Ni Mkakati wa kuwaondoa 'Shikamoo', ili kuikabidhi nchi kwa vijana

PakiJinja

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,683
15,858
Mabadiliko ya mawaziri ambayo yamekuwa yakifanywa tangu rais Samia aingie madarakani, yamelenga kupunguza wale wenye umri mkubwa (Senior Citizens) katika nafasi hizo ili kuwapisha au kuwaingiza under 50.
Hili litaenda hadi ndani ya majeshi yetu na taaisi nyingine za usalama.

Mkakati uliopo hivi sasa ni kuingiza fikra mpya kwa kuwaingiza vijana zaidi katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini.

Tumeona, hata waziri mkuu ameshafunguliwa mlango wa kutokea.

Mkakati ni mzuri, ila bahati mbaya ni kwamba, wanaoingizwa sasa kwenye mfumo hawataweza kuipatia nchi kile kilichokusudiwa sababu wengi wamelelewa na kuwa crippled na mfumo ule ambao jitihada zinafanyika kuachana nao.

Wengi ni wahafidhina wa mifumo na siasa za hovyo, zile za kifisadi, za kubebana, kutowajibika, rushwa n.k

Kati ya marais 6 ambao hadi sasa Tanzania imewahi kuwa nao, wawili ndiyo waliingia katika urais wakiwa na umri wa miaka 60 and/or above. Rais Ali Hassan Mwinyi, aliingia akiwa na miaka 60, wakati rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan, yeye aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 61.

Nikionacho hivi sasa, haijarishi ataendelea au ataamua kutoendelea, lakini rais ajaye baada ya Samia atakua na umri chini ya miaka 50.

Wakati huo zaidi ya nusu ya viongozi wengi wa sasa hususana baraza la mawaziri zitakua ni sura mpya kabisa.
 
“Tumeona, hata waziri mkuu ameshafunguliwa mlango wa kutokea”

Ni kweli utashi wenu wote ndio umeishia hapo?? I have seen everyone anazungumzia hivyo, Unahisi kwa mamlaka aliyonayo rais angekuwa hamtaki PM angezukuka huko kote 🤔
 
“Tumeona, hata waziri mkuu ameshafunguliwa mlango wa kutokea”

Ni kweli utashi wenu wote ndio umeishia hapo?? I have seen everyone anazungumzia hivyo, Unahisi kwa mamlaka aliyonayo rais angekuwa hamtaki PM angezukuka huko kote 🤔
Kwani hapa ni swala la kumtaka au kutomtaka mtu? Kama utasoma vizuri, issue iliyopo ni mabadiliko ya mfumo.
 
Hakika kabisa na ukiangalia kwa jicho LA tai ni kama Rais Samia amempa kadi nyekundu Kasimu Majaliwa kiprofesa maana unaibu waziri MKUU kikatiba haupo .Pamoja na yote hayo ni kama mama anataka Majaliwa akae bench kwa lengo LA kwamba ajipange if God wishes anaweza kuwa yeye ndiye mshika kijiti after her.
 
Back
Top Bottom