Ni mtoto yupi Nabii Abraham aliagizwa amtoe kafara? Ni Ishmail au Isaka?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Kwenye Mwanzo 22:1-18, je inawezekana kuwa mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara awe ni Ishmael, siyo Isaka, kama inadaiwa?

Vinginevyo, inawezekanaje Isaka awe "mtoto pekee wa kiume" wa Abram?

Jibu:
Ni Isaka aliyetolewa kafara na si Ishmael kwa sababu angalau nne:

- Hata Kurani haisemi kuwa alikuwa ni Ishmael, Mwanzo 22:2 inasema alikuwa ni Isaka.

- Ingawa Kurani ya kiislam inazungumzia jambo hili kwenye Sura 37:99-111, hakuna sehemu yoyote kwenye Kurani nzima inayosema kuwa huenda alikuwa Ishmael au Isaka.

Wanazuoni wengi wa awali wa kiislam walifundisha kuwa alikuwa ni Isaka, wakati wengine walifundisha kuwa alikuwa ni Ishmael.

Tazama al-Tabari juzuu ya 2 uk.68. al-Tabari juzuu ya 2 uk.82-97 inasema mabingwa 16 wa kiislam walisema kuwa ni Isaka wakati mabingwa 23 wa kiislam walisema kuwa ni Ishmael.

Abram alikuwa na mtoto mmoja tu wa kiume wakati ule: Ishmael alikuwa na miaka 14 wakati Isaka alipozaliwa. Hajiri na Ishamael walifukuzwa na kwenda sehemu nyingine Isaka alipoachishwa kunyonya kwenye Mwanzo 21:8-10. Abraham alijaribiwa "kwa muda mrefu" baada ya hapo kwenye Mwanzo 21:34, na "mtoto wa kiume" alikuwa kwenye meza ya kutolea kafara kwenye Mwanzo 22:12. Mrithi pekee:

Isaka alikuwa mirthi pekee, na mtoto pekee wa kiume, pia inamaanisha "mtoto wa kiume mpendwa". Ingawa utamaduni wa wakati ule uliruhusu watu kuwa na masuria kwa ajili ya kupata watoto, urithi na haki ya mzaliwa wa kwanza vilienda kwa watoto wa kiume wa mke halisi, siyo watoto wa kiume wa masuria. Mwanzo 21:12 inasema, "katika Isaka uzao wako utatajwa".

Embu tuelimishane.
 
Back
Top Bottom