Ni lazima kizazi hiki kipite kwanza ndipo CCM ing'oke madarakani!

we kwel haunazo,wakat mwingine ucdande kwa mbele utafanywa ka opereshen tokomeza,chama chako ni kwako vipofu wenzako,hapa naongelea Tanzania kwa mifano si vyama vyenu vya kupelekana ka misukule

Mbona povu linakutoka, tulia uogeshwe, katengeneze jeneza, tena sidhani kama utapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho, utafuatilia live tbccm.
 
Ni vigumu sana kujua maamuzi ya watanzania wote na kuanza kuwasemea hizi ni ndoto za mchana.
 
Vijana mkinywa gongo mnaota mumesimama?
Chadema mko ICU jishikeni kifua muone kama mapigo ya moyo yanadunda kama hakuna mjue mko mochwari.
 
CCM kufa ni lazima ila inaweza kuchelewa kufa lakini kifo, kiko pale pale. Nyerere mwaka 1995 aliwaambia kamati kuu ya C.C.M kwamba watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipo yapata C.C.M watayatafuta sehemu nyingine.Mabadiliko yameanza Tanzania na huwezi kuyazuia.

Watanzania watayatafuta mabadiliko popote hata kama itakuwa kwa shari. Ni kwa nini nasema C.C.M haiwezi kupona kwanza kabisa kizazi hiki cha miaka ya 1990 ni kizazi ambacho kinafuatilia taarifa na wanajua kuhoji sio kama wale waliokuwa wanafundishwa zidumu fikra za Mwenyekiti.

Pia hiki kizazi huwezi ukawaambia C.C.M imekulea maana wamekuwa wauona mfumo wa vyama vingi kwa hiyo wabunge wa C.C.M wanavyosinzia,wanavyozomea,wanavyo shabikia ujinga vijana wanaona kwa hiyo C.CM kufa ni lazima.

Pili katika kizazi hiki ambacho wanaona mafisadi,wauaji wabakaji na wauza unga wanatamba serikalini na C.C.M imewaacha watambe C.C.M haiwezi kupona.

Mtu kama Kamuhanda ameshuhudia polisi wakimuua Mwangosi halafu kesho yake akapandishwa cheo C.C.M haiwezi kupona.Cha muhimu muandae majeneza yenu.

Tatu katika kizazi ambacho babu zao walioitumkia nchi kwa uaminifu wanapigwa mabomu na maji ya pilipili kisa wazee walidai haki zao. Wazee wanalalamika mpaka wanavua nguo barabarani hakika C.C.M haiwezi kuikwepa hiyo laana fuatilia sakata la wazee wa Afrika Mashariki Tatizo la ajira haliwezi likawaacha salama.

Mtwambie hawa watu wanaomaliza vyuo mnawapeleka wapi?.Mmewasaidia namna gani?.Ofisini mnaweka vigezo eti mtu awe na uzoefu wa miaka mitano.

Huo uzoefu wanaupata wapi?Na sasa hivi mmeanzisha propaganda eti wajiajiri Je mmewapatia mtaji wa kujiajiri?.Hawa siku moja watajitoa mhanga ili kumuondoa mkoloni C.C.M. Katika kizazi ambacho kinaona C.C.M mumeua reli yetu ambayo ilikuwa msaada kwa wananchi wa chini mmeiua ili mabasi na malori yenu yafanye kazi.

Hakika yake ipo siku mtalia na kusaga meno. Katika kizazi ambacho mnasema mmeboresha elimu mwanafunzi anasoma masomo ya Sayansi na anamaliza kidato cha nne hajawahi kuiona ‘’Test tube’’.

Huyu hatawaacha lazima C.C.M mtambe. Mnadai mmeboresha huduma za Afya mbona nyie kucheki afya mnaenda Afrika ya Kusini, India, Uingereza na Marekani.Piteni hospitalini muone mgonjwa mmoja anamlalia mwingine. Mara unaambiwa hospitali hazina dawa .

