Ni kweli umeondoka kipenzi?

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
6,764
13,815
Wasalaam,

Maisha ya mwanadamu yamejawa na matukio mengi ya huzuni, furaha, majonzi, kukata tamaa ya kuishi n.k
Hii ni story ya kweli iliyonikuta ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Ilikuwa kipindi cha mwisho wa mwaka Kama hiki, nikiwa "kisiwani" kwenye shughuli zangu za "wageni". Asubuhi na mapema nikifanya mazoezi ya mwili kwenye fukwe ya bahari. Karibu na sehemu moja ya kulaza wageni iliyopo fukweni hapo.

Macho yangu yanakutana na binti mmoja wa kihalf-caste, akionekana kutokea kwenye "bungalows", mashaalah! Niliduwaa, alikuwa mzuri wa sura, rangi yake ya "kicapuccino" ilizidi kunifanya nizidi kumkodoloe macho, alikuwa akitembea kuelekea kwenye viti vya fukweni karibu na nilipokuwa.

Niliendelea kufanya mazoezi wakati huu nikimuangalia kwa jicho la wizi wizi huku yeye akiwa busy na simu yake, sikutaka ajue Kama ninamuangalia.

Punde anatokea kijana muhudumu aliyekuwa anafanya usafi wakati huo kwenye restaurant, wanazungumza kidogo na yule kijana anaondoka. Baada ya muda naona anarudi na beer za Kilimanjaro mbili, ilibidi nipause kidogo, nikiduwaa, haikuwa kitu cha ajabu, lakini sikutegemea kuona kutoka kwa msichana yule, imagine ni saa moja kasoro asubuhi hiyo.

Wakati naendelea kushangaa ghafla anageuka upande wangu na macho yetu yakakutana, nikaona anatabasamu, damn it! "Let me take my shot" nikajisemea moyoni, nikainuka kujipangusa mchanga, huku nikielekea alipoketi.

Namsogelea karibu nakaribishwa na macho yake makubwa yaliyokaa kimahaba, huku uzuri wake ukinogeshwa na nywele zake za "singa singa" zikiwa na rangi ya blonde.
"Hi, naitwa mla Bata" nikajitambulisha kwa kujiamini, "naitwa Maggie, (si jina halisi) karibu" nilishangaa kusikia ana fluent nzuri ya kiswahili, nikapata kwa kuanzia.

Baada ya chit-chat ya muda mfupi ndio nilipojua kuwa alikuwa ni half Tanzanian, half European (sitoitaja nchi), wakati nikiendelea na small talks huku nikitaka attention yake ghafla namuona muhusika (manager) wa sehemu ile akija kuelekea pale tulipokuwa, anafika na kusalimia na kuanza maongezi na yule "mgeni" nikasema mambo yasiwe mengi ngoja niwapishe.

Baada ya mazungumzo ya muda fulani naona yule dada anainuka (sura yake ikionekana na hasira wakati huu) anaondoka na kuelekea vyumbani. Nikasubiri kwa muda arudi ili nikazungumze nae nipate walau mawasiliano yake, ikizingatia muda wangu wa mazoezi ulishaisha.

Dakika 15, 20, nusu saa, hola nikasema ngoja niende pale alipokaa labda naweza kukuta ujumbe wowote wa kunihusu😅, kufika pale nikapiga jicho la haraka haraka kuona Kama kuna chochote, hakuna nilichokikuta zaidi ya packet la embassy.

Ikabidi nisogee pale restaurant kuongea na yule kijana walau naweza kupata dondoo zozote.

Moyo wangu ulipasuka kusikia kuwa yule mgeni alikuwa amekwisha ondoka, mbaya zaidi hakukuwa na mawasiliano yoyote, nilijiona mjinga na nisie na bahati, mwili uliishiwa nguvu, nikajikokota kuondoka pale fukweni huku nikijikatia tamaa ya kumuona tena yule mrembo aliyeuteka moyo wangu kwa muda mfupi Sana.


Inaendelea...

Part Two: Ni kweli umeondoka kipenzi?

Part Three: Ni kweli umeondoka kipenzi?

Part Four: Ni kweli umeondoka kipenzi?

Part Five: Ni kweli umeondoka kipenzi?

Part Six: Ni kweli umeondoka kipenzi?

Part Seven (Mwisho):
Ni kweli umeondoka kipenzi?
 
Inaendelea.......

Wiki inapita, wiki mbili, naelekea zangu atm, kuna mtu anatoka ATM inabidi nimpishe apite, Siamini macho yangu...ni yeyeeee! Anatoka ATM uso kwa uso tunakutana, furaha yangu inachanganyika na sintofahamu baada ya kuona macho yake yamejawa na machozi, namsalimia, hanijibu, anaondoka kwa kasi.

Namkimbilia huku nikisahau kilichonipeleka pale, namuomba tusogee kivulini ili anieleze kilichomsibu, anakubali kwa shingo upande. Tunaenda chini ya mti ulio karibu na eneo lile na kuanza kumuhoji, nini shida?

Hataki kuzungumza, anasema Kama nataka nimsaidie basi niende nikamnunulie beer mbili itakuwa nimefanya jambo jema Sana, at the same time nasikia anasmell beer, na ukimuona unaona hayupo sawa, nagundua she's stressed.

Nikamuomba anisubiri, naingia ATM narudi namkabidhi 20k namwambia naomba ukanywe hizo beer but let's meet later in evening Kama hutojali,
Ananipa namba zake, moyoni nilijiona mshindi.

Mida ya jioni, baada ya kumaliza majukumu yangu, navuta simu nakumpigia, tunapanga appointment ya kuonana. Moyo wangu unajawa na furaha, bado najiona mshindi.


Itaendelea...

Carrasco putin , Shimba ya Buyenze
 
Inaendelea.....

Muda unawadia, nakwenda kumpick, she was with the same dress, kilichoongezeka ilikuwa ni beer kichwani tu, nachagua sehemu tulivu nje ya mji tunafika na kuagiza vinywaji. Haonekani kutosheka na pombe, haonekani kulewa.

Anasimulia,
Amezaliwa na baba Mtanzania na mama mzungu, huko ughaibuni, wakati baba yake akiwa kikazi huko, mama yake anatengana na baba yake, baada ya miaka kadhaa mzee wake anarudi nchini, anabaki na mama ake pekee ughaibuni.

Wakati anafikisha miaka 15 anagombana na mama ake na anaamua kuondoka nyumbani, anakuwa mtoto wa mtaani, baada ya muda anajiunga kwenye vikundi maalumu vya kutetea ubaguzi wa rangi na kuanza kuwa chini ya taasisi huku akiendelea na masomo yake.

Wakati mama ake akimtamfuta na kumsihi arudi nyumbani, yeye anaendelea ku"hustle" na maisha yake, huku muda mwingi akitumia kwenye movements za kutetea "people of color".

Miaka inaenda huku muda mwingi akitumia kufanya kazi kwenye restaurants, kumbi za sinema n.k, she started to save. Anahitimu masomo yake na anaamua kwenda kujiendeleza nchi tofauti na hiyo.

Wakati akiwa ugenini tayari ashakuwa msichana mkubwa sasa, anaanza mahusiano kwenye mtandao na kijana wa nchi yake ambae walikutana college (akiwa nyumbani). Mahusiano yanazidi kunawiri huku kijana akiuteka moyo wa binti.

Masikini hakuyajua mapenzi, he was her first lover (kwa maelezo yake). Miaka inakwenda and she made herself a boss, anaanzisha Tech initiative company na inafanya vizuri.
Baada ya muda wanaamua kufanya maamuzi na the guy, jamaa anaamua kureallocate kumfuata binti ili waweze kuishi pamoja.


Itaendelea....
 
Inaendelea....

The guy anafika kwa binti, anapokelewa kwa mapenzi mashamsham, wanaanza kuishi pamoja, ikumbukwe at this time tayari Maggie ana muda mrefu huku ugenini, tayari ameshapata Permanent resident na yupo hatua za mwisho kuchukua uraia wa nchi husika, wakati jamaa ndio Kwanza mgeni na kamba mguuni, simply Maggie alikuwa ndio Kila kitu kwa jamaa, corner zote za mji akamuonyesha na kumtambulisha kwa rafiki zake.

After seven years of dating wanaengage, binti Pete kidoleni wakijiandaa kuwa mke na mume. Huku the guy akiwa tayari ni sehemu ya kampuni, wananunua apartment na inaandikwa jina la the guy.

*************************************

Ananyamaza kusimulia huku machozi yakimtililika, naendelea kufanya kazi ya kumbembeleza, wakati huo tayari beer zisizo na idadi zishakatika kwa Kila mmoja wetu.

Anaendelea kulia huku this time sauti ikizidi mpaka waliokuwa karibu yetu wanaanza kugeuza shingo, naamua kumsogelea na kumuweka kifuani.

Yeeeah! Nafanikiwa kumtuliza huku nikisikia ile mihemo ya uchungu na hasira bado, I felt her. Lile joto la kumbato na zile sauti za kihisia ukijumlisha na zile beer, tukajikuta tumezama kwenye romance nzito bila kujali walimwengu.


Itaendelea.....
 
Ni heri mtu ukangoja upate free time, umetulia zako home huna mzuka wa kutoka then unaandika kisa chako vizuuri unaweka bandiko lako.

Hizi itaendelea taendelea Zinakata stimu sana.

Mtu unakuta headline imekaa kihuzuni huzuni, unaamua hebu nione huyu mtu anapitia maswahibu gani tena labda naweza mshauri chochote hata kumtia moyo.

Then unakutana na itaendelea kila paragraph mbili.
 
Inaendelea...

Baada ya kuengage muda unapita Maggie anakuja kugundua baadhi ya sintofahamu kati ya fiance wake na rafiki wake wa karibu, ikawa ngumu kuamini kirahisi kwa kuwa hakuwa na ushahidi, akapiga moyo konde huku akiendelea kuignore zile feelings, lakini za mwizi ni arobaini, wahenga walishasema.

Maggie anakuja kumfumania the guy na rafiki yake kipenzi, tena kwenye apartment na kitanda alichonunua kwa pesa zake mwenyewe.

Hasira za kizungu, simu inapigwa kwa wazazi wa pande zote mbili na Maggie anaamua kumvulia jamaa Pete, anachukua begi la nguo na kuacha Kila kitu Safari ya kuja Tanzania inawadia.

*******************
Baada ya kufika Bongo anakwenda kwa mzee wake na kumsimulia Kila kitu, Mzee anamshauri binti yake akae nyumbani ili apate muda wa kuspend na familia labda itampunguzia stress,

Maggie hataki kuelewa hilo, she is really stressed, anaingia kwenye matumizi ya pombe kupindukia, wakati yupo kwao, the guy anaamua kufunga safari kutoka ughaibuni kuja bongo kuomba msamaha na kumchukua mchumba wake.

Kufika bongo, the guy anafanikiwa kuonana na Maggie lakini Maggie anakuwa mbogo, hasikii la mwanzini Wala la mnadi swala. Jitihada za jamaa zinagonga mwamba anaamua kurudi ughaibuni.

Baada ya safari muda mrefu kujiponya, wakati huu stress zinampeleka Maggie kisiwani.
Pombe na yeye, yeye na pombe Mpaka siku namtia machoni kwa mara ya Kwanza pale fukweni.

Ni Nini kilikuwa kinamliza Maggie pale ATM?

Itaendelea...
 
Inaendelea....

Baada ya jitihada za jamaa kugonga mwamba anaamua kurudi Ughaibuni, muda unapita hamna mabadiliko yoyote, sio simu wala emails zinazojibiwa. Finally jamaa anaona Kama mbwai na iwe mbwai tu anaamua kublock bank account ya Maggie ambayo walikuwa wakitumia wote "joint account".

Lengo ikiwa ni kumkomoa, aishiwe pesa arudi ughaibuni warudiane.
Hii ilimuumiza sana Maggie na kumfanya atoe machozi ya uchungu, pesa zake/zao, jasho lake lakini jamaa anamkatia access, WHY?

Baada ya kugundua hilo anatoka ATM kwa kilio cha uchungu mpaka nakutana nae.

***************************************

Nilishikwa na uchungu Kama binadamu, hisia za huruma zilizidi hisia za mapenzi, nikaanza kumuhurumia na kumpa maneno ya faraja.

Mpaka kufikia wakati huo ni watu wachache tu ndio tulibakia pale bar, kucheki muda ilikuwa inakaribia saa Saba, ikabidi tufanye utaratibu wa kwenda kupumzika. Kutokana na hali tuliyokuwa, ulevi, uchovu na muda ukiwa umeenda tuliamua kuchukua chumba karibu na maeneo yale.

Licha ya hali ya uzuni na hisia za huruma nilizokuwa nazo lakini nilipata kuenjoy uzuri na "utamu" wa Maggie, hakika ilikuwa usiku wa kipekee sana baina yetu. Na mwanzo wa "ukaribu wetu" wa muda mfupi.
 
Back
Top Bottom