Ni mtumishi gani wa umma anayetoa SIRI za Serikali kwa watu nje!

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,318
Mange amekuwa akipata baadhi ya taarifa za ndani sana za Serikali na hata watu wengine wamekuwa wakijigamba kuwa kila linalofanyika ndani ya Serikali wao wanapata taarifa hizo A to Z.

Swali la kawaida tu ni nani hao wanaotoa hizo taarifa kwa watu ambao hawapo katika mfumo huo wa kupata taarifa hizo.

Lengo lao ni nini kwa hao watumishi kwa kutoa hizo siri kama kweli wanazipata toka kwa hao watumishi wa umma.

Kiutaratibu ndni ya Serikali kuna taarifa za kawaida ambazo mwananchi anatakiwa kuzipata lakini kuna taarifa ambazo ni nyeti lakini bado taarifa hizo hata mwananchi wa kawaida hazina shida sana lakini kuna taarifa ambazo ni SIRI tena kwa muhuri wa rangi nyekundu unazikuta mitaani ni nani huyo ambaye anathubutu kutoa taarifa kama hiyo kwa watu wasiohusika.

Serikali ifuate taratibu zake kuhakikisha watumishi kama hao wanapatikana na kufikishwa mbele ya sheria.
 
wote wasiopenda zulma wale wa hide my id si mmoja wala wawili tena wengine ni haohao wa tiss maana unakuta vitu vizito vipo instagram.........
 
classified doc zilizo kwenye hardcopy? ni watu wa huko huko ndani waliochoshwa na mfumo..
Mzee mwenzangu, Kinachodukuliwa kama ni kwenye system ni interms of Softcopy, Ila wakati mwingine wakati wa udukuaji kunakuwa na conversion Kutoka hardcopy kwenda Soft then baadae itarudi Hardcopy ndizo ambazo utazikuta mtaani.

Example: Document imeonekana na mmoja wapo wa watu wa Karibu au Waziri, au Msaidizi wake, Kifaa cha kudukulia kikawa ni simu, Anapodukua palepale na conversion inafanyika kubadili kutoka Hardcopy (inayodukuliwa) kwenda Softcopy (kidukuz).
So ni suala ya Machine/Aina ya Udukuzi wenyewe tu.
 
Moja ya sababu za mahangaisho kwa watumishi wa umma. Mtu anaenda ripoti kwa mange matatizo ya ofisin anategemea nn kwamba rais awe anaendeshwa na mange aiseeeee labda awamu nyingine ila sio kwa mwanaume toka chato
Kwel ndugu yangu hiko ndio chanzo cha haya yote?
 
Back
Top Bottom