Ni lazima mama wa mume kuhudumiwa na mke wa mtoto wake?

Il
Sijui dini yako ila kama ungelikuwa mkristo ungekumbuka neno la Mungu linavyo kuusia kuwa "Utamwacha baba yako na mama yako na mtaambatana pamoja na mumeo nanyi hamtakuwa wawili tena bali mwili mmoja. Sasa, kwa kuwa umeenda kuwa mwili mmoja na yule mume, ndo maana linakuwa jukumu lako wewe mwanamke kumtendea mema yule aliyekupa wewe mume.
Huolewi ukaenda kukaa na mumeo kule kwenu bali unaenda kukaa na huyo mumeo kule kwao. Huko kwao ndiko kuna mama mkwe wako. Kaka zako nao wataleta wake zao nao kazi yao ni moja, kumtunza mama yako wewe.
Acheni kukwepa majukumu. Wanawake wengine wamefika mahali pa kulaaniwa mchana peupe kwa kuwadharau wakwe zao na kujisifu kuwa wanawatunza wazazi wao. Hii ni kukosa mawazo mazuri.
Mungu amenijalia, nina wasichana 6. Kati ya watoto 8. Hao wasichana wameolewa 5 bado mmoja. Lakini, naomba nikuambie kuwa, huwa natamani wao waje kuchukua kwangu na hata kuwapelekea wakwe wao kutoka kwangu kuliko kuwagandamiza kuwa walete kutoka huko kwao. Huyu mwali wangu mmoja ananitunza vyema mno pamoja na mama mkwe wake. Anatuheshimu kiasi nasema, natamani hao wa kwangu wafanye vivyo huko waliko.
Ilo andiko kasome tena.hakuna sehem inasema Mke ataenda kuishi kwao mume.Bali wataambatana na kuwa mwili mmoja
 
tatizo ni Mila na Tamaduni za jamii kubwa kuwa Mama hawezi kwenda kukaa kwa Mkwewe wa kiume ambapo wanatafsiri ni kama matusi. ndio maana wanaendaga kwa watoto wao wa kiume. ila kwa watoto zao wa kike wanaweza kwenda kusalimia na kulala mara moja moja ila sio kuweka makazi. ila ikitokea binti yuko single basi anaweza kukaa na mama yake. maana kwa mtoto wa kike kukaa ni kujidharaurisha...kumbuka ndoa zetu hizi za kubeep mke mmetibuana na bwana mmeanza vurumai haya kawatimua na mama yako mnafungasha virago ni aibu na fedheha.. thus y wanakaaga kiumeni kwa vile ndio safe zaidi. Ni issue za Mila na Utamaduni tu.
 
Labda uwe hujaolewa. Lakini mama kukaa na mkwe (mume wa binti yake) ni kama hatakuwa na amani 100% kulingana na mila na desturi zetu waafrika. Kukaa kwa mwanaye wa kiume ni kawaida sana.
 
Il

Ilo andiko kasome tena.hakuna sehem inasema Mke ataenda kuishi kwao mume.Bali wataambatana na kuwa mwili mmoja

Weye ndo ukalisome miye silisomi tena kwa sababu nililielewa mara ya kwanza tu. Mke wangu aliwaacha wa kwao akaja kuishi kwetu. Akawa wangu, familia ya babangu, ukoo wa kwetu hivyo ni wa kwetu. Ndo maana ya kuambatana na kuwa mwili (Wangu) mmoja. Au vip??
 
Sonia;
Ukiusoma uzi ulioandikwa na huyu mdada ni wazi kabisa kwamba hampendi mama mkwe wake. Ameogopa kusema tu. Swali; Hivi ka si huyu mama, huyo mume wako ungelimpata wapi?? Kwa nini ulikubali kuolewa badala ya kukaa na mamako ukamlea hadi afe ndio uolewe?
Hata angelikuwa na watoto 8 wa kike na wakiume 1 tu aliyekuoa. Wewe ndiye wa kumlea, kumtunza na kumuogesha. Ni heshima kuwa, kakuzalia mume. Mtunze kwa heshima kama unamheshimu mumeo. Ila kama ni hao wanawake wa siku hizi mnaowadharau waume zenu, hata mamake utamdharau tuuu.
Hao mawifi nao kule waendako watawakuta mama mkwe. Wawatunze ka wa kwao anavyotunzwa.
Kama hujaolewa naomba nilete barua ww ndio mks
 
Kwa ni wazazi wao si walikuwa na maisha yao, kama waliyaharibu kwa nini liwe jukumu la Mtoto wa wengine kuwalea?
Nilidhani ni mtu unayeelewa kumbe umelewa uzungu wakati upo Africa.
nani kakwambia kuwa kila mzazi anayeishi kwa watoto wake kaharibu maisha yake kabla??
alivyowalea watoto wake mpaka wakawa na mafanikio alihamia!??
tatizo huwa hamtaki waume zenu wasaidie ndugu zao. ndio maana inawauma mama/baba kuwa naye. responsibility itakuwa moja kwa moja. akiwa kwingine si unaweza ukamzuia asitume hata hizo hela!!!
vya kwenu ndio dhahabu!!!
 
Inategemea jamani..
Siyo kila mtu anaweza kukubali mke ampeleke mama yake kwenda kuugulia kwake..
Wengine hata ndugu akija kwako kidogo atakuambia naomba umwambie huyo ndugu yako aondoke
Ila ndugu zake wakiwepo hamna shida kabisa...
Na siku zote ikumbukwe baba ni kichwa cha familia.
 
``` salamu.makabila mengi ya tanzania mwanaume anabeba majukumu ya ukoo.ila pia kumvumilia mama mkwe kunakuongezea uwezo wako wa kuhimili mikikimiki ya dunia.kwa kawaida wzee wa zamani ilikuwa kuoana lazima familia zifahamiane,hivyo ulipaswa uwafahamu kabla hujajiingiza kuunga undugu
 
Me nawaelewa ujue, it's not easy kuishi na mama mkwe wala mawifi, hata wakiwa kwao sembuse kuishi nao ndani ya nyumba moja.

Ila tu tuwe wakweli, ni mangapi mnayavumilia kwenye ndoa zenu? How many times tunasikia wake wakisema "no matter what sitoondoka for the sake of my kids"? Hapo unakuta mama ndo anahangaikia familia kama baba, baba hana mchango wowote, bado mume kitombi, mkong'oto unapata, una watoto ulioletewa, na magonjwa Huna tu uhakika coz hujapima bado. Kwa nini usimvumilie mama mkwe for the sake of your husband and kids? (Ingawa mtu akiniambia pia Kuwa yamemshinda namuelewa vizuri tu, sikubaliani na nafsi moja kuifia nafsi ya mtu mwingine)

Mabinti tunapay a very high price kuzipata hizi ndoa jamani, Mungu tu ndo anajua. Kanisani utatukuta tunabubujika khaa, tukisikia mkesha tupo, sijui kuna mtumishi gani tupo. Haya mchumba kapatikana, Mungu tu ndo anajua sacrifices ngapi tunazifanya kumuimpress baby, yani hadi mtu aseme "will you marry me" mmh ni tumekoma tumekomazika. Hapo sijaongelea upande wa kilingeni woiiiiiii. Kama tunaingia gharama kiasi hicho, kwa nini tusiingie gharama kuzilinda ndoa zetu? Do you expect maisha Kuwa smooth after ndoa, shetani mwenyewe anajitahidi kweli ndoa zisambaratike, tusimpe chance kabisa. You fought to be the his only one, God knows umefight michepuko mingapi ya mumeo Ila bado upo. Kwa nini usifight kwenye hili jaribu la mama mkwe? Ni mapito tu kama mapito mengine. Mama mkwe ni pasua kichwa

1. Angalia kama kuna visababishi vyovyote Kwa upande wako. Sio mara zote wakwe ndo wana matatizo, na sisi mabinti tuna maghubu wakati mwingine. Afu na hivi tumeshajijengea Kuwa wakwe wana matatizo tunaishi nao Kwa machale mno, basi akikosea tu kidogo ushajipa mawazo "ooh ameanza, ntamyoosha", kumbe kakosea tu kiubinadamu maskini. Na wamama wengine ile saikolojia kwamba she is the only one kwenye maisha ya mwanae, sasa kukubali Kuwa kuna mtu mwingine sasa hivi kwenye maisha ya mwanae, anaona kama mtacompete for affection. Ndo tatizo hapo

3. Mu-ignore kama Umeona kila unalofanya kwake halikubaliki, Wewe timiza wajibu zako. Familia, kazi na Mungu. Ila make sure mama mkwe unamuheshimu, anakula, anavaa, anatibiwa yani anapata vitu vyote vya msingi, usimtukane mbele ya mumeo wala watoto wako. Kama Huna kazi, ndo tafuta kazi au kibiashara chochote cha kukuweka busy, at least usitumie muda mwingi na mama mkwe wako. Make sure wewe ndo mama mwenye nyumba ndani ya nyumba yako na Sio yeye aje na amri zake

2. Ongea na mumeo juu ya kutoelewana na mama mkwe. Ila be careful Sio unamuongelea mama yake as if unamuongelea nani sijui, no matter what she is still his mother. Mumeo atakusaidia kujua mfanyaje kumu-handle mama ake. Na hata siku yakitokea ya kutokea, at least utakuwa na support yake Coz ameshuhudia mambo yalivyokuwa yanaenda

4. Mkabidhi tu kwa Mungu. Mbona kanisani tunaendaga hadi na picha za waume, majina ya michepuko etc tukiomba Mungu adeal nao? Mpeleke na mama mkwe kwa Mungu, atadeal naye effectively kuliko ambavyo wewe binadamu unavyoweza kudeal naye

Kingine jamani, kabla hujaolewa, chunguza hiyo familia unayokwenda kuolewa, na omba Mungu akufunulie familia hiyo. Kuna watu mpo tu kwenye mahusiano ila unaona kila kitu mama ndo anacontrol, na watoto wengine wameoa kabisa ila mama ndo remote. Unategemea wewe uolewe tu na kuanza kumcontrol huyo mumeo, mtakwazana tu na mama mkwe. Na mwingine unaolewa na unajua kabisa mnaenda kuishi kwenye nyumba ya familia, please jiandaeni tu vizuri kisaikolojia
Well said, umebalance vizuri bila unafiki. Barikiwa sana
 
imeshazoeleka kuwa mwanamke huwa hataki ndugu wa mume waje kwao. ila wa kwake hana shida nao. hilo hata dada zetu wanafanya na tumeshuhudia. lakini mtambue kuwa mama/baba hawezi kukaa kwa binti yake alikoolewa. labda huyo bintiye awe single au kusiwepo watoto wa kiume ambapo atatafuta hata kwa mdogo wake akaishi kuliko fedhea ya kutukanwa wewe na binti yako. ndoa zenyewe ndio hizi hizi watu wanaolewa ili kuondoa mikosi unategemea nini???
siku jamaa kacharuka anawarushia mizigo yenu nje itakuwaje!!!?
 
Mkuu ikibidi unamuogesha Mungu atakulipa wewe fanya tu kwa moyo mmoja bila kulalamika maana hujui hata wewecatakayekuogesha utakapozoeeka.so fanya wema then sepa.
Sina tatizo na kutoa usaidizi huo, ila nasi mila za kwetu kichina...
 
Nyie kinachowasumbua ni nafasi....

Hamjaweka mipaka ta nafasi ya mkw na nafasi ya mama

Pili mko kwenye nyumba yake.... hicyo huwezi kuwa huru inabidi muishi kwa kanuni na sheria zake

Ilipaswa muhame yete aje kwenu......
Na msigombee huo upendo wa kijana mtaishia kufarakana

Mwisho ukushamjua tabia baadhi ya msmvo ignore..... mradi utimize wajibu wako kama mke

Kwa mfano wa huyo dada, unaona kama kuishi tu kwenye nyumba ya mama mkwe ndio kunamfanya awe alivyo? Au ni hulka yake tu? Nafikiri kwenye maisha yetu tunagoma kuweka mipaka ya uelewa kuwa huyu ni mama wa mume wangu, hivyo ni mama yangu; likewise huyu ni mke wa mwanangu hivyo ni mwanangu...Anyways, hizi issue ni tete na kila mtu nahisi anapambana na uhalisia anaoukuta, coz mtu anaweza akatimiza wajibu wake na bado akawa treated kama ha-exist kama mfano wa hapo juu.
 
Mtoa mada je mme ana haki ya kumtunza mama mkwe? maana kama mama yake hana haki ya kulelewa na wewe basi mama yako hana haki ya kulelewa na yeye FINITO. ila kwa kifupi hujajua maana ya maisha ya ndoa kwa kulinganisha Mila, desturi na taratibu za kiafrika.
 
Tatizo mabinti mnaoolewa...

Hebu mkawe baraka kwenye miji ya watu

Mama wa mumeo ni sawa na mama yako..... hata mama yako anaweza kulalamikia huduma. Utampeleka kwa nani?
Kwani ukitimiza wajibu wako na kumhudumia kwa upendo maneno na lawama zitakuchubua ngozi???

Kiafrika wazazi huenda kwa watoto wao wa kiume unless kuwe na sababu nzito... ndio wazazi huenda kuugulia kwa binti...kumbuka binti kaolewa. Yupo mji mwingine ndio maana wazazi wa kiafrika huona shida kwenda kwa binti....


Hivyo wakamwana jamani...muwe na upendo....muwe wavumilivu
....muwe na kiasi mkawe baraka ktk nyumba na miji muingiayo

Umenena Vema
 
Ninavompenda mume wangu, automatically nawapenda na ndugu zake wote, nafurahi nikiwa nao,.. Mama mkwe ndo usiseme siwezi ona shida yoyote kumtunza, kuanza kuchagua watu wa kukaa nao hiyo ni roho mbaya tu, kama kweli unampenda mumeo huwez ona mama yake mzigo
 
wewe ukizeeka utakwenda kuishi kwa binti yako badala ya kwa kijana wako wa kiume?
 
Siyo adabu kiafrica mama kwenda kukaa kwa binti tena aliyeolewa,anagongana toilets/makoridoni na mkwewe wakati mwanae wa kiume yupo na ana familia na mazingira ya yeye kukaa kwa mwanae huyo ni rafiki...wanawake,tukiwapenda wakwe zetu kama tunavyowapenda wazazi wetu,maisha yatakuwa rahisi
 
Back
Top Bottom