Ni kweli Tanzania tunafahamika dunia nzima?

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,654
2,000
Huwa nawasikia CCM wakiongea ni kama vile jambo linalofanywa na chama chao hapa Tanzania huwa linaleta Mwangwi dunia nzima. Kwa mfano hata suala la Makinikia ilisemwa "magufuli atikisa dunia" kwa maamuzi yake ya kuzuia makinikia kusafirishwa nje ya nchi yetu. Ni kweli Hisa za Acacia zilishuka thamani kwenye masoko ya Hisa, lakini ni kweli kuwa ulimwengu wa masoko ya Hisa ulitikiswa na kushuka huko kwa thamani ya Hisa za Acacia?

Ni kweli kwamba jambo likifanyika hapa Tanzania "Dunia nzima" inafuatilia kile kinachofanyika hapa? Yaani kwa mfano tulipofanya mabadiliko ya matumizi ya Bandari yetu wasafirishaji wa dunia "Nzima" waliitisha vikao na kujadili nini cha kufanya kutokana na hatua hiyo?

Tanzania tumefikia hatua ya kutikisa dunia. Yaani sisi kwa Afrika ni zaidi ya Nigeria, Afrika ya Kusini, Kenya na nchi nyingine kama Misri?
 

Wapoti

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
2,821
2,000
Ni kweli tunafahamika Dunia nzima Kama kituo cha kujizolea utajiri kwa urahisi
 

Yellow bone

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
257
500
Ungesema Tanzania tunafahamika Said I dunian kuishi Marsha ya ujanja ujanja na uongo ningekubali
 

Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
944
1,000
Hakuna kitu kama hicho, nilishangaa pale nilipo jitambulisha kuwa natoka Tanzania, nikajibiwa, "where is it," "i never heard about that"
 

ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,777
2,000
kwenye ile komedi ya.jana ya eid komedi gala,nimegundua wauganda na wakenya wanatufuatilia na kutujua mpaka historia yetu. sijui nchi nyengine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom