Ni kweli BAHATI NJEMA ipo?

City Owl

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,300
7,170
Heshima kwenu wakuu..

Naamini mara kwa mara umewahi kuambiwa maneno kama vile
"Nakutakia usiku mwema"
'Nakuombea safari njema'
'Kila la kheri'
"Asubuhi njema" n.k. yote kwa lengo la kukutakia Bahati nzuri/hali njema..
Sasa Je,
1.Hizi wishes huwa na impact yoyote kwenye maisha ya kawaida? Mf. Ikitokea hata mtu mmoja hajakuwish good night, Je huo usiku unaweza kuwa mbaya kiuhalisia?

2. Je kuna mtu ambaye akikutakia hali fulani basi ni rahisi kwa hali hiyo kutokea? Mfano. Mama mzazi akikutakia good luck kwenye interview ya kazi, Je utaipata kirahisi kuliko jirani tu akikuwish?

3. Je yaweza kuwa kwamba the more the good luck wishes the luckier you become?

Karibu share uzoefu wako nasi..
 
Anayesema "Mtu akikutakia Bahati Njema au Nzuri" inakuwa kweli, ajibu hapa.
Wale wanaoenda vitani, na huku nyuma wakiwa wameagwa kwa kuambiwa maneno yote mema/mazuri. Na wafikapo huko vitani, hupokea kipondo hadi kifo, hao nao wakae wapi?
 
Bahati njema ipo kwa kuzaliwa na wala siyo kwa mtu kukuwish,

watu hawawezi kukutakia bahati njema bali hukutakia baraka na mafanikio.

Wengine wanaiita random chance, yaani hutokea tu bila sababu yoyote. Kwa mfano; kuna watu wana bahati njema ya kupata pesa kwa njia rahisi, wengine bahati katika kupata kazi n.k
 
Back
Top Bottom