Ni kwanini siasa za vyama vingi zimepoteza mvuto tofauti na enzi za Kikwete na Mkapa?

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Hakuna kipindi ambacho siasa za vyama vingi zilikuwa zimepambana moto kama enzi za JK na Mkapa.

Kila nikikumbuka enzi za Ukawa, CuF ipo moto, NCCR mageuzi ipo moto, Chadema ipo moto, CCM nayo ipo moto mashabiki wa vyama wako moto, mijadala ya kisiasa, wanasiasa ilikuwa sio mchezo.

Lakini sio sasa hivi siasa za vyama vingi zimepoteza mvuto ule ushabiki haupo tena umebaki ushabiki wa mpira, siasa hawataki tena kusikia.

Je, nini kimepelekea?
 
Mtanzania gani mwenye akili tumamu anaweza kuvutiwa na siasa ambazo hazina usawa? Nani anaweza kuvutiwa na maigizo yanayofanywa na chama tawala?

Yaani utumie mamilioni ya shilingi kununua wabunge na madiwani wa upinzani, halafu baadaye ufanye uchaguzi wa marudio! Na watu hao hao wanagombea kwa chama tawala, na kushinda tena!!!
 
2007 mtu kaitwa fisadi,2015 siyo fisadi tumpigie kura...watz Wana akili,wanajua tu 'biashara' imefanyika
 
Hakuna kipindi ambacho siasa za vyama vingi zilikuwa zimepambana moto kama enzi za JK na Mkapa.

Kila nikikumbuka enzi za Ukawa, CuF ipo moto, NCCR mageuzi ipo moto, Chadema ipo moto, CCM nayo ipo moto mashabiki wa vyama wako moto, mijadala ya kisiasa, wanasiasa ilikuwa sio mchezo.

Lakini sio sasa hivi siasa za vyama vingi zimepoteza mvuto ule ushabiki haupo tena umebaki ushabiki wa mpira, siasa hawataki tena kusikia.

Je, nini kimepelekea?
Gia za angani zimeharibu Siasa za Tanganyika,nimeshudia Siasa za Tanganyika tokea enzi za akina Mrema NCCR mpaka wanapasuana huko Tanga, mpaka chadema,ila nilichogundua tanganyika hakuna mwanasiasa mkweli wote ni wanasiasa masilahi,labda Dkt Slaa kwa mbali, lakini akina Mbowe amna kitu,tokea chadema walivyomleta Lowassa ili awe mgombea wao,baada ya kutemwa na Ccm,tokea hapo niliona Tanganyika bado tunasafari ndefu sana,tokea gia ya angani ya Mbowe Cop,watanganyika wengi walikata tamaa sana na viongozi wa vyama vya upinzani.
 
Usipindishe ukweki, Magufuli ndio alikuja kuua hamasa ya siasa za vyama vingi hapa nchini. Alitaka kushurutisha ccm ipendwe huku akitumia ulevi wake wa madaraka kuhujumu vyama vya upinzani hasa cdm. Kwa bahati mbaya alichojaribu kukifanya kimeenda kinyume na kizazi hiki, maana kizazi hiki hakiikubali ccm, na wanahujumiwa wakionyesha kuwapenda wapinzani hasa cdm.

Dhalimu alitaka kuhadaa umma kuwa amerudisha uimara wa ccm, kumbe alikuwa anatumia madaraka yake kuendesha uhalifu dhidi ya umma ulioichoka ccm. Matokeo yake amesababisha wananchi kulidharau box la kura, na kutojihusisha na hamasa ya kisiasa, kwani hawaipendi ccm, na ni hatari kuwashabikia wapinzani.
 
Gia za angani zimeharibu Siasa za Tanganyika,nimeshudia Siasa za Tanganyika tokea enzi za akina Mrema NCCR mpaka wanapasuana huko Tanga, mpaka chadema,ila nilichogundua tanganyika hakuna mwanasiasa mkweli wote ni wanasiasa masilahi,labda Dkt Slaa kwa mbali, lakini akina Mbowe amna kitu,tokea chadema walivyomleta Lowassa ili awe mgombea wao,baada ya kutemwa na Ccm,tokea hapo niliona Tanganyika bado tunasafari ndefu sana,tokea gia ya angani ya Mbowe Cop,watanganyika wengi walikata tamaa sana na viongozi wa vyama vya upinzani.
Ni kweli walikata tamaa na vyama vya upinzani, je wameipenda ccm? Vyama vya upinzani sio cdm tu waliompokea Lowasa, je hivyo vyama vingine vya upinzani vilimpokea nani? Ukweli uko wazi, Magufuli ndio aliyeua hamasa za siasa hapa nchini, kwa kushurutisha watu wote kuikubali ccm, wakati nature haiko hivyo. Matokeo yake watu hawaipendi ccm, na hawana nafasi ya kuonyesha hisia zao kwa wapinzani maana ni hatari, na ari ya watu iko chini kuhusu siasa.

