Ni lini ulifikia ukomo wa ukuaji?

Super Charged

Member
Jan 12, 2020
65
125
Habari wana JF,

Kuna vitu huwa tunaviona vya kawaida katika jamii lakin kumbe vinaathiri maisha ya baadhi ya watu. Nina mdogo wangu ana umri wa miaka 19 yeye amekuwa akiathiriwa na suala la ufupi. Yani kiufupi anapoteza pesa zake nyingi kutafuta dawa ya kuongeza urefu, mara leo kaagiza kutoka india, mara leo kafanya hivi.

Kiukweli ni kama anapoteza pesa tu, ingali kuna njia dawa aliagiza kutoka mataifa ya nje ikamsaidia kuongeza kama nusu inchi, ni kidogo sana kiukweli. Maisha yake yote yeye yuko na kutafuta urefu. Ana urefu wa futi 5.3 kikawaida ni mfupi mbele ya wanaume warefu lakn pia ni kama yuko average.

Anapenda kucheza baskteball, kwa umaridadi alonao katika huo urefu wake naona unamtosha maana ni hatari katika basketball na ninataman kumuona anafika mbal katika career ake. Huwa tunamwambia achana na urefu miaka 19 bado unaweza refuka mpaka unapofikisha umri wa miaka 21, lakini amekuwa akikataa kwa sababu anajiona kama ameshakuwa mkubwa na hawez refuka tena kwa sababu ana ndevu. Naomba kujuzwa wana JF.

Je, mwisho wa kurefuka ni miaka mingapi, anaweza ongezeka kidogo kwa umri alonao miaka 19.

Kama kuna dawa ya kumfanya aongezeka inches kadhaa zaidi ya hapo naomba mnijulishe pia mbali na surgery maana anachosikia chochote anafanya ni kama kavurugwa hajui kizur wala kibaya, naomba kujuzwa kama kuna dawa au njia nzuri ili nimsaidie dogo.

Changia na wewe katika umri gani uliacha refuka kwa wanaume.

Naomba kusaidiwa maoni wakuu maana huku ndo nyumbani kwetu, maana dogo tunaona suala dogo lakin linaathiri maisha ake kiujumla maana anaona kama ndoto zake hazitatimia hata kama akifanikiwa anaona ataitwa mchezaji mfupi, kingine anachoona kama hataongezeka licha ya kuambiwa ana nafasi mpaka miaka 21, ni yeye alibalehe mapema akiwa na umri wa miaka 16, (kiume).

Naomba msaada wana JF usijibu kwa dhihaka jibu kama mtoa elimu.
 
Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
1,764
2,000
Kuna growth & development

Growth mwisho ni 25yrs
Development ni mpaka mtu anapokufa

Mwisho wa kurefuka ni 25yrs ..sema tuu rate inaanza kupungua mtu akifika 20 to 25 anakua anaongezeka kwa rate ndogo sana tofauti na kipind Cha miaka 8 to 17 akiwa anabalehe
 
Super Charged

Member
Jan 12, 2020
65
125
Kuna growth & development

Growth mwisho ni 25yrs
Development ni mpaka mtu anapokufa

Mwisho wa kurefuka ni 25yrs ..sema tuu rate inaanza kupungua mtu akifika 20 to 25 anakua anaongezeka kwa rate ndogo sana tofauti na kipind Cha miaka 8 to 17 akiwa anabalehe
Hapo Sawa mkuu kwa maana Hiyo Dogo bado anachance ya Kurefuka kidogo licha Ya Kuwa Na ndevu ee
 
XII Tz

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
563
1,000
Kuna kitu inaitwa constitutional growth delay, ni moja ya growth patterns ambayo mtu mwenye nayo huchelewa kukua ( hufikia potential height a little bit later than usual ie early 20s). Vitu vinavyoashiria CGD ni muonekano wa kitoto yani kuanzia sura mpaka umbo ( haendani na umri wake) .. but at some point these people tend to catch up and reach their potential height .. kwahiyo muangalie huyo mdogo wako kama ana sifa tajwa hapo juu huenda akaendelea kukua, na kama tayari ana muonekano wa kikubwa ( adult) basi asijisumbue .. lastly, height is genetic na hawezi kucontrol genes ..
 
Sawa mkuu ana Sura ya Kikubwa Lakn Umbo lake bado Ni Dogo(Hajatanuka)Vp hapo ananafasi
 
Teenager

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
1,691
2,000
obviously urefu unatoka kwa wazazi.
mimi ni 17 but ni 6 feet tall sababu wazazi ni warefu hivyo nimerithi.

sasa kama yeye wazazi wake ni warefu basi kuna uwezekano mkubwa wa yeye kurefuka hapo baadae ila kama ni wafupi basi hakuna njia nyingine zaidi ya kujikubali, ila nadhani kuna njia za kufanya mazoezi nimeona watu wanatoa shuhuda kwamba wameongozeka some inches.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom