Ni kweli umeondoka kipenzi?

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
6,764
13,815
Wasalaam,

Maisha ya mwanadamu yamejawa na matukio mengi ya huzuni, furaha, majonzi, kukata tamaa ya kuishi n.k
Hii ni story ya kweli iliyonikuta ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Ilikuwa kipindi cha mwisho wa mwaka Kama hiki, nikiwa "kisiwani" kwenye shughuli zangu za "wageni". Asubuhi na mapema nikifanya mazoezi ya mwili kwenye fukwe ya bahari. Karibu na sehemu moja ya kulaza wageni iliyopo fukweni hapo.

Macho yangu yanakutana na binti mmoja wa kihalf-caste, akionekana kutokea kwenye "bungalows", mashaalah! Niliduwaa, alikuwa mzuri wa sura, rangi yake ya "kicapuccino" ilizidi kunifanya nizidi kumkodoloe macho, alikuwa akitembea kuelekea kwenye viti vya fukweni karibu na nilipokuwa.

Niliendelea kufanya mazoezi wakati huu nikimuangalia kwa jicho la wizi wizi huku yeye akiwa busy na simu yake, sikutaka ajue Kama ninamuangalia.

Punde anatokea kijana muhudumu aliyekuwa anafanya usafi wakati huo kwenye restaurant, wanazungumza kidogo na yule kijana anaondoka. Baada ya muda naona anarudi na beer za Kilimanjaro mbili, ilibidi nipause kidogo, nikiduwaa, haikuwa kitu cha ajabu, lakini sikutegemea kuona kutoka kwa msichana yule, imagine ni saa moja kasoro asubuhi hiyo.

Wakati naendelea kushangaa ghafla anageuka upande wangu na macho yetu yakakutana, nikaona anatabasamu, damn it! "Let me take my shot" nikajisemea moyoni, nikainuka kujipangusa mchanga, huku nikielekea alipoketi.

Namsogelea karibu nakaribishwa na macho yake makubwa yaliyokaa kimahaba, huku uzuri wake ukinogeshwa na nywele zake za "singa singa" zikiwa na rangi ya blonde.
"Hi, naitwa mla Bata" nikajitambulisha kwa kujiamini, "naitwa Maggie, karibu" nilishangaa kusikia ana fluent nzuri ya kiswahili, nikapata kwa kuanzia.

Baada ya chit-chat ya muda mfupi ndio nilipojua kuwa alikuwa ni half Tanzanian, half European (sitoitaja nchi), wakati nikiendelea na small talks huku nikitaka attention yake ghafla namuona muhusika (manager) wa sehemu ile akija kuelekea pale tulipokuwa, anafika na kusalimia na kuanza maongezi na yule "mgeni" nikasema mambo yasiwe mengi ngoja niwapishe.

Baada ya mazungumzo ya muda fulani naona yule dada anainuka (sura yake ikionekana na hasira wakati huu) anaondoka na kuelekea vyumbani. Nikasubiri kwa muda arudi ili nikazungumze nae nipate walau mawasiliano yake, ikizingatia muda wanting was mazoezi ulishaisha.

Dakika, 15, 20, nusu saa, hola nikasema ngoja niende pale alipokaa labda naweza kukuta ujumbe 😅, kufika pale nikapiga jicho la haraka haraka kuona Kama chochote, hakuna nilichokikuta zaidi ya packet la embassy.

Ikabidi nisogee pale restaurant kuongea na yule kijana walau naweza kupata dondoo zozote.

Moyo wangu ulipasuka kusikia kuwa yule mgeni alikuwa amekwisha ondoka, mbaya zaidi hakukuwa na mawasiliano yoyote, nilijiona mjinga na nisie na bahati, mwili uliishiwa nguvu, nikajikokota kuondoka pale fukweni huku nikijikatia tamaa ya kumuona tena yule mrembo aliyeuteka moyo wangu kwa muda mfupi Sana.


Itaendelea......
 
Back
Top Bottom