Elections 2010 Ni kweli CCM walitaka kumhonga Askofu Mokiwa?

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Leo asubuhi nilisikia kwenye redio Free Afrika katika mapitio ya magazeti kwamba Askofu Mokiwa alilalamika kuwa alipelekewa rushwa ya shilingi milioni 11 ili kunyamazisha baada ya ile kauli yake ya kukemea rushwa.
Wale waliokuwa kwenye ibada hiyo tunaomba habari kamili.
 
Jamani hakuna mtu kasikia habari hii au kuisoma katika gazeti lolote leo atuwekee vizuri hili?
 
Jamani hakuna mtu kasikia habari hii au kuisoma katika gazeti lolote leo atuwekee vizuri hili?

MU!
Hii habari nilishaitundika hapa lakini cha ajabu watu waliikacha kiaina. Ni kutoka gazeti la mwananchi...

Askofu Mokiwa akataa rushwa ya Sh11 milioni

SIKU 16 kabla ya kufanyika wananchi kupiga kura, askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa amedai kuwa hivi karibuni alipelekewa rushwa ya Sh11 milioni na mtu asiyemfahamu ili asizungumze masuala ya uchaguzi.

Dk Mokiwa alisema hayo kwenye tamasha la kuombea uchaguzi mkuu lililoandaliwa na Usharika wa Yombo wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Dar es Salaam jana.

Alisema tukio hilo lilitokea siku moja baada ya watu wawili mmoja akiwa anamjua kwenda nyumbani kwake kwa lengo la kumsalimia ambapo alizungumza nao kisha wakaondoka.

"Siku moja baadaye, mlinzi alinipigia simu akaniambia yule mgeni wa jana ameleta ….nikamwambia kwa nini ulichukua? sina ahadi na mtu yeyote kuniletea mzigo," alisema Dk Mokiwa.

Alifafanua kuwa taarifa hizo zilimlazimu aende nyumbani kwake ili kujua nini kimeletwa... na alipofungua alikuta fedha taslimu Sh11 milioni ambazo zilimtia wasiwasi.

"Nikampigia yule ninayemfahamu nikamwambia njoo uchukue fedha za jamaa yake, akaniambia 'usiwe na wasiwasi', nikamwambia haiwezekani njoo akaja akachukua zile fedha," alisema.

Aliongeza kuwa alikumbuka maneno ya mtu yule wakati walipokwenda nyumbani kwake kuwa nyinyi (viongozi wa dini) mkizungumza nchi inatikisika, akaona ile ilikuwa ni rushwa ili anyamaze kuzungumzia masuala ya uchaguzi mkuu ujao.

Alisema aliamua kukataa fedha hizo kwa sababu alikuwa na wasiwasi asije baadaye akaambiwa na yeye alipewa fedha za rushwa na kumalizia nyumba yake kwani ile kwake ilikuwa ni rushwa ili anyamaze.

Akizungumzia hoja yake iliyopingwa na taasisi za serikali zinazohusiana na rushwa na uchaguzi kwa madai kuwa anahamasisha watu kupokea rushwa, Dk Mokiwa alisema:

"Mimi sikuhamasisha rushwa ila nilikuwa nawapinga viongozi wabaya wanaotoa rushwa kwa wapiga kura. Sheria ya Gharama za Uchaguzi si mbaya, lakini wasimamizi wa sheria hiyo ndio wabaya," alisema Dk Mokiwa.

Alidai kuwa atafanya awezalo kuhakikisha kuwa viongozi wala rushwa hawaiongozi nchi hii kwa sababu mwaka huu rushwa imeenea na wakati huu wa kampeni rushwa ndio inaliwa sana na viongozi wasiokubalika ndio watoa rushwa.

"Tunamuomba Mungu leo, tupate viongozi ambao hawajawahi kutuongoza nchi hii; viongozi watakaotuletea amani bila ya kuwepo polisi shirikishi kwa kuwa hapa tulipofika ni matokeo ya kuwapa ushirikiano viongozi wabovu," alisema.

Akizungumzia kauli ya vyombo vya usalama juu ya amani kulekea kwenye uchaguzi, Dk Mokiwa alisema ili kulinda amani iliyopo hakuna budi vyombo hivyo vikatenda kazi yake bila ya upendeleo katika kusimamia uchaguzi.

"Nani alisema hakuna amani, tatizo ni vyombo hivi vinataka kuwalinda watu waendelee kuongoza wakati wananchi wamewachoka. Wanatakaiwa wawe fair katika usimamizi," alisema.

Kutoka Askofu Mokiwa akataa rushwa ya Sh11 milioni
 
Jamani weeeee wamehongwa watu hata kufikia kuhonga maaskofu ? Aiseeeeeeeeee eti ngapi?
Mi nawambia baada ya uchaguzi lazima waliochezea pesa yetu tuwashitaki!
 
Back
Top Bottom