Ni kweli wanaume hukwepa kuvaa pete za ndoa?

Ni kweli wanaume hukwepa kuvaa pete za ndoa?

Mimi saa, cheni, mapete vidoleni sipendi.
Ila kuna rafiki yangu hajaoa ila anavaa aliniambia ni njia salama n ya kiutu uzima kukamatia wadada mjini cz wanajua lazima atakuwa mtu smart n responsible pia. Jamas anawapiga kinoma
 
Unajikontradikti kaka. Umesema pete ni ishara ya upendo? Kwa hiyo wewe humpendi mkeo ama hupendi kutoa ishara?
Dada yangu, pete ni ishara ya upendo. Japo shostito wako ameachana na hubby wake, inawezekana kabisa bado anampenda.
Wife huwa ananiambia, kwa nini huvai pete, nikiwa na wewe nahisi watu wanahisi sisi ni michepuko. Nacheka tu, upendo wangu upo moyoni, nadhiri yangu imejengwa nafsini. Siku hizi na Pete zetu tunadanganya (cheat) sana tu.
 
Unajikontradikti kaka. Umesema pete ni ishara ya upendo? Kwa hiyo wewe humpendi mkeo ama hupendi kutoa ishara?
Ndio nikasema, yangu imefichwa moyoni. Sio lazima kila mtu aione ili kujidhihirisha kuwa nampenda mke wangu. Muhimu ni kuishi zile ahadi mlizopeana wakati mnasema "YES, I DO". BTW, hilo neno ni zito sana...
 
Hahaa kwanza ungeuliza ni mwanaume gani anaweza kujitangaza kuwa ameoa kama ambavyo wanawake hujitangaza kwa fahari kuwa wameolewa.. Kwa mwanaume Ndoa ni kama jela na kitu kikubwa tunachopenda katika Ndoa ni watoto... Lakini Mwanamke anachukulia Ndoa kama uthibitisho kuwa na yeye ni mzuri, yupo aliyempenda na kummiliki...na Pete Ya Ndoa ni ishara Ya wazi kwa hilo
 
Jamani waungwana hivi kuna ukweli kwa hili? Mimi binafsi toka nimeowa navaa Pete na niko huru nayo tu, na sioni ajabu pia, lakini nina rafiki yangu kaowa yeye daima hapendi hii kitu, tena zaidi anavaa akiwa kwake tu, na kiuchunguzi changu kidogo nimegundua vijana wengi hawapendi kuvaa sijajua kama kwa sababu gani
kwa dini ya kiislamu nadhan kuvaa pete si lazima utavaa kama ukipenda ila ndo hivyo wengi hawataki kwa sababu wanaogopa zitawaharibia kwa michepuko
 
Kwani haikuwa ya vito vya thamani? Usingeitupa ukampa mwenza wako atengenezewe hereni bwana.
(nime-presume wewe mwanaume)

mie mwanamke bwana,
hapana inabidi tu itunzwe ndani unajua uzee ukifika mahaba uanza upya hivyo itavaliwa.
 
Wananikera kweli wanaume waliooa afu hawavai pete... Sijui kwanini hawajiamini....

Kuna mchezaji mmoja jina nimesahau alikuwa anaibusu pete yake kila mara kama ishara ya kukumbuka agano lake na mkewe...

nadhani wanaume wanapenda kuowa muda ule tu wajulikane wameowa baaada ya hapo huwa hawataki tena kujulikana wameowa,
 
Kuliko idondoke chooni wakati ameiweka mfuko ndo maana wanavua.
 
Wananikera kweli wanaume waliooa afu hawavai pete... Sijui kwanini hawajiamini....

Kuna mchezaji mmoja jina nimesahau alikuwa anaibusu pete yake kila mara kama ishara ya kukumbuka agano lake na mkewe...

Raul Gonzalez..anyway wengi tunaogopa kutokewa na mademu vicheche wapenda waume za watu. usipovaa wanakuona msela haunaa dili
 
mbona watu wanavaa na michepukoni wanaenda. tena inasaidia mchepuko anajua una mke so vigezo na masharti anazingatia
 
Hii muhimu hii. Mimi ya kwangu kwa kweli navaa na nipo comfortable. Sababu hata kama ni mchepuko huwa sifichi kuwa I have a family.

Tena michepuko wanapenda sana watu wanaovaa pete zao wakiamini kuwa wameoa/wameolewa na hivyo basi wana uwezo mzuri wa kulea na kumtunza mtu na pia usiri kati yao utakuwepo.
 
Wananikera kweli wanaume waliooa afu hawavai pete... Sijui kwanini hawajiamini....

Kuna mchezaji mmoja jina nimesahau alikuwa anaibusu pete yake kila mara kama ishara ya kukumbuka agano lake na mkewe...

Raul Gonzalenz wakati yupo real madrid
 
Nilikua na mfanyakazi mwenzangu yeye alipoona mumewe kavua pete nae akavua so wote hawavai pete zao za ndoa, anyway kuvaa pete kuna raha yake bana though siku hizi pete haziheshimiki kabisa, mtu anaweza tongoza au kuchepuka na pete yake inang'aa bila aibu yoyote

Ni Rahisi kutongoza ukiwa umevaa Pete kuliko ukiwa huna pete
 
Mimi saa, cheni, mapete vidoleni sipendi.
Ila kuna rafiki yangu hajaoa ila anavaa aliniambia ni njia salama n ya kiutu uzima kukamatia wadada mjini cz wanajua lazima atakuwa mtu smart n responsible pia. Jamas anawapiga kinoma

Exactly, mademu wengi hapa mjini ni mademu za watu hivyo ukiwa na pete anajua mtaenda sawa
 
Jamani waungwana hivi kuna ukweli kwa hili? Mimi binafsi toka nimeowa navaa Pete na niko huru nayo tu, na sioni ajabu pia, lakini nina rafiki yangu kaowa yeye daima hapendi hii kitu, tena zaidi anavaa akiwa kwake tu, na kiuchunguzi changu kidogo nimegundua vijana wengi hawapendi kuvaa sijajua kama kwa sababu gani

Kwa some married couples kutokuvaa Pete ujue wana plan zao B that's it .. Kama hawakutaka jukumu la kuvaa rings ( na kuziheshimu, maana some huvaa and still are cheating .) then wasingeoa or kuolewa period.. Thanks .
 
Back
Top Bottom