Picha inayoonesha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akiwa uwanjani amevaa jezi ya Argentina imekuwa ikisambazwa mtandaoni akidaiwa kushabikia Argentina katika mechi ya Kombe la Dunia 2026 kati ya Argentina na Austria.
Ni upi uhalisia wa picha hiyo?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI), na siyo tukio halisi.
Picha hiyo ilisambaa kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii ikidai kuwa Netanyahu alihudhuria mechi iliyochezwa Juni 22, 2026 kati ya Argentina na Austria huko Dallas.
Hata hivyo, nyenzo ya kuthibitisha picha ya
OpenAI ilibaini kuwa picha hiyo ina alama ya SynthID, teknolojia inayowekwa kwenye maudhui yaliyotengenezwa kwa AI. Mfumo huo ulithibitisha kuwa picha hiyo ilitengenezwa kwa kutumia zana za OpenAI.
Mbali na hilo, zana nyingine za uchambuzi wa maudhui ya AI, ikiwemo
InVID-WeVerify,
Hive Moderation pia zilibaini kuwa kuna ushahidi mkubwa unaoonyesha picha hiyo ni ya kutengenezwa kwa AI.
Aidha, rekodi za shughuli rasmi zinaonyesha kuwa siku hiyo Netanyahu hakuwa nchini Marekani. Alikuwa
Jerusalem akiendesha mikutano ya kikazi, ikiwemo kukutana na Željka Cvijanović.