Ila nawapongeza maana wakati wa msiba mnaonyesha huruma lakini hiyo haitawasaidia. Mama Ntilie mnawakimbiza usiku na mchana machinga hawana raha na maisha yao wakati wa uchaguzi mtawaambia nini? Hakika yake kifo cha C.C.M ni lazima Hivi hii kilimo kwanza mmemsaidiaje mkulima?mbona wakulima wa pamba,korosho,kahawa, kila siku wanalia mbona kuna sehemu nyingine Tanzania bado kuna tatizo la chakula tukiuliza mnatuambia tulime kilimo cha kisasa.

Je hicho kilimo mmetufundisha? Hakika siku ikifika mtawaambia nini wakulima? Zamani walimu walikuwa wapiga kampeni wenu siku hizi mmewageuka . Mishahara yao midogo madai yao hawalipwi nasikia wanapigwa hadi viboko .

Je mna uhakika kama mmegeukwa na walimu ambao wamesambaa nchi nzima mtapona? Jiandae kwa ajili ya kifo cha ukweli.

Haiwezekani ndani ya nchi ya Kidemokrasia kama Tanzania watu wanapigwa mabomu,watu wanang’olewa kucha,watu wanamwagiwa tindikali, halafu Waziri Mkuu mwenye akili timamu anasema watu wapigwe tu kisa yeye kachoka.Na tumesikia juzi Mawaziri wamejiudhuru yeye kaendelea kuwa Waziri Mkuu. Hakika yake kwa sababu mliruhusu watu kupiga na kuua.

Siku moja mtapigwa nyie maana apandacho mtu ndicho avunacho. Wanafunzi hawa wote wanaopata daraja 0 hawa wote ni zao lenu na lazima siku moja ndio watasimama na kuwapiga chini.

Hakika yake siku hiyo hamtaamini lakini ndio itakuwa imetokea. Wakati wa Mwalimu Nyerere tulikuwa na viwanda vya nguo,viatu hadi redio siku hizi mmeua vyote.Ajira ndio hivyo zimeondoka kazi yenu ni kubinafsisha kila kitu mwisho mtabinafsisha hata wake zetu hakika yake C.C.M haitapona.

Suluhisho ni C.C.M kuwaomba msamaha watanzania na kuamua kugeuka. Msipofanya hivyo jiandae kuondoka kwa kilio na kusaga meno.

Imeandikwa na MCHUNGUZI .J. NAMALA 0776655066

wakipona?
 
Katika kitu ambacho kimeniuma na kimenisikitisha sana ni wanafunzi wa vyuo vikuu wa nchi hii mwaka 2010 walinyimwa kwa makusudi kupiga kura na hawakuonyesha kukerwa na tukio hilo. Kama wasomi hawawezi kutetea haki zao kuleta mapinduzi na mageuzi yanayohitajika nchi hii watawezaji kututetea sisi? hawa ni wasomi wa nchi ambao wanachukua viti katika maofisi hawawezi kutetea haki yao. Kunyimwa kupiga kura ni kunyimwa haki yako ya msingi katika nchi ya kuchagua kiongozi wako.

Maana yake anayenyimwa kupiga kura ni mtu ambaye siyo raia wa nchi. Hii aibu ya wasomi wetu tunaweza kufananisha na nini? Mfano wake ni kama wasaka tonge tu hawana faida katika nchi hii machoni kama watu, midomoni wanaongea maneno matamu kumbe mioyoni wamejaza ulaghai mtupu hawa nia afadhali wasipata nafasi hii adimu ya kusoma.

Hakuna kijana anayeweza kutetea wanyonge wanawaza hela hata kwa njia haramu. Je akina samweli sita hawakumwonyesha julius nyerere kwamba hawakubaliani na jinsi alivyopanga ujamaa uwe? na je baada ya kusikilizwa nyerere hakutumia pepa ya akina sita kuandaa azimio la arusha?


mbona kwa hili la katiba wasomi wanafunzi hatuoni usomi wenu katika hili katika malumbano ya katiba? mchango wenu uko wapi kwa maslahi ya wanyonge nje ya bunge? ccm wanaburuza nchi usomi wenu uko wapi vijana

Nasema sio wote ila hao wachache tuonyeshe kiburi aliyosema baba wa taifa ambayo vijana tunakiwa kuwa nayo ni kiburi ya kukataa mifumo kandamizi kwa jamii.

Nawasilisha kwa mjadala.
 
Back
Top Bottom