Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
About 4 years back, nilienda Nairobi, wakati natembea downtown mchana, walinitokezea mijitu minne mirefu na meusi titii! Ilinizunguka huku wakiwa na visu, sikutaka kuleta kukuru kakara kwa kuwa nilihofia watanidhuru, walinisachi na kunichukulia simu na wallet iliyokuwa na 700 usd na kupotea huku kukiwa na watu wengi sana, lakini nobody cared!.. Nilifanikiwa kurudi Dar, nikakutana na rafiki yangu mmoja Mkenya nikamsimulia masibu yaliyonikuta, kisha nikamuuliza kwa nini ile mijizi imeacha watu wote na kunivamia mimi? Alichonijibu kiliniwacha hoi, Aliniambia kuwa wale wezi kabla hawajamvamia mtu kwanza wanaangalia WALKING SYSTEM yake, Na WALKING SYSTEM ya Dar is quite different from Nairobi, na akaniambia pia kuwa kama huamini nenda Msimbazi round about uangalie watu wanavyotembea! Utawaona wanaburuza miguu kama misenge misenge!....Wana JF kuna ukweli wowote ya juu ya hili jambo??