Ni kweli kuna mgomo wa mafuta?

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,082
581
Wadau,

Naomba kuuliza, hivi ni kweli kuna mgomo wa mafuta. Maan nasikia kwenye baadhi ya vituo vya mafuta kuna foleni. Tangu jana niliona kuna email na sms zinazunguka kuwa kutakuwa na uhaba wa mafuta, Luku zitaadimika na dolar itapanda hadi 2000.Wadau mwenye data kamili naomba atujuze.

Nawasilisha
 
Kuhus mafuta sijui lakini kuhusu Dola itapanda zaidi ya sh 2000 kabla ya mwaka 2012.
Na wananchi tulivyo wehu tutakaa kimya tu bilakuchukua hatua zozote zaidi labda tutalalamika tu.
 
Kuhusu mafuta mimi sikuona mgomo, maana nilienda kwenye kituo Victoria Njia Panda Jeti mida ya saa kumi jana nikawekewa wese bila tatizo. Kuhusu LUK huenda kulikuwa na mgomo maana nilienda sehemu mbili nikaambiwa hakuna network. Kuhusu Dola, hiyo haitabiriki inapanda kila siku.
 
Back
Top Bottom