Ni kweli simu feki zimezimwa au mikwara tu

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,788
3,028
mimi natumia simu ya mchina tena mchina ambao wamejitahidi kuutengeneza unajitahid kwa kweli kupiga kazi chakushangaza toka ile siku ya TCRA ilipofika hadi leo simu yangu bado inajinwaga itajavyo tuu wala haina tatizo lolote.
ni kweli hawa watu wamezima au wanaendelea wanavyodai wao?
naamanisha mchina au simu feki.
 
Wamezima IMEI tu ambayo haiendani na simu. Mfano ukiwa na mchina itel alafu ukataka kujua kama ni orijino utatuma hizo imei tcra then utapokeo ujumbe jina la kampuni ya simu iliyotengenezwa (itel) na model namba yake ambayo zinaendana then you are good to go. Tofauti na hapo imei namba yako inafungwa na hautaweza kupata mawasiliano ya mitandao ya simu yako.
 
mimi natumia simu ya mchina tena mchina ambao wamejitahidi kuutengeneza unajitahid kwa kweli kupiga kazi chakushangaza toka ile siku ya TCRA ilipofika hadi leo simu yangu bado inajinwaga itajavyo tuu wala haina tatizo lolote.
ni kweli hawa watu wamezima au wanaendelea wanavyodai wao?
Hivi mliambiwa zinazozimwa ni za wachina au simu feki? Siyo kila simu ya mchina ni feki
 
Mimi ninayo feki tena nilipotuma IMEI namba walinambia kabisa kwamba nifeki,,,ila mpaka saiv ndunda tu
 
Suala la kuzima simu feki ni kweli limefanyika ila kwa kiwango kidogo sana. Kama walivyosema zipo baadhi ya simu ni mfu hadi sasa lkn hapo hapo dola ikatoa onyo kwa mafundi simu kutojaribu kuziamsha hzo simu.
Kiuhalisi mamlaka husika hawasemi ukweli ni kwa kiasi gani zoezi hili lilivyo fanikiwa. Binafsi kwa macho yangu nilibahatika kuona simu iliyopoteza mawasiliano siku zile za mwanzoni ila baada ya muda ilikuja kupata mawasiliano kama kawaida.
Na mwisho muhusika mkuu wa kuona nani feki na nani halisi sii TCRA bali ni hawa network providers.
 
Back
Top Bottom