Ni lipi basi zuri la Dar - Mwanza?

Zero Competition

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
310
451
Ni basi gani zuri kwasasa nikiwa na maana sio uzuri tu wa muonekano wa nje na ndani bali pia ambalo linaweza nifikisha mapema ukilinganisha na mabasi ya kampuni nyingine.

Mana kuna yale mabasi ambayo ukitoka hapa Dar saa 12 asubuhi Mwanza unafika kuanzia saa saba usiku sasa haya mabasi hapana kwakweli.

Kwa ambao mmesafiri hivi karibuni naomba msaada tafadhali wa kujuzwa kuhusu hilo swali langu hapo juu.
 
Kama una roho nyepesi, magonjwa ya moyo, presha, BP. Usipande ally's wanakimbiza gari sana kama wana roho za spea. Kuna allys moja wanaiita ya petrol jamaa anakimbiza na kuovateki vibaya mno. Kuwa makini sana. Inabidi zianzishwe basi nzuri sana ambazo zinaenda mwendo wa wastani. Maana sikuhizi ni mwendo wa Ligi.

Le Petrole mnyama DRG.!
 
Ni basi gani zuri kwasasa nikiwa na maana sio uzuri tu wa muonekano wa nje na ndani bali pia ambalo linaweza nifikisha mapema ukilinganisha na mabasi ya kampuni nyingine.

Mana kuna yale mabasi ambayo ukitoka hapa Dar saa 12 asubuhi Mwanza unafika kuanzia saa saba usiku sasa haya mabasi hapana kwakweli.

Kwa ambao mmesafiri hivi karibuni naomba msaada tafadhali wa kujuzwa kuhusu hilo swali langu hapo juu.
Kuna kitu Alhushoom
 
Nenda panda kati ya hizi chuma utakuja kunishukuru

1.DRG 554 (la petrol) Ally's star (dereva juma na Wadiki) - 22:15 utakua nyegezi

2. DRR 754 (higher la mineso) Dar lux (dereva mtoto Chris na imma kiduku) - around 22:10-30 utakua nyegezi

3. DVA 964 allys star dereva Ginimbi - Hii chuma imebakiza kupaa tu.

4. DUP 897 Tanzanite ya Father Goliama - saa name kasoro mpaka saa nne na nusu upo nyegezi

5. DSE (JESHI) na ile Most wanted ally's star bus - kidogo zimepoa ila za moto sna hutachelewa.

6. DVA 963 & 965 - hili balaa lingine

Usikubali kupanda chuma yeyote ambayo sijaitaja apo , maana utakuja kulalamika mmefika nyegezi saa 8 usiku.
 
Back
Top Bottom