Ni kwanini watanzania ni wafupi wafupi ukilinganisha na raia wa nchi zingine?

Tujadili AKILI ya watanzania na sio urefu, ufupi.Wachina,Japani,Korea nk Hawatufikii urefu sisi Watanzania ila akili yao ina fanyakazi mpaka wazungu wanaweweseka. Urefu unafaida gani zaidi ya kukimbia riadha,mieleka,ngumi Kikapu.Akilu inafaida gani zaidi kuliko urefu, bora upate akili ukose urefu.
 
Ni tatizo la udumavu toka utotoni, unakuta kitoto chini ya miaka 5 kinashindia uji wa mhogo. Ukiona takwimu za udumavu kwenye website ya shirika la takwimu huwezi shangaa hiyo hali, na hapo watu wamekomaa kusafirisha samaki kwenda ulaya.
 
Wakati wa zama hizo wale wenye maumbo madogo walikimbia vita kwa majayant ndo Tanzania ilikua salama kwao ndo mana sisi ni waoga na wanyonge hata kutawaliwa sio tabu ni asili yetu
 
Hili nimeliona sana nje ya nchi na siku nikirudi nyumbani ndio huona huruma sana nkiingia mitaani.Lakini nimegundua kitu kimoja kuna ufupi wa dhiki ya maisha na ufupi kulingana na eneo mtu alipozaliwa na kukulia.Kwani watu wa milimani wana afya nzuri lakini ufupi kwao ni muhimu ili waweze kutembea huku na huko kwa urahisi na wale wa sehemu za tambarare pia lazima wawe warefu kwa ajili hiyo wasidhurike na vumbi kirahisi. Kwa kweli watanzania wengi pamoja na ufupi wao si wafyefye wana afya nzuri.Ukiona wafupi na wembamba sehemu za tambarare kama Dar es salaam ujuwe ni wale wagonjwa na waliokosa shibe au ni wahamiaji kutokea maeneo ya milima kama vile Mbinga na Lushoto.
 
Mbegu za warefu zilipelekwa ulaya kipindi cha trans Antarctic slave trade wazazi walio baki ni wafupi sie ndo wajuku wao
Sio wajukuu, ni vitukuu na vilembwe. Iliongezeka na lishe ya matobolwa, mchele unaooshwa maji mara tano, sembe ya kulowekwa nyeupe kama theruji, wasichana kuzaa hawajakomaa, nk nk.
 
Nina cm 173 je mm ni mfupi ama mrefu

Uzito wangu ni kg 71.

Ufupi na urefu visikutishe kiafya kinachozingatiwa ni BMI (body mass index) ratio kati ya urefu wako na uzito ulionao..
 
Back
Top Bottom