Mimi ni kijana fulani mdogo hivii, labda nianze kwa kuwaelezea sifa zangu ili nisaidiwe kwenye hili linalonikabili kwa sasa.
Mimi ni mchamungu japo sio sana lakini ni mtu mstaarabu alafu mpole sana kifupi sijawahi kuwa na historia ya kugombana na mtu.
Kutokana na utu nilionao watu wa jinsia zote na wa kila rika wamekuwa wakipenda kukaa na mimi, alafu kubwa zaidi mimi ni mtu ninayejua karibu kila kitu hamuwezi kuamini lakini najua lugha za makabila zaidi ya 10 kuzizungumza japo sio kiufasaha sana, najua pia kufanya kazi nyingi na kwa bidii yaani kila ninayeishi nae huwa anadai kunifurahia sana naweza nika socialize na kila mtu najua kuchekesha, watu wote wananipenda kwa sababu kila tukipga stori huwa nasikiliza na pia nachangia kwa hoja nzuri na zenye maana, IKUMBUKWE PIA NI MUONGEAJI MKUBWA SANA.
Tukiwa wawili naongea sana napenda kutawala mazungumzo yote nikigundua unapenda mieleka basi ntajitahidi kufuatilia nini kinaendelea ili siku tukikaa tukipga story kuhusu mieleka basi ntakuwa nakuteremshia habari zote kwa ukweli na uhakika hivyo hivyo pia katika muziki, siasa, biashara, tiba, movie, utani, fasheni, science na technology najua kuhuru sanaa pia nafanya sanaa.
Chumbani kwangu kuna vitabu vingi sana zaidi hata ya 200 alafu pia natembelea mitandaon sana hata hapa JFkaribia kila jukwaa natembelea kujifunza kutoka kwa magreat thinker wenzangu hivo najua mengi sana.
sijisifii lakini nahisi nina akili sana na nikigundua hulka yako, kama ni marafiki tunaokutana mara nyingi basi ntafanya juu chini nijifunze mengi unayopenda kusikia ili twende sawa, najua kucheza na akili za matajiri mpaka maskini , watoto wadogo wananipenda sana, wazee pia wanadai na nidhamu sana na ni ukweli mtupu nahisi sijazaliwa na hasira.
Watu wengi sana wanapenda ku share mambo yao na mimi na kwa kulijua hilo mda wote nachunga ulimi wangu nisikukwaze wala kuongea mabaya.
Kimsing nadhani mmeshanielewa mimi ni raia wa aina gani.
Hivi karibuni nilipata mpenzi mtoto flani wa kishua nikawa nikikaa nae nampigisha stori weeh kama ilivyo tabia yangu na kwa kuwa mdada mwenyewe sio mwongeaji kivile na mimi kama nilivowaambia najua kila kitu basi ikawa ndo jukumu langu kumstorisha .
Eti juzi from now where kaamua kuachana na mimi, nikamuuliza rafiki yake akanambia eti binti havutiwi na mimi sijui ooh na kiherehere sijui mara ooh naongea sana.
Sasa huyu mwanamke ana matatizo yake au ndo wanawake wote hawavutiwi kimapenzi na wanaume wa tabia zangu?