Madhara ya siasa za kidhalimu za magufuli zitachukua muda mrefu, ni labda yatokee mabadiliko ya kweli kwa njia ya amani, jambo ambalo si rahisi, ama machafuko au mapinduzi ya kijeshi Ili tuanze na katiba mpya isiyo na upendeleo kwa chama chochote Cha siasa. Tutashuhudia wapiga kura wachache kuliko maelezo kwenye chaguzi zetu, maana tayari box la kura limedharaulika, na sababu hasa ni utawala wa hovyo wa Magufuli
 
Wananchi wengi wana fikra za kiombaomba hivyo kutegemea viongozi wa vyama ndiyo wawasaidie badala ya wao kuwa sehemu ya kujiweka vizuri kisiasa na kiuchumi.
Bado fikra za kitumwa zimetamalaki, na ndiyo sababu leo kila mtu anamlaumu rais Samia na viongozi wa vyama vya upinzani.
Ni lazima wananchi wajue kwamba wana wajibu katika siasa ikiwemo kujiunga na vyama vyenye ilikadi, sera na fikra zinazofanana na za kwao.
Na kwa umoja wa fikra zinazofanana wawawajibishe viongozi badala ya kuwalaumu.
Ni muhimu wananchi wafundishwe kuwa kwa wingi wao wana nguvu dhidi ya viongozi wa vyama vyao, wa kitaifa na hata kupambana na mataifa ya nje.
 
Hakuna kipindi ambacho siasa za vyama vingi zilikuwa zimepambana moto kama enzi za JK na Mkapa.

Kila nikikumbuka enzi za Ukawa, CuF ipo moto, NCCR mageuzi ipo moto, Chadema ipo moto, CCM nayo ipo moto mashabiki wa vyama wako moto, mijadala ya kisiasa, wanasiasa ilikuwa sio mchezo.

Lakini sio sasa hivi siasa za vyama vingi zimepoteza mvuto ule ushabiki haupo tena umebaki ushabiki wa mpira, siasa hawataki tena kusikia.

Je, nini kimepelekea?
Wakati wa Mkapa na Kikwete ilikuwa ni rahisi sana kwa vyama vya upinzani kupata ajenda za kuzungumzia. Ajenda ungeweza kuzihesabu toka ufisadi mpaka watoto wa shule kusomea chini ya miti huku mvua ikinyesha.
Leo hii ajenda ni za kuokoteza toka DP World mpaka kwenye Uzanzibar na Utanganyika, sijazungumzia ajenda ya udini isiyo na mashiko mpaka mavazi ya mtu. Du kweli upinzani unakufa.

Sasa hivi ajenda ni za kuzitafuta sana na wapinzani wenye akili wameamua kukaa kimya kwa sababu Meli inaendeshwa vizuri.

Kwa mfano, Hivi Mama alivyoushikilia usukani na gari lishakwenda service, utamshika kwa kosa gani mpaka wananchi wakuelewe? Acheni, acha twende mpaka stesheni ya mwisho.
 
Shida njaa kaka.
Trust me kupitia wakina Joshua Nasari, Silinde, Mkumbo ,Yule wa shinyanga mjini, na wengine wote walionunuliwa na jpm.
Achana na mamluki akina zito na thelasin na mbatia ,toa hao kovid 19.
Raia saiz washaelewa ukwel kua siasa ya Tanzania ni biashara tu hakuna kumanisha Kama tunavyowaza.

Hata Mimi mwenyew nilikuawaga mfuas Sana wa Chadema ulikua huniambii kitu ,Ila kwasasa hata wakipita sehemu naona Kama nimepishana na wahuni fulani.
Tanzania hii tuna wapimzani wawil tu .
Nao ni Lisu na Mdude pekee wengine wote ni Malaya wa kisiasa na wengine wapo kazi maalum.

Washatuvunja mioyo raia
 
Wakati wa Mkapa na Kikwete ilikuwa ni rahisi sana kwa vyama vya upinzani kupata ajenda za kuzungumzia. Ajenda ungeweza kuzihesabu toka ufisadi mpaka watoto wa shule kusomea chini ya miti huku mvua ikinyesha.
Leo hii ajenda ni za kuokoteza toka DP World mpaka kwenye Uzanzibar na Utanganyika, sijazungumzia ajenda ya udini isiyo na mashiko mpaka mavazi ya mtu. Du kweli upinzani unakufa.

Sasa hivi ajenda ni za kuzitafuta sana na wapinzani wenye akili wameamua kukaa kimya kwa sababu Meli inaendeshwa vizuri.

Kwa mfano, Hivi Mama alivyoushikilia usukani na gari lishakwenda service, utamshika kwa kosa gani mpaka wananchi wakuelewe? Acheni, acha twende mpaka stesheni ya mwisho.
Gari inayofanyiwa service na mafundi ccm, hakuna kitu, subiri awamu ijayo ndio utaona madudu ya awamu hii, sasa hivi ni sifia sifia uteuliwe
 
Ni kweli walikata tamaa na vyama vya upinzani, je wameipenda ccm? Vyama vya upinzani sio cdm tu waliompokea Lowasa, je hivyo vyama vingine vya upinzani vilimpokea nani? Ukweli uko wazi, Magufuli ndio aliyeua hamasa za siasa hapa nchini, kwa kushurutisha watu wote kuikubali ccm, wakati nature haiko hivyo. Matokeo yake watu hawaipendi ccm, na hawana nafasi ya kuonyesha hisia zao kwa wapinzani maana ni hatari, na ari ya watu iko chini kuhusu siasa.

