Ni manufaa yapi tunayapata kuwa Raia wa Tanzania?

Averos

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
993
695
Habari,

Leo nimekuwa katika tafakuri ya kuangalia ni privilege zipi tunazipata kama Raia wa Tanzania.

Hapa namaanisha katika nyanja zote za maisha Mtanzania anapata unafuu upi?

Nitoe mifano kidogo

Kwa mfano katika huduma za kijamii

- Mtanzania anapata unafuu gani katika huduma ya maji, ikilinganishwa na nchi nyengine ambazo wanalipiii huduma ya maji

-Mtanzania anapata unafuu upi katika umeme ikilinganishwa na nchi nyengine ambazo unalipia umeme ikizidi unit 200 katika matumizi yako lakini chini ya units 200 ni bure

-Mtanzania anapata unafuu upi katika huduma ya elimu ikilinganishwa na nchi nyengine ambazo mwanafunzi anapatiwa facilities zote za kielimu kama stationaries na chakula bure

-Mtanzania anapata unafuu upi katika huduma ya mawasiliano ikilinganishwa na nchi nyengine ambazo kupiga simu Ndani ya nchi ni bure

-Mtanzania anapata unafuu upi katika huduma ya usafiri ikilinganishwa na nchi nyengine ambazo nauli na mafuta ni bei nafuu Sana ingawa hawana bandari za kushusha mafuta

-Mtanzania anapata unafuu upi katika huduma ya ulinzi ikilinganishwa na nchi nyengine ambazo askari wanaotoa huduma ya usalama bure bila ya kudai rushwa kwa mteja

Katika uchumi,

Mfanyabiashara, mkulima, mwekezaji, mchimba madini, mwenye hospital, shule wanapata vipaumbele na msaada upi kama Raia ikilinganishwa na nchi nyengine zinazotuzunguka kuwa Raia kumekuwa na unafuu gani kwako katika maisha?

Naomba kuwasilisha
 
Ukitaka kujua unafuu wa hayo yote tusianzie mbali. Ingia hapo Kenya, pitiliza ingia Uganda halafu malizia na Rwanda. Njoo na ripoti kuhusu namna ulivyofanya mahusiano na polisi wa huko, customer care kwenye huduma za kijamii, uhuru wa kuongea kijiweni na gharma za maisha. Hivi unajua kwamba Zanzibar pia ni Tanzania?

Peleka bidhaa yako yoyote kama mahindi au mchele waambie nimekuja kufanya biashara. Majibu ya hazo site yatakwambia kama ukiishi Tz unapata unafuu au la.
 
Ukiachilia mbali huduma za kiserikali, mtanzania ananufaika kwa mambo mengi kama raia wa Tanzania. 1.Urahisi wa kumiliki ardhi. 2.tabia ya nchi na sura ya nchi vimepunguza ugumu wa maisha,tunapata mvua za kutosha hivyo maisha yanarahisika maana tunakuwa na chakula.
 
Wee jamaa Unagubu sana.. wanaoishi nawewe wanapata tabu kwelikweli.

Watu wamezijenga nchi zao mpaka zikafikia apo unapopaona, mambo hayakuja tuu kama miujiza.

Wewe kama raia, umelifanyia nini Taifa kitu special cha kujivunia ili in-return upate hivyo unavyo vidai ? Wajibika Mzee usipende vitu mtelezo mtelezo tuu

Wee jamaa nakukumbusha tena unagubuu
 
Mtanzania ananufaika kwa kupata platform nzuri ya kupigia majungu na kula mademu kwa mpaka chini ya buku 2
 
Ukitaka kujua unafuu wa hayo yote tusianzie mbali. Ingia hapo Kenya, pitiliza ingia Uganda halafu malizia na Rwanda. Njoo na ripoti kuhusu namna ulivyofanya mahusiano na polisi wa huko, customer care kwenye huduma za kijamii, uhuru wa kuongea kijiweni na gharma za maisha. Hivi unajua kwamba Zanzibar pia ni Tanzania?

Peleka bidhaa yako yoyote kama mahindi au mchele waambie nimekuja kufanya biashara. Majibu ya hazo site yatakwambia kama ukiishi Tz unapata unafuu au la.
Brother hapo Kwenye Zanzibar ikikupendeza naomba ufafanuzi kidogo
 
Ukitaka kujua unafuu wa hayo yote tusianzie mbali. Ingia hapo Kenya, pitiliza ingia Uganda halafu malizia na Rwanda. Njoo na ripoti kuhusu namna ulivyofanya mahusiano na polisi wa huko, customer care kwenye huduma za kijamii, uhuru wa kuongea kijiweni na gharma za maisha. Hivi unajua kwamba Zanzibar pia ni Tanzania?

Peleka bidhaa yako yoyote kama mahindi au mchele waambie nimekuja kufanya biashara. Majibu ya hazo site yatakwambia kama ukiishi Tz unapata unafuu au la.
Mkuu kama una experience ya aina hiyo tusaidie
 
Ukiachilia mbali huduma za kiserikali, mtanzania ananufaika kwa mambo mengi kama raia wa Tanzania. 1.Urahisi wa kumiliki ardhi. 2.tabia ya nchi na sura ya nchi vimepunguza ugumu wa maisha,tunapata mvua za kutosha hivyo maisha yanarahisika maana tunakuwa na chakula.
Nakushukuru kwa mchango wako, ila unahisi nchi yetu imefanya juhudi ya kutosha katika kuwapatia Raia unafuu wa maisha?
 
Wee jamaa Unagubu sana.. wanaoishi nawewe wanapata tabu kwelikweli.

Watu wamezijenga nchi zao mpaka zikafikia apo unapopaona, mambo hayakuja tuu kama miujiza.

Wewe kama raia, umelifanyia nini Taifa kitu special cha kujivunia ili in-return upate hivyo unavyo vidai ? Wajibika Mzee usipende vitu mtelezo mtelezo tuu

Wee jamaa nakukumbusha tena unagubuu
Nashkuru kwa mchango

Nilitegemea kupata mchango wako na sio mashambulizi binafisi (Appeal to a person)

Ila umenisaidia kujua kuwa nani nashiriki kwa kiasi katika dhana ya gubu, gubumeter yako inaweza kunipima kiwango changu?
Sote tunajenga nchi Mkuu, ili ili tuendelee tunahitaji vitu bonne

Watu
Ardhi
Siasa safi
Uongozi bora
Katika vitu hivyo vinne kipi kimetukwamisha kupata unafuu wa maisha kama Raia wa Tanzania?
 
kaoe mzanzibari mkuu, mtoto atakuwa raia wa Zanzibar na atafaidi mengi mno.

Mambo gani hayo atafaidi mkuu
 
Ukitaka kujua unafuu wa hayo yote tusianzie mbali. Ingia hapo Kenya, pitiliza ingia Uganda halafu malizia na Rwanda. Njoo na ripoti kuhusu namna ulivyofanya mahusiano na polisi wa huko, customer care kwenye huduma za kijamii, uhuru wa kuongea kijiweni na gharma za maisha. Hivi unajua kwamba Zanzibar pia ni Tanzania?

Peleka bidhaa yako yoyote kama mahindi au mchele waambie nimekuja kufanya biashara. Majibu ya hazo site yatakwambia kama ukiishi Tz unapata unafuu au la.
Kipofu hujilinganisha na kipofu wenzake hataki kabisa kusaidiwa aone

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom