Ni lazima mama wa mume kuhudumiwa na mke wa mtoto wake?

kumbe mnatumia hisia zaidi ya uhalisia. eti atadhalilika, atadhalilika kwa mtoto wake? wazazi ndio ni baraka kila mtu anafahamu lakini bado haina ulazima wa mtoto wa kiume alazimishe mke wake amlee mama'ke hata kama dada zake wapo na uwezo wa kufanya hivyo. mpeleke mama'ko kwa dada zako uwe unapeleka pesa na mahitaji mengine wao watamuhumia nayo pia ni baraka na uhakika wa kupata huduma nzuri ni mkubwa zaidi kuliko kwa mkeo
Nooh! Mbona Me alinilea???? Tatizo liko wapi??? Huko anakwenda kusalimia tuu, Yani siku Dada kakorofishana na Mumewe,
Mumewe aanze kumtusi dada yangu mbele ya Mama yangu???? Au aanze kutukana mama na mwana?? Aah!!
Maisha yangu ni Magumu lakini hayajafikia huko haisee! Hiyo Me Kama Jembe siikubali.
 
Sonia;
Ukiusoma uzi ulioandikwa na huyu mdada ni wazi kabisa kwamba hampendi mama mkwe wake. Ameogopa kusema tu. Swali; Hivi ka si huyu mama, huyo mume wako ungelimpata wapi?? Kwa nini ulikubali kuolewa badala ya kukaa na mamako ukamlea hadi afe ndio uolewe?
Hata angelikuwa na watoto 8 wa kike na wakiume 1 tu aliyekuoa. Wewe ndiye wa kumlea, kumtunza na kumuogesha. Ni heshima kuwa, kakuzalia mume. Mtunze kwa heshima kama unamheshimu mumeo. Ila kama ni hao wanawake wa siku hizi mnaowadharau waume zenu, hata mamake utamdharau tuuu.
Hao mawifi nao kule waendako watawakuta mama mkwe. Wawatunze ka wa kwao anavyotunzwa.
 
Tatizo mabinti mnaoolewa...

Hebu mkawe baraka kwenye miji ya watu

Mama wa mumeo ni sawa na mama yako..... hata mama yako anaweza kulalamikia huduma. Utampeleka kwa nani?
Kwani ukitimiza wajibu wako na kumhudumia kwa upendo maneno na lawama zitakuchubua ngozi???

Kiafrika wazazi huenda kwa watoto wao wa kiume unless kuwe na sababu nzito... ndio wazazi huenda kuugulia kwa binti...kumbuka binti kaolewa. Yupo mji mwingine ndio maana wazazi wa kiafrika huona shida kwenda kwa binti....

Hivyo wakamwana jamani...muwe na upendo....muwe wavumilivu
....muwe na kiasi mkawe baraka ktk nyumba na miji muingiayo
Kabisa
Enyi binti muende mkawe baraka huko mnakolewa
Jamani for sure am proud to be born in Kilimanjaro.......
kiukweli ni heshima mama kwenda kukaa kwa mwanae wa kiume.. tena sana ila kwa mtoto wa kike labda awe hajaolewa kama ameolewa ni ngumu sana.

Na km binti ana hekima lazima awe karibu na mama mkwe wake
 
mwee kikwetu sie kumlea mama mkwe sio ombi ni lazima, na kwanini usimlee labda, huyo ndo mama mzaa chema kama unampenda mumeo lazima upende na familia yake, wala hutakiw kuuliza. yani wew ukae na mama yako kwa mumeo halaf mama yake asiwepo, hiyo haipo

ila inategemea na mila zenu na tamaduni zenu, lakin kwa ushaur kama mama mkwe yupo jivunie kuwa nae na umjali vyema, na mama yako nae atatendewa the same.
Kabisa

Mimi nina wifi yangu mama asikanyage mjini yaani anavyohaika nae mimi ni mwanaye kabisa yaani binti yake lakini siwezi yale matunzo anayopewa na mke wa kaka yangu......

Na uzuri kaka pia hapendi mama aje alale kwa dada zake hata saa tano usiku atamfuata tuu aje alale kwake....

enyi mabinti mnaolewa wapendeni sana mama wakwe zenu kama wapo hai
 
Kwa kabila letu siye utake usitake ni lazima na ukimfanyia mambo ya ajabu mama wa mumeo na mumeo akabaini kuna uwezekano mkubwa ukaachika..so dadangu acha roho mbaya wewe mlee vizuri tena muheshimu sana mama wa mumeo maana huyo mama ndo kakuzalia huyo unaemwita mume leo!
 
Sonia;
Ukiusoma uzi ulioandikwa na huyu mdada ni wazi kabisa kwamba hampendi mama mkwe wake. Ameogopa kusema tu. Swali; Hivi ka si huyu mama, huyo mume wako ungelimpata wapi?? Kwa nini ulikubali kuolewa badala ya kukaa na mamako ukamlea hadi afe ndio uolewe?
Hata angelikuwa na watoto 8 wa kike na wakiume 1 tu aliyekuoa. Wewe ndiye wa kumlea, kumtunza na kumuogesha. Ni heshima kuwa, kakuzalia mume. Mtunze kwa heshima kama unamheshimu mumeo. Ila kama ni hao wanawake wa siku hizi mnaowadharau waume zenu, hata mamake utamdharau tuuu.
Hao mawifi nao kule waendako watawakuta mama mkwe. Wawatunze

Hili neno mkuu
 
Mi mama angu, mama wa mume wote wangu. Pesa ikiwepo hata nikiwaweka wote hapa wakawa wanakula na kulala sawa.
Mi ndo dada mkubwa. Mume akiwa hapendi shauri yake. Wote wangu.
 
Jamani ni lazima mama wa mume kulelewa na mke wa mwanae hata kama huyo mama ana watoto wake wa kike wakubwa wengine wana kazi zao na wanajitegemea wenyewe? mie binafsi naona si sawa kama mama ana watoto wake wakike ni bora kuenda kukaa kwa watoto wake wa kike wamhudumie kuliko kuenda kuhudumiwa na mke wa mwanae.

Tabia ya binadamu hawezi kuhudumia mtu ambae si wake kama atakavyo muhudumia mtu wake na endapo atamuhudumia basi lazima matatizo yatatokewa yule anayehudumiwa anaweza akahisi kama hapewi huduma inayostahili kupewa hata kama mhudumu anajitahidi kwa kiasi gani. jamani wadada ambao mna mama zenu baba zenu ambao wanahitaji huduma wachukueni wazazi wenu muwahudumie wenyewe msiwasukumie wifi zenu kwani wifi zenu pia wana mama zao baba zao wanahitaji kuwahudumia vilevile. acheni kuwatafutia watu matatizo ya lazima.

Mie binafsi siwezi kumuacha mama'ngu aende kuhudumiwa na mke wa kaka yangu hali ya kuwa mie nipo. huko ni kumpa mtu mzigo huku ukijuwa kabisa mama yako hawezi akapata huduma nzuri kama utakayompa mwenyewe. mwisho wa siku mnaona watu wabaya wakati wabaya ni nyie wenyewe uwezo wa kulea wazazi wenu mnao lakini mnawapeleka kulelewa na mtu aliekutana na kaka yako ukubwani hamfahamu amelelewa vipi halafu mnaleta lawama tu.

Kina dada chukueni wazazi wenu muwalee wenyewe kama pesa ya kumtunza kaka yako atakuletea huko kwako lakini si kuenda kumuachia wifi yako kama vile yeye ndo ana haki ya kukulelea wazazi wako hali ya kuwa yeye mwenyewe ana wazazi wake wanahitaji kulelewa?

Kwanini ushindwe kumlea mzazi wako uzeeni akiwa mgonjwa mpaka umsukumie mtu baki wakati yeye alikulea kwa hali zote raha na furaha ukiwa mdogo. jamani leeni wazazi wenu wenyewe wifi zenu pia wana wazazi wao wa kuwaleaaa

Mkuu mbona unaikataa heshima kubwa uliyopewa!¿¿!

Tambua kuwa kwa makabila mengi ya Tanzania (ninayojua) msichana akishaolewa anakuwa officially ameondoka kwenye familia yake na kujiunga na familia ya mume wake. While mtoto wa kiume anabakia kuwa sehemu ya his original family tree.

Kwa hiyo mara nyingi wazazi wanaenda kulelewa/kuhudumiwa kwa mtoto wa kike aliyeolewa pale tu inapokuwa ni lazima. Hakuna option nyingine bora.

Mpende mama/baba mkwe banaa...ili upate baraka. Ina nourish mapenzi pia. Na kwenye dhoruba za kimapenzi/kimahusiano investments kama hizi zinasaidia sana.
 
Jamani ni lazima mama wa mume kulelewa na mke wa mwanae hata kama huyo mama ana watoto wake wa kike wakubwa wengine wana kazi zao na wanajitegemea wenyewe? mie binafsi naona si sawa kama mama ana watoto wake wakike ni bora kuenda kukaa kwa watoto wake wa kike wamhudumie kuliko kuenda kuhudumiwa na mke wa mwanae.

