Ni mbinu chafu za kutaka kubakia madarakani kwa ccm hata baada ya 2015 kufika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mbinu chafu za kutaka kubakia madarakani kwa ccm hata baada ya 2015 kufika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by omuhabhe, Aug 19, 2012.

 1. o

  omuhabhe Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa hadanganyiki mtu,kwa mbinu zozote zile zitakazobuniwa na ccm ili 2015 isomeke hivyo kuwa tuna vita na Malawi kwa sababu ya Lake Nyasa,ili waendelee kuwa madarakani.
  Katika sura ya pili ya katiba tunayoipigia chapuo kwa mabadiliko yake inaelekeza kuwa Nchi inapokuwa na vita dhidi ya adui na Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi,Bunge laweza mara kwa mara kupitisha azimio la kuongezea muda wa miaka 5 uliotajwa ktk ibara ndogo (2) kwa muda wa kushika madaraka ya Rais hiyo inapatikana ktk sheria ya 1984 No. 15,ibara 9 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa TZ.
  Mheshimiwa wetu walishamalizana na mwenzake kuwa tusiwe na wasiwasi hakuna jambo kama hilo
  sasa wale ndugu zetu waliotangulia kutuambia kuwa tuko tayari kwa vita sijui walitumwa na nani?
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Waliona rais ni dhaifu wakaamua kuingilia madaraka yake, nae rais kuonyesha ni dhaifu akazidi kukaa kimya
   
Loading...