya kijana yule itapotea ndani ya miezi.

Sikumoja vijana wenzake walimwambia wanahitaji milioni 50 wakachukue mzigo China. Kijana alishajua wazi kuwa mzee wake hawezi kumpa pesa ile. Alimlia timing akiwa mwenyewe ofisini. Aligonga mlango, alipoingia ndani alimwambia mzee shida yake. Mzee alikataa kwa capital NO. Ndipo alipomkaba shingo huku akimpiga mateke mpaka mzee akakata roho.

Baada ya mama kushtuka mzee amechelewa wala hapokei simu yake. Walimkuta amelala sakafuni. Ingawa alikuwa na matatizo ya high patention lakini ilikuwa controlled na dawa. Maiti ilipelekwa hospitali kwa post-mortem.

Majibu ya post-mortem ndiyo yalileta kizaa zaa Ilikuwa wazi jamaa amekufa kwa physical injuries. Rafiki na msiri mkubwa wa marehemu alikuwa ni daktari aliyefanya mipango ya kuiba mtoto wa kiume wa mama mmoja wodini na kumpa mke wa tajiri. Mama yule aliambiwa mtoto aliyejufungua hakuwa rizki.

Kwa kuogopa kijana asije kuwaua mama na dada zake. Alimweleza mke wa marehemu ukweli baada ya mazishi. Mke wa marehemu hakuamni alichoambiwa. Hakujua kabisa kuwa analea mtoto asiye wake. Siku ambayo mwana sheria anasoma mirathi na kuwa mtoto mkubwa wa marehemu ndiye mwendeshaji wa biashara zote. Mtoto wa kiume alimrukia mama yake na kumkaba shingo. Walinzi walimuahi na mtoto yule kuwekwa chini ya ulinzi.

Baba alileta jambazi nyumbani kwa tamaa ya mtoto wa kiume. Pia yule kama aliyeibiwa mtoto hajui dua gani aliomba kwa Mwenyezi Mungu.
 
Kuna bwana mmoja alikuwa na utajiri mkubwa sana. Alianza taratibu mpaka kufikia kutengeneza faida ya milioni 300 -400 kwa mwaka. Kitu kilichomsumbua bwana huyu ni kukosa mtoto wa kiume. Mtoto wa kwanza na wa pili wote walikuwa mabinti waliozaliwa na afya njema.

Bwana huyu alikosa usingizi akiwaza akifa yeye hakuna wa kubeba jina la familia. Hili lilinfanyavanywe sana pombe. Mke alipobeba mimba ya tatu mipango mikubwa ilifanywa. Mke Alisha has kuwa anapelekwa kujifungua kwenye hospitali ya serikali.
Sky endelea sasa..au una usingizi jamani...Muke ya Asprin...
 
Sky endelea sasa..au una usingizi jamani...Muke ya Asprin...
Je alikuja kupata Mtoto wa Kiume?nini hatma ya maisha yake...je watoto hao wa kike walikuwa msaada gani kwake baadae...maswali ni mengi kwako Sky....
Je story hii inatufundisha nini?
 
Turidhike na chochote tunachojaliwa na Muumba wetu.

Muumba wetu ndiye anayejua ya dhahiri naya ghaibu, kila jambo analotufanyia Muumba wetu linakuwa na faida katika maisha yetu.
 
Back
Top Bottom