Tabia ya binadamu hawezi kuhudumia mtu ambae si wake kama atakavyo muhudumia mtu wake na endapo atamuhudumia basi lazima matatizo yatatokewa yule anayehudumiwa anaweza akahisi kama hapewi huduma inayostahili kupewa hata kama mhudumu anajitahidi kwa kiasi gani. jamani wadada ambao mna mama zenu baba zenu ambao wanahitaji huduma wachukueni wazazi wenu muwahudumie wenyewe msiwasukumie wifi zenu kwani wifi zenu pia wana mama zao baba zao wanahitaji kuwahudumia vilevile. acheni kuwatafutia watu matatizo ya lazima.

Mie binafsi siwezi kumuacha mama'ngu aende kuhudumiwa na mke wa kaka yangu hali ya kuwa mie nipo. huko ni kumpa mtu mzigo huku ukijuwa kabisa mama yako hawezi akapata huduma nzuri kama utakayompa mwenyewe. mwisho wa siku mnaona watu wabaya wakati wabaya ni nyie wenyewe uwezo wa kulea wazazi wenu mnao lakini mnawapeleka kulelewa na mtu aliekutana na kaka yako ukubwani hamfahamu amelelewa vipi halafu mnaleta lawama tu.

Kina dada chukueni wazazi wenu muwalee wenyewe kama pesa ya kumtunza kaka yako atakuletea huko kwako lakini si kuenda kumuachia wifi yako kama vile yeye ndo ana haki ya kukulelea wazazi wako hali ya kuwa yeye mwenyewe ana wazazi wake wanahitaji kulelewa?

Kwanini ushindwe kumleat mzazi wako uzeeni akiwa mgonjwa mpaka umsukumie mtu baki wakati yeye alikulea kwa hali zote raha na furaha ukiwa mdogo. jamani leeni wazazi wenu wenyewe wifi zenu pia wana wazazi wao wa kuwaleaaa
Ndugu kama ni mkristo hilo ni jukumu lako kama neno lisemavo Mpende jirani yako kama nafsi yako.Lakini sababu tuna ubinafsi mno wanadamu hatuwezi kuyafanya hayo bado tunataka kwenya mbinguni kwa kweli ni neema tu.Hilo la kumuhudumia mama wa mumeo ni sawa na umchukulie kama mama yako binafsi na ufanye kwa upendo sio ubaguzi haijalishi atakavyokuchukulia hilo ni yeye na Mungu wake.So mama yako muhudumie si umwache na pia mkwe vilevile na ndo mana kuona ni majukumu ndugu its not a joke na hapo ndo uvumilivu unahitajika .So hilo ni sawa na utakavyokua unawasaidia yatima na wote wasio jiweza kwa upendo wako wote kama Mungu asemavyo.
 
mama'ko hawezi kuwa sawa na mama wa mumeo hata siku moja. unaweza ukafanya kosa dogo tu tena si kama umedhamiria kufanya hivyo mama'ko anaweza akachukulia poa tu lakini fanya hilo kosa kwa mama wa mumeo uone litakuzwa hilo utaonekana mbaya utachukiwa maisha yako yote. kuepusha mambo kama haya bora watoto wa kike wawahudumie wazazi wao.
Me nimekuelewa ila twende tu kwenye uhalisia. Hivi mama zetu wazazi wote ndo hawana matatizo? Hakuna muda tunatibuana na mama zetu, je tunawasusa? Kama unavyoweza kumvumilia mama yako mzazi ndo na mama mkwe wako jifunze tu kumvumilia. Na kama unavyo-ignore baadhi ya makosa ya mama yako, na ya mama mkwe ya-ignore hivyo hivyo. No one is perfect, na kama mnataka mtibuane na mumeo basi lete figisu figisu kwa mama ake (unless uwe umemshikia akili). Wewe tenda tu mema yaliyo ndani ya uwezo wako, asipoappreciate kazi kwake, na uzuri hata mumeo anaona kuwa mke wangu alisimama kwenye nafasi yake. Ingawa sikatai kuwa kuna mama wakwe pasua vichwa hatare, but once ukiolewa, mama mkwe ndo anakuwa mama ako.
 
Dada angu me nadhani umeraise kitu kizuri. Ila lazima uelewe kile kilichopo na asili yake ndo ukibadilishe. Lazime ujue kwa nn utaratibu ulikua vile ulivo sasa na si vile unavyotaka ww. Hasara na faida za kila utaratibu. Judging from the history kwa haraka haraka mwanamke hua anaolewa anatoka kwao anaenda kwa mume nakila kilicho chake km ni chumba chake kinapewa mtu mwingine. Mwanaume hua anaoa anapewa na ardhi ya kujenga mji wake aishi na mkewe. Then wewe mwanamke mama mkwe wako ndo atakuonyesha ule ukoo watu wanaishije kwa kua hata yeye kwenye hua ukoo aliletwa na baba yake mumeo. Halafu kingine kihistoria mwanaueme ndo alikua anafanya kazi mwanamke alikua mama wa nyumbani majukumu yakutafuta yalikua ya mwanaume kwa jamii nyingi which means yeye ndo mwenye kipato na uwezo wa kulea familia na wazee ingawa kwa sasa wanawake pia wanatafuta na wanawake pia wanarith ardhi hizi walizonunua washua uku mjini utofauti ndo umeanzia hapo. Kwa jamii nyingi mwanaume ndio baba mwenye mji mwanamke analetwa kuendeleza ile jamii kwa kuizalia na kulea. Sasa wewe ukileta na mama ndani ya mji wa mumeo wakati mama nae aliolewa kwenye mji mwingine itakua kama vile uyo mume ameoa mama na mtoto tho alikutolea mahari ww tu. Ila mama wa mumeo ye ni wa mji ule ule wewe ulioolewa.
 
