Ni lini inabidi tuseme ndoa hii sasa basi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lini inabidi tuseme ndoa hii sasa basi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 3, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hakuna kipimo hasa kwa sababu kila mmoja anaguswa kwa namna tofauti na jambo fulani, lakini kila mmoja wetu ana kiwango tofauti cha kuwavumilia na hata kuwasamehe wengine. Watu wengi huwa wanajiuliza wanapokosewa na wenzao kwenye ndoa, ‘sijui nimwache au nimpe tena nafasi?'

  Dini zinasisitiza kusameheana, washauri wa masuala ya ndoa hivyo hivyo na hata mila na desturi zetu. Lakini kusisitizwa na kutenda ni vitu au mambo mawili tofauti. Bado dini hizo hizo kuna makosa ya kindoa ambayo zinayatazama kama makosa yenye kusameheka, lakini ambayo hayaruhusu au kutoa nafasi kubwa kwa ndoa kuendelea.

  Moja ya makosa hayo ni uzinzi, yaani kutoka nje ya ndoa. Kutoka nje ya ndoa ni kosa ambalo limechangia katika kuvunja ndoa nyingi sana. Hata hivyo, kwa bahati mbaya imetokea kuvunja ndoa pale ambapo zaidi anayefumaniwa ni mwanamke.

  Mtu anapozini tunasema hampendi mwenzake. Hii ina ukweli kidogo kwa sababu kuzini kunafanywa kwa sababu ambazo ni tofauti kutoka moja hadi nyingine.
  Kwa hiyo inashauriwa kwamba ndoa inaweza kuvunjwa au ni vizuri ikavunjwa kama inahusisha kuzini. Hata hivyo kama ni kuzini ambako kumetokea mara moja, inabidi mtu atafute sababu kwa nini kulitokea. Kama atathibitisha kwamba mazingira yaliyopelekea kuzini huko yalikuwa na ugumu katika kuepukwa, mume au mke wa huyo aliyefumania inabidi ajaribu kutoa nafasi kwa mwenzake.

  Kama kuzini ni mara kwa mara, haishauriwi ndoa kuendelea kuwepo.
  Mtu anapoishi kwenye ndoa ambayo imegubikwa na uzinzi, anajiweka kwenye hatari nyingi sana. Kwa siku hizi, hatari ya kwanza ni maradhi. Lakini kuna hatari nyingine kadhaa. Kuishi na mzinzi ni kuishi katika kero kihisia. Wenye wake au waume ambao ni wazinzi, mara nyingi pia wanakabiliwa na maradhi yasiyoonekana hospitalini kwa sababu ya kujiumiza kihisia.

  Kosa lingine ambalo linapotokea, mtu anatakiwa kufanya uamuzi wa kuifikisha ndoa tamati ni ulevi. Kama mme au mke ni mlevi sugu, hatua ya awali ni kwa mume au mke huyo kujitahidi kumsaidia mwenzake. Hilo linaposhindikana, kuna haja ya kufikia mahali ambapo talaka ndio njia mafaka.

  Ulevi sugu una maana ya mtu kuthamini pombe kuliko kitu kingine na hivyo kunywa karibu muda wote. Hii ina maana pia kwamba, mtu huyo hatajali kuhusu mke wala watoto. Lakini ulevi sugu huwafanya wengine kuwa wakorofi, kuwa wazinzi, kufuja fedha na kuingia kwenye maradhi kirahisi.

  Itaendelea…………………
   
 2. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold inawezekana mwanamke apewi msamaha akizini kwa kuwa kuna chance kubwa kuwa mwanamke mzinzi anakuwa hana mapenzi tena na mumewe ila mwanaume anaweza kuwa mzinzi kwa tamaa za mwili tu lakini mapenzi bado yako kwa mkewe kwa kuwa sex ina maana tofauti kwa mwanamke na mwanaume. Kwa mwanaume anaweza kucheat ili apate pa kupunguza/kumwaga xxx badala ya kujipiga nyeto wakati kwa mwanamke kama si changudoa sex inateka mpaka akili na inahusiana na kupenda.

   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  QUOTE
  "Moja ya makosa hayo ni uzinzi, yaani kutoka nje ya ndoa. Kutoka nje ya ndoa ni kosa ambalo limechangia katika kuvunja ndoa nyingi sana.
  Hata hivyo, kwa bahati mbaya imetokea kuvunja ndoa pale ambapo zaidi anayefumaniwa ni mwanamke."

  @Nyumba Kubwa... Kwa hiyo unakubaliana na mimi au?
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mtambuzi speed yako tu....
   
Loading...