Ni kweli wanaume hukwepa kuvaa pete za ndoa?

Ni kweli wanaume hukwepa kuvaa pete za ndoa?

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,464
Jamani waungwana hivi kuna ukweli kwa hili?

Mimi binafsi toka nimeoa navaa pete na niko huru nayo tu, na sioni ajabu pia, lakini nina rafiki yangu kaoa yeye daima hapendi hii kitu, tena zaidi anavaa akiwa kwake tu, na kiuchunguzi changu kidogo nimegundua vijana wengi hawapendi kuvaa sijajua kama kwa sababu gani.
 
Nilipoona kichwa cha habari tu nikajua atakua ameuliza mwanamke,anyway waliooa watajibu.
 
Nilikua na mfanyakazi mwenzangu yeye alipoona mumewe kavua pete nae akavua so wote hawavai pete zao za ndoa, anyway kuvaa pete kuna raha yake bana though siku hizi pete haziheshimiki kabisa, mtu anaweza tongoza au kuchepuka na pete yake inang'aa bila aibu yoyote
 
Wananikera kweli wanaume waliooa afu hawavai pete... Sijui kwanini hawajiamini....

Kuna mchezaji mmoja jina nimesahau alikuwa anaibusu pete yake kila mara kama ishara ya kukumbuka agano lake na mkewe...
 
mie mpaka nakufa sivai pete kabisa yaani sijui hata nilipoitupia.
 
wengine tuna aleg nazo... zinatuongezea joto tu mwilini!!!
 
Nivae ya huku chini na ya vidoleni tena? Khaa!!!
 
Mi bro wangu kaoa juzi juzi basi hadi kero home full mashauzi kila akiongea anaonyeshea ishara ya kidole kilichovaa pete, akijichokonoa jino hivo hivo...watu tukasema subiri ndoa ifikishe mwaka atavua mwenyewe!
 
Kwani haikuwa ya vito vya thamani? Usingeitupa ukampa mwenza wako atengenezewe hereni bwana.
(nime-presume wewe mwanaume)
mie mpaka nakufa sivai pete kabisa yaani sijui hata nilipoitupia.
 
Niliwahi kumuuliza shosti why havui pete na mwanaume wametengana zaidi ya 5yrs. Akaniambia pete inampandisha hadhi. Mwanaume anaetongoza mke wa mtu shurti awe anajiamini vya kutosha. Na hasemi wametengana, anasema mume yuko masomoni.

Usije ukamuuliza mkeo kwa nini anavaa pete. Ana hesabu zake, hehehe
Tena mtu asinisumbue kuhusu pete, siitaki.
 
Niliwahi kumuuliza shosti why havui pete na mwanaume wametengana zaidi ya 5yrs. Akaniambia pete inampandisha hadhi. Mwanaume anaetongoza mke wa mtu shurti awe anajiamini vya kutosha. Na hasemi wametengana, anasema mume yuko masomoni.

Usije ukamuuliza mkeo kwa nini anavaa pete. Ana hesabu zake, hehehe
Dada yangu, pete ni ishara ya upendo. Japo shostito wako ameachana na hubby wake, inawezekana kabisa bado anampenda.
Wife huwa ananiambia, kwa nini huvai pete, nikiwa na wewe nahisi watu wanahisi sisi ni michepuko. Nacheka tu, upendo wangu upo moyoni, nadhiri yangu imejengwa nafsini. Siku hizi na Pete zetu tunadanganya (cheat) sana tu.
 
Mi bro wangu kaoa juzi juzi basi hadi kero home full mashauzi kila akiongea anaonyeshea ishara ya kidole kilichovaa pete, akijichokonoa jino hivo hivo...watu tukasema subiri ndoa ifikishe mwaka atavua mwenyewe!
Unamuonea bro wako wivu, teh(joke!!)
 
Hii muhimu hii. Mimi ya kwangu kwa kweli navaa na nipo comfortable. Sababu hata kama ni mchepuko huwa sifichi kuwa I have a family.
 
Attachments

  • 1449892578058.jpg
    1449892578058.jpg
    34.6 KB · Views: 469
Back
Top Bottom