Kwa karne hii ya mwendo kasi...
mama mkwe na mkaamwana wote shida...
ingawa mila na desturi ni mzazi kukaa kwa mtoto wa kiume lakini kuna changamoto nyingi sana na pia kwa sasa tunaangalia zaidi labda wapi kuna huduma nzuri na karibu kutokana na mahitaji ya mgonjwa.
muhimu ni kujipanga na kumsoma ili ujue mipaka na namna ya kuruka viunzi.
 
mwee kikwetu sie kumlea mama mkwe sio ombi ni lazima, na kwanini usimlee labda, huyo ndo mama mzaa chema kama unampenda mumeo lazima upende na familia yake, wala hutakiw kuuliza. yani wew ukae na mama yako kwa mumeo halaf mama yake asiwepo, hiyo haipo

ila inategemea na mila zenu na tamaduni zenu, lakin kwa ushaur kama mama mkwe yupo jivunie kuwa nae na umjali vyema, na mama yako nae atatendewa the same.
Ww sasa ndo mwanamke,wanaume tupo vzr sana kwenye kurudisha favour ingawa nyie wenzetu baadhi yenu mna roho mbayaaaa almost 75%roho zao ni za kushindana shindana tu
 
kama ana watoto wa kiume tu inakuwa haina jinsi inabidi ahudumiwe tu lakini kama ana watoto halafu aende kukaa kwa mtoto wake wa kiume si vizuri. mtoto hata akiwa hajielewi hawezi kumuacha mama ateseke acheni kutafuta sababu ambazo si za kweli
Roho mbaya zenu hlf mnalalamika hampendwi
 
kumbe mnatumia hisia zaidi ya uhalisia. eti atadhalilika, atadhalilika kwa mtoto wake? wazazi ndio ni baraka kila mtu anafahamu lakini bado haina ulazima wa mtoto wa kiume alazimishe mke wake amlee mama'ke hata kama dada zake wapo na uwezo wa kufanya hivyo. mpeleke mama'ko kwa dada zako uwe unapeleka pesa na mahitaji mengine wao watamuhumia nayo pia ni baraka na uhakika wa kupata huduma nzuri ni mkubwa zaidi kuliko kwa mkeo
Unafikiria km mwanamke hlf wengi waliokushauri ni wanaume sasa fikra zako hazitoshi hizi za wanaume huu jf ndo fikra pevu ambazo znahitajika Ili uweze ishi na mume (mwanaume ) vzr Bisha ubakie na fikra zako za kibinfsi na ushindani ushindani mara mi ndo bora mi ndo bora hii nyumban ni yako sitaki mwanamke mwingne humu hlf uone km huyo mwanaume km utakae mwandama mama yake km ht atakutamani utasema mumeo adindi kisa kibri yako na majivuno ya kike
 
Sema mama mkwe usitake kuharalisha dhambi zako hapo kaja kwa mwanae wa kiume sasa wewe unaanza mara mama wa mme sema mama mkwe wako...!
 
Me nimekuelewa ila twende tu kwenye uhalisia. Hivi mama zetu wazazi wote ndo hawana matatizo? Hakuna muda tunatibuana na mama zetu, je tunawasusa? Kama unavyoweza kumvumilia mama yako mzazi ndo na mama mkwe wako jifunze tu kumvumilia. Na kama unavyo-ignore baadhi ya makosa ya mama yako, na ya mama mkwe ya-ignore hivyo hivyo. No one is perfect, na kama mnataka mtibuane na mumeo basi lete figisu figisu kwa mama ake (unless uwe umemshikia akili). Wewe tenda tu mema yaliyo ndani ya uwezo wako, asipoappreciate kazi kwake, na uzuri hata mumeo anaona kuwa mke wangu alisimama kwenye nafasi yake. Ingawa sikatai kuwa kuna mama wakwe pasua vichwa hatare, but once ukiolewa, mama mkwe ndo anakuwa mama ako.

Mpendwa nimependa haya madini ya nguvu...naamini happymsafi atazingatia huu ushauri wako.
 
Back
Top Bottom