Ni lazima wote tuwe chama tawala?

Ni lazima wote tuwe chama tawala?

ZEMAN

Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
5
Reaction score
8
Habari wadau. Nimekua nikifuatilia mijadala mingi humu ndani. Tukiwa kama wadau katika kuleta chachu ya maendeleo ya Tanzania yetu, nimeshindwa kukubali kwanini tunashindwa kuelewa wapinzani wapo kuikosoa serikali iliyopo madarakani na watakuwepo milele. Tanzania haina tofauti na nchi yoyote duniani lijapo swala la siasa na matamanio ya maendeleo.

Kupatikana kwa rais mpya (kwa njia yoyote unayoweza ielezea ambayo si kawaida kwa wengi) hakusababishi upinzani ukae kimya na kutotumia wajibu wake wa kuifuatilia, kuikosoa na kuishauri serikali ya chama tawala.

Labda kama wewe ni shabiki na si mtaka maendeleo vinginevyo huwezi pinga na kushutumu kila kinachopingwa kwa kuwa chama tawala ndo kilicholeta hoja. Jaribu kufikiri uone katika hilo linalopingwa..., Tanzania ina nafasi ya kupiga hatua au la...?. Wengi wetu tulishabikia uongozi wa awamu ya nne na kilichotokea wote ni mashahidi. Furaha ya kupata kiongozi aliyechapa kazi wizarani isitusahaulishe kutimiza wajibu wetu kama waTanzania.

Upinzani tutakuwepo. Mimi ni mpinzani wa serikali iliyopo si kwa kigezo cha kupinga kila kiletwacho mezani bali kupinga kilicholetwa ili kiweze kurekebishwa na kuletwa kilicho bora mezani. Na ninawahakikishia, huko nyuma nilikaa kimya kwa uoga (wengi ni kama mimi) nikifikiri nchi hii itabadilika kwa miujiza.

Miujiza iko kwenye kuhesabu kura tuu. Kwenye kutoa ushauri, kukosoa na kuirekebisha serikali ya chama tawala hakuna Miujiza!!

WaTanzania!!! Si lazima wote tuwe CCM!
 
Naomba Mungu anipe uzima nije nishuhudie siku CCM ikiondoka madarakan,
 
Back
Top Bottom