Madhara ya siasa za kidhalimu za magufuli zitachukua muda mrefu, ni labda yatokee mabadiliko ya kweli kwa njia ya amani, jambo ambalo si rahisi, ama machafuko au mapinduzi ya kijeshi Ili tuanze na katiba mpya isiyo na upendeleo kwa chama chochote Cha siasa. Tutashuhudia wapiga kura wachache kuliko maelezo kwenye chaguzi zetu, maana tayari box la kura limedharaulika, na sababu hasa ni utawala wa hovyo wa Magufuli
Wapinzani walijialibia wenyewe Magufuli ni kisingizio tu maana upinzani ni Sera sio blablaa,kama upinzani ungelikuwa imara wala Magufuli asinge uvunjavunja, Magufuli kakuta upinzani regelege wa kusubiria CCM wakosee ndipo wapate hoja, Magufuli alipoanza kushugulika wapinzani wakakosa hoja,hapo ndipo kifo cha upinzani kilipoanzia baada ya kujenga hoja wakaanza kejeli na kupinga kila kitu,kumbuka kuna vyama pinzani vilikuwa vimejipambanua kuwa ni vipigaji vita ya ufisadi nchini, Magufuli alivyoanza vita na mafisadi hakuna mwanasiasa au chama kilimunga mkono,sanasana walisema Magufuli anavita na matajiri maana hapendi matajiri,hata kwenye kurekebisha sheria za madini kuna wanasiasa walikejeli mpaka kuita tume za Magufuli rabbis h, ndipo wananchi wenye akili walianza kupuuza upinzani na wanasiasa masilahi.
 
Watu hawana imani na tume ya uchaguzi ie wanajua hata wakipiga kura bado haziwezi kuheshimiwa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Hapa hakuna cha tume wala nini, wapinzani hawaaminiki angalia Kenya tu hapo akina Odinga wako bega kwa bega na wananchi hata wakitangaza maandamano wako msitari wa mbele huku akina Mbowe na Lisu wanauraia pacha hadi family zao.
 
Wapinzani walijialibia wenyewe Magufuli ni kisingizio tu maana upinzani ni Sera sio blablaa,kama upinzani ungelikuwa imara wala Magufuli asinge uvunjavunja, Magufuli kakuta upinzani regelege wa kusubiria CCM wakosee ndipo wapate hoja, Magufuli alipoanza kushugulika wapinzani wakakosa hoja,hapo ndipo kifo cha upinzani kilipoanzia baada ya kujenga hoja wakaanza kejeli na kupinga kila kitu,kumbuka kuna vyama pinzani vilikuwa vimejipambanua kuwa ni vipigaji vita ya ufisadi nchini, Magufuli alivyoanza vita na mafisadi hakuna mwanasiasa au chama kilimunga mkono,sanasana walisema Magufuli anavita na matajiri maana hapendi matajiri,hata kwenye kurekebisha sheria za madini kuna wanasiasa walikejeli mpaka kuita tume za Magufuli rabbis h, ndipo wananchi wenye akili walianza kupuuza upinzani na wanasiasa masilahi.
Ni kweli Magufuli alianzisha hivyo vita dhidi ya mafisadi mpaka mahakama ya mafisadi ikaanzishwa lakini nani amewahi fungwa na mahakama hiyo tangu ianzishwe mwaka 2017 ?Huoni hizo ni comedy!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli Magufuli alianzisha hivyo vita dhidi ya mafisadi mpaka mahakama ya mafisadi ikaanzishwa lakini nani amewahi fungwa na mahakama hiyo tangu ianzishwe mwaka 2017 ?Huoni hizo ni comedy!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Sio Comedy ndugu, ili vita yako unayopigana hifanikiwe inaitajika kuungwa mkono jamii unayoishi nayo, Magufuli Vita alikuwa ya ufasadi alipigana peke yake, wanasiasa masilahi walianza kejeli nakusema anaonea matajiri maana hapendi matajiri, lakini angalau tuliona akina Lugemaria na wenziwe ambao walikuwa hawagusiki waliguswa, mpaka wengine wengi wameachiwa na Samia.
 
Hakuna kipindi ambacho siasa za vyama vingi zilikuwa zimepambana moto kama enzi za JK na Mkapa.

Kila nikikumbuka enzi za Ukawa, CuF ipo moto, NCCR mageuzi ipo moto, Chadema ipo moto, CCM nayo ipo moto mashabiki wa vyama wako moto, mijadala ya kisiasa, wanasiasa ilikuwa sio mchezo.

Lakini sio sasa hivi siasa za vyama vingi zimepoteza mvuto ule ushabiki haupo tena umebaki ushabiki wa mpira, siasa hawataki tena kusikia.

Je, nini kimepelekea?
Jiwe ndio alikuja kualibua system.
 
Back
Top Bottom