Ni lini Tanzania tutakuwa na flyovers?

Mkwele

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
206
24
Flyover-Nairobi.jpg Flyover-Nairobi..jpg
Fly overs katika jiji la Nairobi, Ee Mungu tujalie na sisi Tanzania tujengewe na viongozi wetu barabara juu kama Kenya.
 
Tumeshindwa kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini, tutaliweza hili la flyovers? Miti tunayo, mafundi seremala kibao, lakini madawati mnhh....Flyovers kwa hali tuliyo nayo ni luxury sio necessity.
 
mchakato na upembujzi yakinifu bado unaendelea na ukimalizika ndio atatafutwa mfadhili wa mradi mpaka sasa bado upembuzi yakinifu haujamalizika
 
Ni lini Tanzania mtoto wa mwananchi mwenye kipato duni hatowaza bodi ya mikopo katika utoaji wa mikopo yao.....?
 

Hii ndio ilikuwa flyover yetu, kuna mbili ama tatu kama hizi zinakuja na ujenzi unaondelea sasa hivi
 

Attachments

  • bridge-mazense.jpg
    bridge-mazense.jpg
    34.2 KB · Views: 80
Saa zingine ukiwa haujawahi kufika Afrika au Tz na ukawa unafwatilia jinsi watu wake wanavyoongea na kujadiliana unaweza ukafikiri labda hawa watu matatizo yao ni level nyingine kabisa na sio basic kama ilivyo, lakini ukifika na kuona tunavyoishi na mambo ambayo tumeyapa kipaumbele basi hautashangaa kwa nini ni maskini na watu wa mwisho Duniani karibu kwa kila kitu isipokuwa labda anasa!

Ni mambo ya kushangaza sana, watu wanalilia flyovers, wakati si ajabu hao wote wanaolilia flyover zijengwe Dar wakitaka kwenda kuwatembelea wazazi wao vijijini kwao wanaulizia kama mvua zimeanza ili wasikwame kwenye matope, si ajabu walisoma shule za bila madawati na walikaa kwenye sakafu kama walikuwa na bahati kidogo vinginevyo vumbini na mpaka leo si ajabu shule walizoma hali ni hiyo hiyo kama sio mbaya zaidi.

Mtu anaacha kulilia barabara zijengwe kuunganisha Tz nzima, analilia flyover Dar kwa maana anaishi Dar ili aweze kupiga picha, mtu anaacha kulilia reli ya kati ifufuliwe ili ipunguze gharama za usafiri kwa watu na hasa mizigo ili angalau hata kama yeye anaishi Dar labda bei chakula inaweza kushuka analilia flyover!
Sitashangaa kama Serikali ikifanya kura ya maoni Je, wajenge flyovers Dar au wakamilishe miradi wa barabara Tz nzima na kukufua Reli, kukawa kuna watu wengi tu watakaopigia flyovers ili wakapige picha na kuweka facebook!

 
Back
Top Bottom