Ni Kweli wamethubutu, Ni kweli wamejaribu, na ni kweli wameweza lakini hawako makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Kweli wamethubutu, Ni kweli wamejaribu, na ni kweli wameweza lakini hawako makini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uswe, Oct 16, 2011.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nimekua nikiwaza mambo mbalimbali yaliyotokea, almost yote yameongelewa sana humu, nimekua nikijiuliza, watanzania tumekosea wapi? sipati jibu.

  Wakati flani nilikua naongea na baba yangu (mzazi) ye akasema inawezekana ni kwa sababu tanzania hatukuanza na Mungu, i mean kwamba babu zetu badala ya kumtanguliza Mungu wao wakawa watu wa kutambikia mizimu tu.

  Lakini mbona wengine wamebarikiwa ili hali hawakuanza na Mungu, Kwa nini Mungu aamue kuiadhibu Tanzania kwa kiwango kikubwa hivi?

  Nikiwaza haya roho inaniuma sana, hivi hawa viongozi hawaoni kwamba wakiacha kijilimbikizia mali (ambazo watakufa na kuziacha) wanaweza kuifanya Tanzania nchi nzuri sana kuishi.

  Mtanzania anaefanya kazi kama analipwa 1M, laki tatu zinarudi serikalini kama DIRECT TAX na hizo saba zilizobaki zinapigwa INDIRECT TAX kila ninaponunua kitu dukani, hata iwe maji ya kunywa pamoja na tozo mbalimbali

  Kwa kifupi kwa kila mtanzania anayelipwa mshahara, anarudisha serikalini zaidi ya asilimia 50 ya kipato chake kama kodi na tozo mbalimbali, HIZI PESA ZINAFANYA KAZI GANI?


  Mbali na kodi ambazo ni kubwa sana, tanzania ni nchi yenye resources nyingi sana, madini, bahari, ardhi, wanyama, gas nk hivi vitu vinatufaidishaje? haingii akilini kwamba miaka 50 ya uhuru Tanzania kuna mgao wa Umeme, TUMEKOSA UONGOZI KABISA!

  Wamethubutu ni kweli, wamejaribu ni kweli, na wameweza ni kweli lakini hawako makini na si wabunifu, miaka 50 hakuna kitu cha maana pamoja na kwamba wananchi tunafunga mkanda kuchangia serikalini na tuko na resources nyingi sana
   
 2. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  You are right MKUU,lakini solution itapatikana 2015 kama ni kweli tumechoshwa na UONEVU huu.
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  na kama tutajitahidi kuzuia kuingizwa kwa karatasi zile za toka china town
   
 4. m

  mharakati JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  he he chinese wako kwa ajili yetu..CCM kuachia dola ni kama CDM wakipata 70% ya vote zote hapo hata wizi utawaumbua CCM watakubali kwa shingo upande
   
 5. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Mh! na hii tume ya uchaguzi? labda ichaguliwe tume huru.
   
 6. f

  firehim Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu ahsante sana kwamba umeliona hilo. Tatizo linalloikumba nchi yetu siyo uchache wa kodi ni uwezo mdogo wa kufikiri na kujua tunahitaji nini baada ya muda gani. Na hii inatokana na hizi sera za kuongozwa na chama kimoja hazina maana kwa manufaa ya taifa ila zina maana kwa wale wenye kufaidika na chama husika kwani wanapata fursa ya kulindanana na kufichiana maovu. Kama taifa tunahitaji kuwa na vision moja ambayo kila mwanasiasa haijalishi ni wachama gani itaifuata. Tuachane na hizi sera za AHADI. Sisi kama walipa kodi tusiwe mbumbumbu. Tujitokeze tuulize ni kwa nini tuko hapa ili hali tunalipa kodi kila siku. KATIBA MPYA NI SULUHISHO.
   
 7. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  katba mpya ndio suluhisho but kwa muda gani kukamilika na kutatua kero zetu?
   
 8. f

  firehim Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunatakiwa kuidai. Tunahitaji maendeleo nasi tuwe miongoni mwa nchi zinazoendelea. Kero haziwezi kuisha kwa siku moja ni kweli ila lazima uwe na muono (vision) ambayo itakufikisha unakoenda. Sio hii zima moto tunayoenda nayo. Na vision ya nchi lazima aijue kila mtanzania. Ajue wapi tunaenda na tutafika lini. Isiwe mikononi mwa wanasiasa iwe mikononi mwa wananchi mwanasiasa awe ni msimamizi tu. Huwezi ukafika kesho kama hujaanza leo
   
Loading...