Ni marufuku kutumia jina la 'wanaume'

Tumpara Dudu

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
617
487
Ndugu zangu,nikiwa kama mwenyekiti wa Chama cha wanaume mashababi wa Tanzania(Chawamata) napenda kutoa Taarifa rasmi ya chama chetu kuhusu maamuzi ya kikao chetu tulichoketi jana Tar 12/11/2017.

Kwamuda mrefu tumekuwa tukipokea malalamiko kuhusu mwenendo wa kujilegeza,uwoga na uvivu wa kupindukia wa wanaume wa Dar na hivyo kudhalilisha jinsia ya uwanaume,na sisi tukaamuwa kuunda timu makini kuchunguza tuhuma hizo na kwa ushahid ufuatao

1/Kupigwa mbele ya wakwe zao kutoka kwa watu wanaodhaniwa kuwa ni FFU pale ukonga huku wanaume wa Dar wakishindwa kujitetea wakat ni haki yao kikatiba.

2/Kulazimishwa kulala saa 11 jioni na vijana 11 wa Panya road wenye mapanga tu huku wakishindwa tena kujitetea.

3/Kushindwa kumtetea mwanaume mwenzao huku wakimuacha anatobolewa macho na mtu mmoja tu aitwae Skopion

Baada ya kutafakar kwa kina ushahidi huo viongoz tumejiridhisha kuwa wanaume wa Dar mnatudhalilisha wanaume sote hivyo kuanzia leo tunawapiga marufuku kujiita Wanaume wa Dar na pia tunapiga marufuku mtu yeyote au kikundi chochote kukuiteni hivyo na badala yake mtaitwa WAZEE WA CHIPS KUKU.

TII SHERIA BILA YA SHURUTI.

imetolewa leo na mw/kiti wa CHAWAMATA-TAIFA.

WATOA POVU HODARI 10 wa mwanzo WATAJISHINDIA TIKETI YA KWENDA KUSHUHUDIA LIGI KUU YA UINGEREZA (VPL)
 
Basi wavae magauni tu hakuna namna
tapatalk_1490550602673.jpeg
 
vipi hata wewe ni mwanaume wa dasalamu, hii picha mbona inatia mashaka!!
398933.jpg
 
Back
Top Bottom