Ni kweli Rais Samia kayasema Haya?

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,393
Reaction score
10,153
Katika pita pita kwenye magazeti ya leo nikakutana na haya maneno kwenye gazeti mojawapo, eti kayasema Mama hivyo wamemnukuu akiongea na Makatibu katika mkutano mkuu wa kitaaluma.

"Uadilifu ni pamoja na kuweka siri za mahali ulipo, Kuweka siri za bosi wako na pale mazingira ya kazi ulipo sio wewe tena umemuona bosi kaingiza king'asti, kwanza unakitazama kwa jicho la kushoto pembeni"

Haya Magazeti jamani yasijekuwa yamemnukuu Mama vibaya...... ! Kama akili yangu inakataa kukubali kuwa huu ndio ushauri wa Mkuu kwa Watumishi..!
 
Kasema kweli hata mimi nimemsikia
 
Your browser is not able to display this video.
 
King'asti siyo mchepuko; king'asti ni neno la mtaani lenye maana ya "mtu ambaye una mahusiano naye ya kimapenzi"

Anaweza kuwa mpenzi wa kike au wa kiume.

Rejea pia wimbo Mr. Nice.. alimwimba king'asti wake

Nafikiri ujumbe wa Rais Samia ni "utunzaji wa siri na kuwa na heshima kazini"
 
Ndio madhabahu walizo amua kusimama nazo na uzinzi ni moja ya sadaka zinazoimarisha madhabahu sasa wafanyeje?

Na bado mazingira yanatengenezwa swala na uzinzi liwe swala la kawaida sana katika jamii ikiwemo mapenzi ya jinsia moja na utoaji mimba ni swala la muda tu nao si mrefu.
 
Kuingiza king'asti ofisini ni utovu wa nidhamu, kwahiyo haipaswi kifanywa Siri. Kama rais kayasema haya amekosea sana, maana ni kama anaufagilia ubatili.
Mwanawane Comment yako hii napigia mstari na kuboldi kabisa..!

Hatuwezi kuwa na Viongozi Wahuni wahuni ofisi ya Kazi, tena wengine ofisi za Umma wewe Unaingiza Ving'asti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…