Ni muda muafaka wa kufukuza Mabalozi wote wa mabeberu na kufunga balozi zetu kwenye nchi zenye mabeberu

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
276
1,000
Mabeberu katika nyakati tofauti yametoa onyo la ukiukwaji wa haki za raia kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Na leo hii Lissu anaongea na Mabalozi wa mabeberu jijini Dar.

Kwa kuwa Magufuli na CCM yake wana chuki na hawa mabeberu kwa kuleta umaskini na kutuingilia uhuru wetu, nashauri ni muda muafaka wa kuwafukuza hawa mabalozi wa mabeberu na pia ni muda wa kufunga balozi zetu zilizopo katika nchi za mabeberu ili Tanzania iwe na maendeleo.

Tunategemea baada ya mabeberu kuondoka tutakuwa na ndege zaidi ya milioni moja, tutajenga fly over kila kona ya nchi, tutakuwa na umeme wa kutosha, tutakuwa na treni zinazoelea (lavitating trains), tutakuwa na nyumba bora, maisha bora, mazao yetu yatapata masoko, tutakuwa na elimu bora nk.

Ni muda muafaka wa Magufuli kufunga balozi za mabeberu nchini na kwenye nchi za mabeberu.
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
17,164
2,000
Pole sana!

Wewe na Lissu wako hujui hata maana ya beberu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom