Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,277
- 33,879
Huwa nawasikia CCM wakiongea ni kama vile jambo linalofanywa na chama chao hapa Tanzania huwa linaleta Mwangwi dunia nzima. Kwa mfano hata suala la Makinikia ilisemwa "magufuli atikisa dunia" kwa maamuzi yake ya kuzuia makinikia kusafirishwa nje ya nchi yetu. Ni kweli Hisa za Acacia zilishuka thamani kwenye masoko ya Hisa, lakini ni kweli kuwa ulimwengu wa masoko ya Hisa ulitikiswa na kushuka huko kwa thamani ya Hisa za Acacia?
Ni kweli kwamba jambo likifanyika hapa Tanzania "Dunia nzima" inafuatilia kile kinachofanyika hapa? Yaani kwa mfano tulipofanya mabadiliko ya matumizi ya Bandari yetu wasafirishaji wa dunia "Nzima" waliitisha vikao na kujadili nini cha kufanya kutokana na hatua hiyo?
Tanzania tumefikia hatua ya kutikisa dunia. Yaani sisi kwa Afrika ni zaidi ya Nigeria, Afrika ya Kusini, Kenya na nchi nyingine kama Misri?