Ni kweli balozi zetu nje ya nchi zimeishiwa fedha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli balozi zetu nje ya nchi zimeishiwa fedha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Feb 14, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Balozi ziko hoi kifedha. Ni taarifa iliyowekwa wazi na vyombo vya habari leo. Hii taarifa imekaaje?

  Tusaidiane kutafuta ufumbuzi, matusi tuweke pembeni. Tujenge hoja namna ya kujinasua na hali hii.


  CHANZO: NIPASHE 14 FEBRUARI, 2012


  MABALOZI WA TANZANIA HOI

   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nitaamini kuwa Hazina wameishiwa pesa kwa kwa kutumia case study ya jimbo la Arumeru!...kama sitaona ugawaji wa fedha na t-shirt na mabango ya 'chagua chama Mama'...basi nitajua hooooi !
  Kwa kauli zao za kawaida hawaaminiki hawa!
   
 3. n

  ngokowalwa Senior Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatua mojawapo iliyochukuliwa ni kupunguza idadi ya watu wanaoambatana na Mhe. Rais kwenye ziara zake nje ya nchi , hili yeye mwenyewe kaliona na ameshatoa maelekezo kwa wizara ya mambo ya nnje kwa utekelezaji. kwa kuzingatia freq. ya safarari hizi ni kubwa pesa za kuhudumia balozi zetu zitapatikana
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni habari za kweli au ni siasa za kuchafuana?
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Asante kwa mchango wako. Ni suluhu mojawapo.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  ni kweli govt imefilisika!mkulo,ngeleja ni mzigo mzito kwa jk!
   
 7. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  TFDA wamelipwa mshaara wa January, tarehe 8 February.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Magazeti yameripoti, je magazeti yametoa wapi taarifa hii? tujue chanzo kwanza ndiyo tutajadili vizuri... vinginevyo tunaweza kujikuta tunajadili uongo tu hapa.
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ukweli ni kwamba serikali imeloweka na JIK
   
 10. +255

  +255 JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Hizo zitakuwa fedha za chama sio za serikali
   
 11. +255

  +255 JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Aliyesema hayo ni katibu mkuu wizara ya mambo ya nje, wakati akizungumza na kamati ya bunge ya hesabu za serikali..
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ha ha haaa!
  Mpaka wa chama na serikali uko wapi?...USHAWAHI KUUONA?
  Hukuwahi kuona magari ya STK yanatolewa namba na kuwekwa T432 CCM?
  Au unaamini chama kiliacha kushika hatamu!
   
 13. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi kubwa za ulaya zina matatizo makubwa ya kifedha, ugiriki hali mbaya wanapunguza ajira na mishahara, sasa cha ajabu nini kwa nchi ombaomba kama tanzania?
  Hizi mada nyingine hazina kichwa wala miguu, wewe utakuwa umesoma chuo kikuu cha kata tu
   
 14. S

  Shembago JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muwe mnaangalia na Channel za kidini mambo haya yametabiriwa na si kwa TZ tu,nchi kibao uchumi utaumba to the maximum kiasi kwamba kutakuwa na limit ya kutumia hela.Ole wao waliozoea kutumia hovyohovyo,mtalazimishwa kuwa na nidhamu za matumizi yenu.Matokeo haya ni kutokana na reaction za seikali au mtu binafsi kwa wale wanaonekana wanafanya makosa,baada ya kuwarudisha katika mstari,Tiba tunayowapa ni makosa juu ya makosa! tafakari,Chukua hatua!
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  KWA sasa napita tu.
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani hiyo habari umeisoma au umeamuwa kufanya kijamiijamii tu? Naamini ungeisoma basi tungekuwa tunaendelea na mjadala badala ya kurudi nyuma.
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Unataka kutwambia tusijadili matatizo yetu eti kwa kuwa wengine wanayo kama hayo? Tuendelee na mada yetu na hasa hili la ziara za viongozi zinakula pesa nyingi kiasi kwamba ungekuwa wazi matumizi yanayofanyika kwenye ziara hizo basi tungeemewa sote!
   
 18. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mi sioni ajabu. Walikojazana waumizane huko huko.
  Na bado mgomo wa waalimu.
   
 19. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hata kama Balozi zikiishiwa sioni kuwa ni suala la kuniwangisha kichwa hata kidogo. Anayetakiwa asumbuliwe na hili ni jk na serikali yake, sisi wengine tusumbuliwe tu na mawazo ya mlo wa watoto wa jioni.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  TAARIFA YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KUHUSU MALIPO YA MISHAHARA KATIKA BALOZI ZETU.


  Tarehe 13/2/2010 Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilifanya kikao cha pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili taarifa ya Hesabu za Wizara kwa mwaka wa fedha 2009/2010.

  Kufuatia kikao hicho baadhi ya vyombo vya habari vilitoa taarifa ambazo siyo sahihi kufuatia masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho.

  Wizara inakanusha taarifa hizo zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari, na sio kweli kwamba Balozi zetu zina matatizo makubwa ya kifedha.

  Kilichozungumziwa katika kikao hicho ni kuwa Balozi zetu bado zinatumia viwango vya Posho ya Utumishi wa Nje ambavyo vimepitwa na wakati. Ili kuhakikisha kuwa viwango hivyo vya Posho ya Utumishi wa Nje vinaboreshwa ili kuendana na hali halisi ya maisha; Awali Wizara ilifanya mapitio ya Kanuni za Utumishi wa Nje (Foreign Service Regulations) zinazohusisha Posho ya Utumishi wa Nje na kuziwasilisha katika mamlaka husika. Kwa kuwa mapitio Kanuni hizo ziliandaliwa muda mrefu uliopita, Wizara iliona kuwa upo umuhimu wa kuunda kamati maalum ya kupitia kanuni hizo za Utumishi wa Nje. Kamati hiyo imeshakamilisha kazi yake na kuiwasilisha kwa Menejimenti ya Wizara kwa ajili ya uhakiki na hatimaye kuiwasilisha katika mamlaka husika.

  Pamoja na kuwepo kwa changamoto hiyo ya kuwa na viwango vya Posho ya Utumishi wa Nje vilivyopitwa na wakati, Balozi zetu zimeweza kupelekewa mishahara yao ya kila mwezi pasipo kuchelewa. Aidha, tatizo jingine lililoelezwa ni upungufu wa Bajeti unaotokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya Fedha nyingine za Kigeni.

  Katika kuwezesha kutatua tatizo hili Hazina imekuwa ikilipa kwa wakati fidia inayotokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania katika kila kipindi cha robo mwaka.

  Kwa ujumla Balozi zetu zimeendelea kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kutumia rasilimali fedha zilizopo katika Bajeti. Aidha, siku zote Wizara imekuwa ikipata ushirikiano mkubwa kutoka Hazina katika kushughulikia masuala ya fedha Balozini.

  IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE
  NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

  14/2/2012
   
Loading...