Ni lazima mama wa mume kuhudumiwa na mke wa mtoto wake?

Pole kwa kufikiria kiufinyu kias hiko ila hapa jukwaani utapanuliwa tu mawazo na kuipata njia sahihi zaidi.
Hajafikiria kiufinyu. Ila amefikiria kiuwazi bila unafiki. Ndio ni mila mtoto wa kiume kutunza wazazi lkn zinapaswa kuwa questioned from time to time. Ndicho alichofanya huyu mdada. Ni kweli mtu anakuwa comfortable na mwanawe kuliko mke wa mwanawe. Mimi naishi na mama yangu, kitu au neno nikimtendea mama atalichukulia poa lkn kitu au neno afanye mdada wa kazi itakuwa shughuli. Sasa sipati picha angekuwa mke wa mwanawe. Hii ni changamoto ambayo haitatatuliwa na unafiki au na mazoea. Iangaliwe hali ambayo ni nzuri kwa watu wengi kama sio wote.
 
Sonia;
Ukiusoma uzi ulioandikwa na huyu mdada ni wazi kabisa kwamba hampendi mama mkwe wake. Ameogopa kusema tu. Swali; Hivi ka si huyu mama, huyo mume wako ungelimpata wapi?? Kwa nini ulikubali kuolewa badala ya kukaa na mamako ukamlea hadi afe ndio uolewe?
Hata angelikuwa na watoto 8 wa kike na wakiume 1 tu aliyekuoa. Wewe ndiye wa kumlea, kumtunza na kumuogesha. Ni heshima kuwa, kakuzalia mume. Mtunze kwa heshima kama unamheshimu mumeo. Ila kama ni hao wanawake wa siku hizi mnaowadharau waume zenu, hata mamake utamdharau tuuu.
Hao mawifi nao kule waendako watawakuta mama mkwe. Wawatunze ka wa kwao anavyotunzwa.
kwani heshima ni kumtunza na kumuogesha tu? kumpelekea pesa ya mtunzo pia ni heshima hata kama haukai nae. ila jamani tuwe wakweli kwa mtoto wake wa kike na kwa mke wa mwanae wapi anaweza akapata huduma stahili? tusifanye vitu kwa mazoea tuangalie hali halisi.
 
Nimeona huu uzi inabidi umenikumbusha mbali sana, baba yangu akiwa kitenda mimba kwenye familia yao bibi mzaa baba aliishi na sisi siku za mwisho za maisha yake. Ilifika wakati hata hakuweza kukaa pekeyake na msaidizi tu. Alikuja akiwa na 80+ na tuliishi nae kwa kama miaka kumi na zaidi. Uzee unakuja na mambo mengi sana. Hakutaka nguo zake zifuliwe na mtu ambae si ndugu yake, house girl, wote hao walikuwa watu baki pamoja na mama pia. Ndugu zangu wakiwa shule ilibidi niwe mfua nguo, sasa ile umetoka kupaka nail polish unaingia chumbani uchukue novel mwenyewe ukasome, unapewa nguo za kufua.
bora huyo wa kufua kuna wengine wana visa mtu mwingine ni vigumu kuvumila labda mtoto wake aliemzaa
 
Binafsi nijuavyo Mimi, Wazazi wetu ni Baraka katika Maisha yetu, Wazazi ndiyo watoto wetu kadiri siku zinavyokwenda mbele, Kwa hiyo mwenye Nguvu kumlea Mama kwa 100% ni Mtoto wa Kiume, Nina Experience na hilo na ni kawaida kabisa.
Yani Mtoto wa Kiume Unapaswa kujua una jukumu la kulea wazazi wako wote kwa 100%, Kwani ndicho walichokufanyia.Siwezi kusemea upande wa Mwanamke sana, lakini naona kama Mama yangu au Baba yangu atazalilika, I don't feel fine.
 
Hajafikiria kiufinyu. Ila amefikiria kiuwazi bila unafiki. Ndio ni mila mtoto wa kiume kutunza wazazi lkn zinapaswa kuwa questioned from time to time. Ndicho alichofanya huyu mdada. Ni kweli mtu anakuwa comfortable na mwanawe kuliko mke wa mwanawe. Mimi naishi na mama yangu, kitu au neno nikimtendea mama atalichukulia poa lkn kitu au neno afanye mdada wa kazi itakuwa shughuli. Sasa sipati picha angekuwa mke wa mwanawe. Hii ni changamoto ambayo haitatatuliwa na unafiki au na mazoea. Iangaliwe hali ambayo ni nzuri kwa watu wengi kama sio wote.

