Ni kweli ccm ilivunja katiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli ccm ilivunja katiba?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rugumye, Dec 14, 2010.

 1. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanajamii ni kweli CCM ilitakiwa kufutwa kwa mujibu wa katika ya jamhuri wa Muungano wa Tanzania ibara ya Ibara ya 20-(2) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake;-
  a) Kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya;-

  i. Imani au kundi lolote la dini.

  Na 19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
  (2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri yaMuungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya kazi za serikali.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mmmh, wako wapi wanasheria wetu watuwekee wazi!
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160

  hapo ndiyo kisiki cha mahakama ya kadhi?
   
 4. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wanasheria tupeni mawazo yenu kwa mjibu wa taaruma zenu pia.
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo lililopo Tanzania Wasomi hawatumii elimu zao katika kazi...Sasa ni wajibu wa wana sheria hapa kukaa na kutusaidia katika mambo muhimu kama haya
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,396
  Likes Received: 3,722
  Trophy Points: 280
  Malaria sugu, Mahmud, Dar na wengine................ mchango wenu wa kimahakama ya kadhi tafadhari juu ya hoja hiyo hapo juu. HIVI BILAL HAJAVUNJA KATIBA KUSEMA SERIKALI ITACHUGHURIKA NA UANZISHWAJI WA MAHAKAMA YA KDHI...?? Maana hiyo ni shughuri ya kidini na katiba yetu inakataza serikali kujishughurisha na mambo ya kidini
   
 7. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  MS hana MAHABA ya kuweza kulijadili jambo hilo na hasa kipengele cha cha katiba kuhusu secularism na non sectorialism iliyopo Tanzania
   
 8. d

  dotto JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mahakama ya Kadhi haiwezi kuanzishwa bila ya kubadili katiba iliyopo na Itasomeka hivi '.... Na.19.(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa shughuli za kiislamu peke yake zitakuwa ndani ya kazi za serikali isipokuwa dini zinginezo na jumuia zake ndogondogo nje na uislamu zitakuwa nje ya kazi za serikali'
   
 9. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kumbe Msingi wa mgawanyiko wa udini Tanzania ulijengwa kwenye ilani ya CCM mwaka 2005, basi chairman wa CCM asitafute mchawi wa chanzo cha mgawanyiko wa udini Tanzania. sijui km nipo sahihi wana jamii nisaidieni.:embarrassed:
   
Loading...