.Sikutegemea huyu mama kusema maneno haya kwa wakati huu, hasa akiwa amechaguliwa kama speaker wa bunge. Hili linanipa shaka katika ufanisi wake wa kazi, kwani ameanza vibaya kwa kutumia siasa za maji taka.
Wote tunajua kuwa suala la kuongelea kuhusu 'wizi wa mke wa mtu' ni nini na linamlenga nani. Hizi ni siasa za maki taka. Ni maji taka hayohayo ambayo yalitumiwa na viongozi wa ccm dhidi ya Dr. Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi. Kwa hili tunaweza kusema kweli kama atafanya kazi yake vizuri? La hasha! Leo hii hakuna haja ya kutafuta maana ya neno 'fisadi'. Kila mtu anajua hata mtoto wa darasa la 3 anajua.
Kwa kutamka hivyo hadharani, ameuhakikishia umma wa Kitanzania kuwa amewekwa pale kuetetea hoja za mafisadi, hakuna mjadala zaidi. Kama yeye alikuwa halijui hilo, basi imeliwa kwake! Sikuwa na imani na utendaji wa ccm tangu mwanzo, lakini hii imeniongezea kutokuwa na imani na Anna Makinda kama Speaker anayefaa.
Anafikiri watu hawana records cha alichoongea mwaka 2008 kuhusu ufisadi!
Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.
Unatakiwa ukiwa mwanasiasa uwe makini sana wakati unapoongea. Ukiweka kwenye context ya kisiasa nchini Tanzania kwa wakati huu, ufisadi unamaanisha ni wizi wa mali ya umma. Hiyo haina haja ya kwenda shule kujua hivyo. Kwa hiyo kusema kuwa huwajui mafisadi na kutoa tafsiri yako katika kamusi, huko ni kupoteza mwelekeo wa mazungumzo.Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.
Interested to know alichoongea!Anafikiri watu hawana records cha alichoongea mwaka 2008 kuhusu ufisadi!
Pasco said:Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.
Pasco,
..Mama Makinda ameulizwa kuhusu mafisadi kulingana na tafsiri ya neno hilo ktk siasa za leo za Tanzania.
..hivi ina maana akiulizwa kuhusu "vigogo" atasema ni vipande vya miti?
..hilo lilikuwa swali la mtego na kutokana na majibu yake amekwepa mtego mmoja na kutumbukia kwenye mtego mwingine.
..huyu ndiye anayedai kwamba amekuwa mbunge "maisha yake yote" halafu anashindwa kujibu maswali mapesi kama aliyoulizwa.
..so far naona kitakachomharibia Mama Makinda ni hii tabia ya kujibu maswali kwa jazba.
NB:
..Mama Makinda hakuwa kwenye timu ya kampeni ya uraisi ya Edward Lowassa mwaka 1995??
- You know what, tutalipeleka pabaya sana hili taifa kama tutadai kujua the meaning ya neno ufisadi as we want ndio should be our litimus test ya nani kiongozi anayefaa na asiyefaa, wananchi tufike mahali tukubali kwamba somebody had to be a new Speaker baada ya Mh. Sitta,
- Na ilikuwa ni lazima atoke kwenye chama chenye majority bungeni in this case CCM, sasa tumpe nafasi Spika mpya afanye kazi yake mpya kwanza ndio tumuhukumu!
William.