Wanawake mpo good sana kwenye ubinasfi.kinachomsumbua huyo dada ni hataki kukaa na mkwe wake lakin hajui tafsiri vizuri za kiafrica.ukiolewa ni kwamba wewe na yule mama mkwe wako ndio wa mama wa ule mji.watoto wa kike wanazaliwa hapo sio wenye mji ni wapita njia tu, maana nao siku moja wataolewa na wataenda kuanzisha mji wao.so kimantiki yeye ndio anapaswa kuwa karibu zaid na mama mkwe wake maana hata wakifa watazikwa sehemu moja.Mkubali hizo ndio garama za ndoa ila ukiwa na upendo haitakusumbua sana.ukiona inasumbua ni kwamba toka kwenu hujaandaliwa kuwa hivyo
 
Tatizo mabinti mnaoolewa...

Hebu mkawe baraka kwenye miji ya watu

Mama wa mumeo ni sawa na mama yako..... hata mama yako anaweza kulalamikia huduma. Utampeleka kwa nani?
Kwani ukitimiza wajibu wako na kumhudumia kwa upendo maneno na lawama zitakuchubua ngozi???

Kiafrika wazazi huenda kwa watoto wao wa kiume unless kuwe na sababu nzito... ndio wazazi huenda kuugulia kwa binti...kumbuka binti kaolewa. Yupo mji mwingine ndio maana wazazi wa kiafrika huona shida kwenda kwa binti....

Hivyo wakamwana jamani...muwe na upendo....muwe wavumilivu
....muwe na kiasi mkawe baraka ktk nyumba na miji muingiayo
mama'ko hawezi kuwa sawa na mama wa mumeo hata siku moja. unaweza ukafanya kosa dogo tu tena si kama umedhamiria kufanya hivyo mama'ko anaweza akachukulia poa tu lakini fanya hilo kosa kwa mama wa mumeo uone litakuzwa hilo utaonekana mbaya utachukiwa maisha yako yote. kuepusha mambo kama haya bora watoto wa kike wawahudumie wazazi wao.
 
bora huyo wa kufua kuna wengine wana visa mtu mwingine ni vigumu kuvumila labda mtoto wake aliemzaa
Mama alikua mwajiriwa pia lakini uzuri wake ni kuwa kipindi chote cha bibi kuishi nyumbani baba alirudi nyumbani mara baada ya kazi, kwakua alikua mtoto wa mwisho, yeye na bibi walikuwa na special bond. Alirudi alipewa mashitaka yale yote aliyofanyiwa mchana kutwa. Hii pia ilikuwa faraha kwa mama kumuona mume wake nyumbani.
 
Na wale ambao wamezaliwa wa kiume watupu mama zao waende wapi???
Na wengine hao watoto wa kike hawajiwe au hawajielewi, mtafurahia mama aendelee kuteseka!??
ndio maana ndoa za siku hizi ha zidumu, watu wanaolewa wakishakuwa na roho mbaya kwa ndugu wa mume.
kama ana watoto wa kiume tu inakuwa haina jinsi inabidi ahudumiwe tu lakini kama ana watoto halafu aende kukaa kwa mtoto wake wa kiume si vizuri. mtoto hata akiwa hajielewi hawezi kumuacha mama ateseke acheni kutafuta sababu ambazo si za kweli
 
mama'ko hawezi kuwa sawa na mama wa mumeo hata siku moja. unaweza ukafanya kosa dogo tu tena si kama umedhamiria kufanya hivyo mama'ko anaweza akachukulia poa tu lakini fanya hilo kosa kwa mama wa mumeo uone litakuzwa hilo utaonekana mbaya utachukiwa maisha yako yote. kuepusha mambo kama haya bora watoto wa kike wawahudumie wazazi wao.
Hivi mumeo akikataa kuishi na mama yako kumhudumia utafurahi?

Tusitendee wenzetu vile ambavyo hatupendi kitendewa.

Yes kuna utofauti na changamoto... ila kikubwa ni mke kusimama kwenye nafasi yako. Fanya wajibu wako. Na ignore kero. Yes kuna watu wana maneno au visa. Ila silaha ni kupotezea....cha msingi kanuni za nyumba yako hazivunjwi.

Ila ukisema uumie kisa ana mabinti utajiumiza mwenyewe na kuumiza ndoa yako.

Sambaza upendo umuaibishe shetani.
 
