happymsafi
Senior Member
- Jul 4, 2016
- 100
- 84
Jamani ni lazima mama wa mume kulelewa na mke wa mwanae hata kama huyo mama ana watoto wake wa kike wakubwa wengine wana kazi zao na wanajitegemea wenyewe? Mi bmiinafsi naona si sawa kama mama ana watoto wake wakike ni bora kuenda kukaa kwa watoto wake wa kike wamhudumie kuliko kuenda kuhudumiwa na mke wa mwanae.
Tabia ya binadamu hawezi kuhudumia mtu ambae si wake kama atakavyo muhudumia mtu wake na endapo atamuhudumia basi lazima matatizo yatatokewa yule anayehudumiwa anaweza akahisi kama hapewi huduma inayostahili kupewa hata kama mhudumu anajitahidi kwa kiasi gani.
Jamani wadada ambao mna mama zenu baba zenu ambao wanahitaji huduma wachukueni wazazi wenu muwahudumie wenyewe msiwasukumie wifi zenu kwani wifi zenu pia wana mama zao baba zao wanahitaji kuwahudumia vilevile. acheni kuwatafutia watu matatizo ya lazima.
Mimi binafsi siwezi kumuacha mama'ngu aende kuhudumiwa na mke wa kaka yangu hali ya kuwa mie nipo. Huko ni kumpa mtu mzigo huku ukijuwa kabisa mama yako hawezi akapata huduma nzuri kama utakayompa mwenyewe.
Mwisho wa siku mnaona watu wabaya wakati wabaya ni nyie wenyewe uwezo wa kulea wazazi wenu mnao lakini mnawapeleka kulelewa na mtu aliekutana na kaka yako ukubwani hamfahamu amelelewa vipi halafu mnaleta lawama tu.
Kina dada chukueni wazazi wenu muwalee wenyewe kama pesa ya kumtunza kaka yako atakuletea huko kwako lakini si kuenda kumuachia wifi yako kama vile yeye ndo ana haki ya kukulelea wazazi wako hali ya kuwa yeye mwenyewe ana wazazi wake wanahitaji kulelewa?
Kwanini ushindwe kumlea mzazi wako uzeeni akiwa mgonjwa mpaka umsukumie mtu baki wakati yeye alikulea kwa hali zote raha na furaha ukiwa mdogo. Jamani leeni wazazi wenu wenyewe wifi zenu pia wana wazazi wao wa kuwalea.