NAAMINI
WOTE TUMESIKIA KISA CHA HUYU BWANA KUDAIWA kuhusishwa na wizi wa vifaa
vya magari.na naamini pia asilimia 90 ya wote waliosoma au kusikia
taarifa hizo wameamini kwamba huyu jamaa ni kibaka na hasa akihusishwa
na madawa ya kulevya.simtetei huyu jamaa lakini tumpe pia haki yake
kiubinadamu,katika yote hayo usikute huyu jamaa si mwizi na wala
hajihusishi na vitendo hivyo,inawezekana kabisa kwamba kwa namna ingine
kabisa amejikuta kahusishwa na hivyo vitendo bila hata yeye kuelewa
kaingizwa vipi,au la aliuziwa mojawapo ya vifaa vilivyoibiwa na ndipo
zigo la k**ba likamwangukia,na kwa bongo kila kitu
kinawezekana,nakumbuka niliwahi kupakaziwa nimebeba madawa ya kulevya
pale airport na wale jamaa eti usalama wa taifa waliniweka pale kwa
masaa matano mpaka wakalazimisha kuninyanganya baadhi ya pesa nizlizotua
nazo baada ya kugoma kutoa rushwa.walinivuruga akili kisaikolojia kiasi
kwamba nikapata ajali ya kufa siku hiyo hiyo baadae ila mungu akasaidia
nikapona.bado naandaa hicho kisa cha bongo ntakiweka hapa.kwa kweli
siku hizi naichukia Tanzania,maana siyo ile nilikua nikiimba naipenda
kwa moyo wote