Huyo mtoto wa kike inawezekana ana kwake lakini ni kwa mumewe pia. Kwahiyo mimi kama mume usimuhudumie mama yangu lakini mama yako akae kwangu umuhudumie.
Ukishakuwa na fikra hizo tayari ushaweka roho mbaya kwenye nafsi yako na huyo mkweo hata akiwa mwema utamtafutia dosari maana tatizo lako si kulea mama wa mwenzio tatizo lako ni roho mbaya. Kumbuka utazaa watoto wa kiume na ipo siku utakuja kuwa mama mkwe wa mtu.
umenielewa vibaya wala si roho mbaya, naongelea urahisi wa kupata huduma iliyo bora. mke wa mwanao na mtoto wako wa kike nani anaweza kumuhudumia mama yako vizuri bila tatizo? mie binafsi nikija kuwa mama siwezi kwenda kuishi kwa mtoto wangu wa kiume na mkewe hata kama nitakuwa na watoto wakiume wote nitatafuta alternative
 
Hajafikiria kiufinyu. Ila amefikiria kiuwazi bila unafiki. Ndio ni mila mtoto wa kiume kutunza wazazi lkn zinapaswa kuwa questioned from time to time. Ndicho alichofanya huyu mdada. Ni kweli mtu anakuwa comfortable na mwanawe kuliko mke wa mwanawe. Mimi naishi na mama yangu, kitu au neno nikimtendea mama atalichukulia poa lkn kitu au neno afanye mdada wa kazi itakuwa shughuli. Sasa sipati picha angekuwa mke wa mwanawe. Hii ni changamoto ambayo haitatatuliwa na unafiki au na mazoea. Iangaliwe hali ambayo ni nzuri kwa watu wengi kama sio wote.
bora umenisaidia maana naona watu wamenielewa vibaya.
 
Binafsi nijuavyo Mimi, Wazazi wetu ni Baraka katika Maisha yetu, Wazazi ndiyo watoto wetu kadiri siku zinavyokwenda mbele, Kwa hiyo mwenye Nguvu kumlea Mama kwa 100% ni Mtoto wa Kiume, Nina Experience na hilo na ni kawaida kabisa.
Yani Mtoto wa Kiume Unapaswa kujua una jukumu la kulea wazazi wako wote kwa 100%, Kwani ndicho walichokufanyia.Siwezi kusemea upande wa Mwanamke sana, lakini naona kama Mama yangu au Baba yangu atazalilika, I don't feel fine.
kumbe mnatumia hisia zaidi ya uhalisia. eti atadhalilika, atadhalilika kwa mtoto wake? wazazi ndio ni baraka kila mtu anafahamu lakini bado haina ulazima wa mtoto wa kiume alazimishe mke wake amlee mama'ke hata kama dada zake wapo na uwezo wa kufanya hivyo. mpeleke mama'ko kwa dada zako uwe unapeleka pesa na mahitaji mengine wao watamuhumia nayo pia ni baraka na uhakika wa kupata huduma nzuri ni mkubwa zaidi kuliko kwa mkeo
 
Wewe unataka mama/baba ahudumiwe na mtoto wa kike , iwapo huyo mtoto wa kike kaolewa na mumewe kamleta baba/mama yake amlee yeye mwenyewe huoni kwamba mnampa mzigo huyo mume? Utaratibu wa kiafrika mzazi hulelewa na mtoto wa kiume hata kama mtoto wa kike ana uwezo au ni mwajiriwa. Sababu mzazi kulelewa na mtoto wa kike na iwapo atakuwa ameolewa siku ukitokea ugomvi mkwe akiporomosha matusi atawaunganisha wote mke na mkwe hivyo italeta picha mbovu,.
Pia itamnyima mume kujitawala na familia yake kisa kuna mkwe nyumbani.
Hivyo ni vizuri mzazi akalelewa na mtoto wa kiume kuliko wa kike ili kuleta heshima kwenye family.
 
Hivi mumeo akikataa kuishi na mama yako kumhudumia utafurahi?

Tusitendee wenzetu vile ambavyo hatupendi kitendewa.

Yes kuna utofauti na changamoto... ila kikubwa ni mke kusimama kwenye nafasi yako. Fanya wajibu wako. Na ignore kero. Yes kuna watu wana maneno au visa. Ila silaha ni kupotezea....cha msingi kanuni za nyumba yako hazivunjwi.

Ila ukisema uumie kisa ana mabinti utajiumiza mwenyewe na kuumiza ndoa yako.

Sambaza upendo umuaibishe shetani.
kwanini akatae wakati anajua kulea mama'ngu ni jukumu langu mtoto wa kike? unaongea vizuri lakini ni vigumu sana kutekeleza labda kama hayajakukuta. anyway, Mungu atupe subira
 
Humu ndani ya JF kama umeolewa na Mchaga habari hii inakuhusu sana .Soma mawazo yote yanayotolewa humu na huna jinsi ya kukwepa ni jukumu lako kuwalea hao wazee.
 
Back
Top Bottom