Abu Ubaidah Commando
JF-Expert Member
- Sep 8, 2016
- 7,590
- 6,956
Hapa Afrika hususani Tanzania kuna imani za aina mbalimbali zihusuzo mambo tofautitofauti katika jamii yetu.Zimekuwepo tangu enzi na enzi na kadri miaka inavyokwenda nazi zinaendekea kuwepo ingawa sio kwa ukubwa huo.
Zipo imani kwenye vyakula(food taboos) mfano mama mja mzito na mayai.Wengine wanasema ukilala usiku na mfupa wa kitimoto wanga hawakusumbui!Sijui ikitokea mama mja mzito akamchukia mtu basi kuna uwezekano mkubwa akazaa mtoto anayefanana na huyo mtu!Ukimuona bundi ni dalili ya mkosi....na kadhalika na kadhalika.
Sasa kuna hii nyingine ambayo Kwangu ni mpya na imenishangaza sana.Sijui wenzangu kama mmeisikia au kuwatokea labda...
Kuna mzee wa makamo tulisafiri nae kwenye basi.Kwenye ile kuangalia mazingira kando ya barabara akaona nyumba moja ina miti ile mirefu inayokuwa na matawi kama ngazi ngazi(siijui jina kwakweli).Ni mizuri kimuonekano na inapendezesha Sana nyumba.Akaanza kudai kuwa mizizi ya hiyo miti ni mirefu na huwa inaingia ndani.Ikishakuwa hivyo nyumba yenye hiyo miti ni lazima afe mwanaume.Na pia migogoro ndani ya nyumba ya hivyo haiishi hasa ya mme na mke!Anashuhudia kuwa kuna rafiki zake wawili wameshafariki kabla hajajulishwa hiki suala.Pia kuna mama baada ya kufiwa na me wake akawa haelewani na watoto wake,hawapigi hata simu.Baada ya kutembea kwa wataalam(hapa naeleweka vizuri tuu!) akaambjwa aukate huo mti na kisha amwagie oili Ili kuua mizizi Iliyoingia ndani Baada ya kufanya hivyo watoto wake wakabadilika wakawa na mapenzi nae.Mzee anaongea kwa kujiamini kuwa anamaanisha anachokisema na akawashauri watu mule ndani kama wana hiyo miti wakaikate kabla haijaanza kuwaathiri.....
Je kuna mtu pia kawahi sikia kuhusu hili..ukweli ukoje maana hii dunia ina siri nyingi sana huwezi amini
Huo mti huitwa panga uzazi, wengine sijui huuita nini. Hata mimi nimesikia hayo, lakini sina uhakika.
Miti yote ya Mwenyezi Mungu, yeye ndie ameumba miti hiyo, sasa iweje mti huo uwe na madhara! Kuna jamaa zangu wana mti mkubwa ndani ya fensi, tena miaka, lakini hakuna kibaya kilichotokea.