Salaam kwenu Wanajukwaa,
Imezoeleka ama sijui ni utamaduni ama sifahamu kama ndivyo tulivyokariri, Wakristo wengi Tunapokua Tunaomba Uwa Tunaomba hivi, Huu ni Mfano wa Maombi yangu "Mungu Wa israel, Mungu wa yakobo, Mungu Wa ibrahimu, Mungu wa eliya Nakuomba unisaidie katika jambo hili, unisaidie kama ulivyowasaidia kina sharack, meshack na abedinego na kuwaokoa kwenye tanuru la moto"
Huo ni mfano tu wa jinsi ambavyo nimekariri namna ya kuomba, yakwamba kama nataka ku-emphasize kuwa Mungu anisaidie lazima nipite humo kwenye hayo majina Tajwa hapo juu.
Swali langu ni....?
Ni kwanini hatuwezi kusema Mungu wa
Mshana Jr au Mungu wa
Kapeace au Mungu wa
dronedrake au Mungu wa
Nakadori ???[emoji2955][emoji2955] kwasababu kama ni sababu ni kuwa Hao kina Yakobo, ibrahimu, isaka, eliya nk. Kuwa-emphasized ni kwasababu Mungu aliwaonekania. Mbona ata mimi Mungu ananionekania pia katika maisha yangu?? Au hili swala limekaaje labda??[emoji2955][emoji2955]
Anyway humu tuko wengi na wenye akili kubwa, wenye uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko platform Yoyote ile apa Tanzania na nchi nyingine nyingi sana, natumai Nitapata majibu.
Naomba kuwasilisha