Vyombo vya habari vya Afrika kusini vimetangaza kwamba ingawa Rais Kikwete amekuwa madarakani kama rais tangu mwaka 2005, ziara ya sasa itakuwa ya kwanza ya kiserikali. Imeelezwa pia ingawa Rais Kikwete ameshatembelea Afrika kusini mara nyingi, lakini hizo hazikuwa ziara za kiserikali kutembelea rasmi Afrika Kusini. Baadhi ya ziara zilikuwa kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya kimataifa nk. Imeripotiwa kwamba Rais ameongozana na ujumbe mzito wa Serikali na baadhi ya wafanya biashara kwa ajili ya kukuza mahusiano ya kisiasa na kiuchumi. Haikusemwa juu ya Rais Kikwete kuhudhuria birthday ya Madiba, kama ambavyo Cameron alisema neno la kumtakia kila la heri Madiba alipokuwa ziarani Afrika Kusini.