Nostradamus
JF-Expert Member
- Jun 8, 2009
- 392
- 6
Kila siku katika kipindi kirefu sasa,Watanzania tumekuwa tumejiingiza katika malumbano na mijadala isiyokwisha.Lakini mjadala uliotuyumbisha zaidi umekuwa ni mjadala kuhusu ufisadi.
Kikubwa kinachonivutia katika mjadala huu ni kwamba wengi wetu tumeshindwa kujiangalia na kujikagua kama kweli kwa nia ya dhati tunastahili kulaani ufisadi.
Hivi kwani fisadi ni nani???? kwa tafsiri yangu ni kwamba" fisadi ni mtu yeyote anayetumia dhamana aliyokabidhiwa na wengi ili awatumikie kwa maslahi binafsi na kuwanyonya wale waliomtuma"(Mwanasiasa,daktari,askari, mhandisi,mkandarasi,mbunge, waziri ,raisi na hata mameneja au wakurugenzi wa mashirika ya umma)
Kwa mantiki hiyo basi,viwango vya ufisadi vinatofautiana kutegemeana na nafasi ya mtu kiutendaji na aina ya shughuli anayoifanya
Just imagine:----
umeajiriwa kwa makubaliano kwamba utaingia kazini saa1:30 asubuhi na utatoka kazini saa10:30 jioni,kwa siku tano za wiki,jumatatu hadi ijumaa.
Lakini badala yake unaingia kazini saa 3 na kutoka saa 9:30 huku muda mwingi ukitumia kunywa chai,kupiga simu za kifamilia,kuchat na marafiki kwenye chat zones,kupiga soga,lunch, na zaidi ni kuchangia hoja katika jamii forums.
Yote niliyoyaorodhesha hapo juu kumbuka hayapo kwenye mkataba wako wa ajira na yana-consume big ammount of your working time.mwisho wa siku unadai nyongeza mshahara huku kwa kigezo maisha yamepanda.
hivi tujiulize,ni nani kati yetu ambaye akikabidhiwa nafasi ya Rostam Aziz, "awe na uwezo wa kuteta na Raisi wa nchi muda wowote,awe na nguvu katika uteuzi wa mawaziri,awe amenunua idadi kubwa ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama tawala,awe na wafuasi walio tayari kujidhalilisha na kudhalilisha wenzao kwa maslahi ya huyo bwana.
Je ni nani atayefanya kinyume na anavyofanya huyu bwana leo hii? Au tutafanya zaidi yake.
Siku yule dada aliyekamatwa kwa kosa la uzinzi,alikuwa anaenda kupewa adhabu inayomstahili ambayo ni kupigwa mawe hadi afe, ndipo Bwana Yesu akawaambia" asiyetenda dhambi hii na awe wa kwanza kurusha jiwe" wote tunafahamu nini kilitokea.
Ushauri wangu ni kwamba... Kizazi hiki cha watanzani kimeshaharibika kwa rushwa,uonevu,uzinzi,ubakaji, tamaaa na mbaya zaidi wivu na husda.Na wengi wetu tunaopiga kelele dhidi ya ufisadi ni kwa sababu tumekosa fursa ya kuwa mafisadi na endapo tukipata fursa tutakuwa mafisadi zaidi ya hawa wa sasa.
Tumuombe mungu ashushe gharika na kufuta hiki kizazi chooote au laa basi atokee mzalendo wa kweli atakayepokonya nchi hii toka mikononi mwa wanasiasa(demokrasia) na kuitawala kidikteta huku akitanguliza maslahi ya taifa mbele na sio maslahi yake binafsi.(rejea utawala wa FIDEL CASTROL.MUAMMAR GADDAFI,ROBERT MUGABE au ADOLF HITLER)
nawasilisha hoja...