GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,689
- 109,111
1. Jumuiya kumekuwa ni sehemu za Majungu.
2. Jumuiya imekuwa ni sehemu za Kuchunguzana Kimaisha.
3. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Masutano.
4. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Wanaume Kutongoza na Wanawake kutafuta wa Kuwachapa Nao ( Kuwabandua )
5. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Kutishana kuwa kama hauhudhurii basi Ukifa ( Ukifariki ) Kanisa Katoliki halitokuombea ukiwa Jenezani Kwako.
6. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya kila Siku kuja na Michango isiyo na Kichwa wala Miguu.
7. Jumuiya imekuwa ni Gulio Kuu la kila aina ya Unafiki unaoujua na usioujua hapa duniani.
Halafu Wewe Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina wa Jumuiya yangu hivi mnavyonitishia kuwa kama nisipohudhuria Jumuiya Nikifa hamtoniombea mmeshazungumza na Baba Mungu na akawaambieni kuwa ataanza Kunitanguliza Mimi Kaburini kabla yenu? Wapuuzi wakubwa nyie.
Je, mnavyong'ang'ania Kutoniombea GENTAMYCINE pale Nikifa je, ile Siku ninazaliwa mlikuja Agha Khan Hospital mbele ya Sister Brendah na Sister Aghata waliohakikisha Nazaliwa vyema na salama Kuniombea? Wapuuzi wakubwa nyie.
Na nani aliyewadanganyeni kuwa Imani ya Ukatoliki inapimwa kwa Kuja Kwake ( Kuhudhuria ) katika Jumuiya za Kikatoliki kila Jumamosi kama ya hii leo?
Nilichoamua tu na najua hata Mwenyezi Mungu ananibariki nacho ni kwamba nitajitahidi Kuhudhuria Ibada zote za kila Jumapili ( hasa Misa yangu pendwa ya Kwanza ) na kutoa Sadaka na Michango ya Kikanisa kama tu nitakuwa Nimebarikiwa na Uchumi kwa wakati huo na kama sina najua hata Mola / Maulana nae atajua na hatonichukia au kuwa na Usununu ( Kinyongo ) nami.
Nawatakieni nyote Jumuiya njema!!!!