Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,570
Hali itaendelea kuwa mbaya endapo serikali haitaacha kukopa benki za ndani. Wachambuzi wa maswala ya pesa wanasema endapo mabenki yatapungukia pesa za kuwakopesha watu/makumpuni yenye miradi ya uzalishaji; pato la Taifa litapungua na hivyo kufanya makusanyo ya kodi yashuke. Hii ndio hali iliyotokea ulaya; mabenki yalipungukiwa na mitaji ikapelekea miradi ya uzalishaji kukosa mitaji na ndiposa GDP ikashuka na serikali zao kufilisika (mapato ya serikali hayatoshelezi kulipia gharama za uendeshaji + madeni makubwa).
Suluhisho mojawapo ya kujikwamua na kufilisika kwa Serikali yetu kamwe Serikali isikope mabenki ya ndani ili pesa zilizoko kwenye benki zielekezwe kwenye miradi ya uzalishaji hivyo kuinua pato la Taifa (GDP).